Msaada: Hali ya Barabara Dsm - Kibiti - Lindi - Mingoyo - Masai - Nachingwea


Njia ni nzuri. Nilisafiri kwa bus la Manning Nice toka Nachingwea kuja Dar,tulitoka saa 2 asb. na kufika saa 11 jioni (Masaa 9). Njia sio mbaya hata kwa Gari ndogo unayotaraji kuitumia! SAFARI NJEMA!!
 
Usimpoteze shemeji yetu, tunamsubiri kwa hamu aje kujua kwetu, atujue na sisi tumjue. Au unataka ajifunze historia ya miaka ya 1990s kurudi nyuma kwa vitendo, Lindi-DSM siku 3-7.
Bila kupita nchinga atafurahia huko kwenu na samaki wakavu?
 
Usimpoteze shemeji yetu, tunamsubiri kwa hamu aje kujua kwetu, atujue na sisi tumjue. Au unataka ajifunze historia ya miaka ya 1990s kurudi nyuma kwa vitendo, Lindi-DSM siku 3-7.

Asante sana Shem Mkulu na Wadau wote.. kwa sasa nipo kwa wzaa chema katika kijiji cha Ruponda - Nachingwea nakula ugali wa muhogo kwa nyama ya Kanga na Nguruka. Hali ya barabara ni njema sana vile inapitika kwa gari za aina zote. Nitaleta picha na tathmini ya barabara mida mida.

HERI YA MWAKA MUPYA 2014 KWENU NYOTE...!
 

Ahsante Mkuu! Nadhani umeonja na Embe zetu huko! Umezipenda?..
 
Mkuu nafikiri wamekukaangia korosho kiasi na chupa ya uraka pembeni! Heri ya mwaka mpya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…