Ipi tofauti ya majukumu kati ya SUMATRA na LATRA?

Sumatra ilikuwa ni mamlaka ya kusimamia usafiri wa nchi kavu na majini. Mwaka 2018 ikagawanywa nchi kavu ikabaki Latra na majini ikawa Tasac.

Sumatra-Surface and Marine Transport Regulatory Authority ilipogawanywa tumepata Latra-Land Transport Authority hii majukumu yake kusimamia usafiri wa nchi kavu yaani barabara, reli na cable.

Majini kuna Tasac-Tanzania Shipping Corporation hii majukumu yake ni haya
(a) Kuhimiza usimamizi na shughuli za wakala za meli zenye ufanisi

(b) Kuhimiza shughuli za bandari na huduma za meli zenye ufanisi

(c) Kuhakikisha Usalama na Ulinzi wa shehena

(d) Kuhimiza na kutunza mazingira, usalama na ulinzi wa baharini na kutoa leseni za meli.
 
Asante sana

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…