Kifua kinaniuma ila sikohoi nikishindilia ngumi napata maumivu makali hata vidole tu nikigandamiza kifuani kifua kinauma chote Nina H paroll positive.
Pole sana.
Ningependa kueleza kuwa unahitajika kumwona daktari na kusikilizwa upya juu ya tatizo lako. Pamoja na kuwa na hao H.Pylori uwezekano kuwa na tatizo jingine pia upo.
H.pylori huweza kupelekea kuumizwa kirahisi kwa njia ya chakula. Hii huweza kuleta hali ya michubuko/gastritis au kuwa na vidonda vya tumbo.
Si kila mwenye H. Pylori positive ana vidonda vya tumbo na si kila mwenye vidonda vya tumbo basi ana H. Pylori.
Mambo ya kuzingatia:
1: H. Pylori huweza kutibiwa na kupona hospitali. Ila, usitumie dawa za kuondoa H. Pylori na kwenda kupima ndani ya si chini ya mwezi mmoja. Kwani, vichocheo vilivyotolewa na mwili huwa havijaisha mwilini. Pia, usiende kupima H. Pylori wakati unatumia dawa za kukontrol acid na gesi kwani huweza kuingilia mfumo wa kipimo na kufanya kuwa positive. Kaa siku saba bila kumeza dawa za acid na gesi ndipo uende kupima H. Pylori.
2: Unapomaliza dozi ya H.Pylori ni vyema kuendelea na dozi ya dawa za kukontrol acid kama wewe uliambiwa una gastritis au vidonda vya tumbo. Kwa muda gani, hutegemea na hali yako, daktaria takuongoza kwa hilo.
3: Kipimo cha kuaminika cha H. Pylori ni kile cha kupima kupitia CHOO TU. Na si zaidi ya hapo. Au sample iliyochukuliwa wakati wa endoscopy tu.
4: Si kila mwenye gastritis au vidonda vya tumbo anahitaji kutumia Heligo kit au antibiotics.
5: Zingatia maelekezo yanayoambatana na tiba yako. Ule au usile nini. Ufanye au usifanye nini.
Tiba njema.