Habari Wana JF,
Mke wangu anasumbuliwa na ugonjwa ambao unafanana na pumu lakini Hana historia ya kuwa na pumu.
Mwezi wa nne alibanwa na kifua, alikuwa anahema kwa tabu sana na akihema Kuna sauti kama ya filimbi ilikuwa inasikika.
Tuliangaika na matibabu baada ya kuugua kwa muda wa wiki moja akapona. Tuliangaika hospital kama tatu ambapo wengine walituambia pumu licha kukiri Kama Jana historia ya pumu haiwezi kuwa pumu na wengine walituambia ni allergy. Leo Asubuhi hali ile imemuanza tena.
Naomba ushauri juu ya hali hii yaweza kuwa ni ugonjwa gani?
Na tiba yake ni ipi?