Kuzaa na wanawake tofauti ni kutafuta Matatizo

Mh. Upo vzr Sana umesomeka
 
Okay, kwahiyo mama watoto anapo olewa na bwana mwingine na baba watoto anapo oa mwanamke mwingine, hawa watoto wanastahili kulelewa na nani??

Kwanza kabisa hamtakiwi kuachana mnapokua tayari na watoto.

Ndoa sio nguo kwamba ikikubana ubadirishe.

Ndoa halisi inaanza pale mapenzi yanapoishia, hapo ndipo kiapo cha kufa na kuzikana katika shida na raha kinaposimama na kuchukua nafasi yake.

Mnapokua tayari mmewaleta binaadam (watoto) katika ulimwengu wa nyama kutoka huko rohoni kwenu kwa tendo lenu hamna budi kujipondaponda nafsi na kutulia na kutengeneza maisha ya baadae kwa ajili yako na family yako.

Watoto ni matokeo ya kilele cha juu kabisa cha hisia kati yenu, lazima walindwe, kuheshimiwa, kuthaminiwa, kuongozwa na kuandaliwa mazingira ya kuendelea mtakapo ishia ninyi.

Watoto wenu ni nyinyi wenyewe wa baadae.

Ndoa ni muunganiko mtakatifu na watoto ni baraka za nafasi nyingine ya uhai wako na Mkeo kuendelea kuishi kupitia wao hata baada ya kufa kwenu.

Na ndio maana kuingiliana kimwili kukaitwa Tendo la Ndoa na Ngono (kufanya matusi Kama kuku) ikaitwa haramu.

Tamaa za ngono Hazina chochote zaidi ya kuwa ni tamaa tu, nusu saa the wave is past!

Sasa why risk the well being of the future you kwa kuachana na fellow creator? You think such a step italeta Amani?

Ukiona Amani sasa inatamalaki, just brace yourself for the future you (wajukuu na vitukuu) one or some are bound to do what you did and a Pandora’s box will be open. It’s reality.

Unfortunately in this World, no Deed goes around unpaid.
 
Makofi mengi kwako
 
Wengine ni wewe na baba yako ambao si riziki
 
Wengine ni wewe na baba yako ambao si riziki
hahahahaaaa!
Mzee wangu ana wake wawili na watoto wake wa kiume tupo 13 na katusomesha. Nyumba ina wahandisi, wachumi, walimu, manesi, wanasheria na wakulima na wafugaji. Mimi mwenyewe nimefyatua vidume vinne (4) na dada yao moja (1) kwa mke moja baada ya kuponea chupuchupu kuwa padri (faza). Ndo nafikiria kuongeza msaidizi wa wife a.k.a mama mdogo wa watoto.
 
Huu ushauri kuntu kabisa. Nimeuchukua mazima. Asante sana kwa haya madini adimu.
 
Sio sifa kuzaa na wanawake wengi
 
Hilo wewe halikuhusu umeshatimiza wajibu wako wa kutia mimba wao wapendane wasipendane wewe haikuhusu, nani kakwambia watoto waliozaliwa tumbo moja wanapendana kuliko ambao hawajazaliwa tumbo moja na baba yao ni mmoja?

Emu acha zako mifano tunayo
Si tuko mitaani tunaona
 
Tena ukiwa na hela ndio watachukuana zaidi, yani ni ha wanawake wenyewe wawe na pesa zao ndio hawatachukiana
 

Ukifa ndio utajua Kama hela zinasaidia nini

Ukiachana na kifo Kuna muda watoto wataitajika kuishi na wewe kutokana na changamoto kwa mama zao

Btw wewe ni mwanaume mara nyingi huwa hamshindi home so hata watoto wenu hamjui wanaishii vipi

Sio dhambi kuzaa watoto wengi na mama tofauti but ni risk tena kubwaaa
 
Elezea risk inatoka wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…