Kaka hata mimi nipo Tuangoma na karibu nahamia huko. Kibanda changu kimeshafikia mahala pazuri. Uzuri wa kule serikali za mitaa kidogo zinafanya kazi nzuri kwani mitaa iliyokuwepo huwa inapishwa grader kila mara na hivyo kufanya kuwa ngumu kwa mtu kuvamia sehemu ya njia. Binasfi sikwenda hata Halmashauri kufanya uhakiki ingawa natambua kuwa si sahihi so kama uko na muda wakutosha na uko na mtu ni bora ukafanya hivyo. Kutokana na mwenendo huu mzuri wa Serikali za Mitaa, tunaamini kuwa hata upimaji utakapokuja wataturasimishia tu eneo letu kwakutupatia hati kwani kazi ya serikali siyo kufukuza hata pale watu walipojenga kistaraabu na majengo yakileo bali ni kuwafikishia huduma zakijamii na maeneo hayo wameshapatiwa. Yapo hata maeneo ya wazi yanayotambulika na serikali za mitaa kule bwana. Tatizo kubwa ambalo mimi baada ya kupata eneo kule Tuangoma nimelipata ni kuwa wenyeji wa kule wameshatambua kuwa eneo lao ni Hot Cake (na hii inatokana na uzuri wa nyumba zinazojengwa kule kwani nymba nyingi zinazonjengwa kule katika maeneo yasiyopimwa ni design ya Mbezi Beach, Masaki, Mikocheni etc maana hakuna uchafu kule) so wapo mataperi wengi ambao huuza kiwanja kimoja zaidi ya mara moja kwa kutumia wenyeviti wa serikali za mitaa tofauti. Imetokea kwa jirani yangu mimi harafu imetokea pia kwa jamaa mmoja ambaye aliuziwa open space. Ukiongea vizuri na hao wenyeviti wa serikali za mitaa wanajuwa mengi sana kwani hata ramani wanazo. Jihadhari na hilo tu. Karibu sana Tuangoma. Otherwise, kama ulivyoshauriwa na Doltyne hapo juu, ukienda pale pale Mtaa wa Tuangona au hata pale Mtaa wa Malela utapewa maelezo yakuridhisha kabisa na unaweza usitamani hata kwenda Halmashauri. Wale jamaa siyo waswahili kama wa Mwananyamala.