Heko Watawanyika!

Omutwale

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2008
Posts
1,429
Reaction score
1,053
BAN ya Moderator naitaka leo. Ilimradi tu matusi yafike kwa Watawanyika. Niwatusi maneno makali, yatakayo waamsha usingizi wa pono. Tumetekwa na nani hata tusihamaki dhuruma kuu? Mbona hata misukule ufika wakati ikajitambua? Sie mateka haya tumetekwa staili gani tusitambue kama hatuko huru? Kodi twakatwa katika kila bidhaa na huduma, na bado hatuhoji maendeleo yako wapi? Nimekwenda hospitali hakuna huduma. Wanakufa walalahoi ambao wangepona, na wanapona walalahai ambao wangekufa! Shuleni tunazalisha majimuni wanaokwenda vyuoni kurudi mbumbumbu. Hawa ndio wasemekana kuwa nguzo ya Taifa la wapumbafu lijalo!

Haya Paw naomba BAN yangu




​
 
Last edited by a moderator:
Labda mimi kiswahili sikijui ila sioni kama umetukana umesema ukweli.
 
Ni kweli mkuu lakini hatuko wajinga tena!. Sema sisi tumekuwa wastaarabu mno.
 
Huoni Arusha wameanza kuwawajibisha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…