Ndio maana nilimuuliza kama kaenda kupima hiyo damu na mkojo, alikwendaje kupima bila ya kumuona daktari? Halafu anakuja kuleta sijui ndio mada au hoja humu jf. Si kila jambo unauliza tuu bila ya kufuata utaratibu.
Kama unaumwa unamuona dakitari, unachukua vipimo wanavisoma halafu unapata ushauri. Sasa mtu mpaka una umri wa kuweza kuandika kwa kutumia tekinolojia halafu haujui utaratibu wa kujitibu?
Wakati mwingine huwa najiuliza hivi nyinyi mnaojiita wasomi mnadhani kila kitu utapata jibu kwa kuandika andika tu. Acha uvivu nenda hospitali!