Nimeshuhudia Madr. Wengi sasa elimu yao wanaiweka upande na kuingia kwenye bishara hii ya kufanyia uperation wajawazito, operation huwa inafanyika kwa malipo makubwa kiasi cha laki6 kila mgonjwa. Ivi tuseme hawa maDr wameshindwa kabisa kutoa tiba na sasa wameamua kufanya biashara? Niliwahi kumpeleka mke wangu alikua mjamzito pale mikumi na nikaambiwa mtoto ameelekeza miguu chini kwaiyo akiwa tayari kujifungua afanyiwe operation ikaishia hapo hakuna tiba yoyote aliyopatiwa. Nilisafiri nikaenda dubai nikafika duka la dawa la kawaida nilipatiwa dawa zinaitwa folic acid na niliambiwa hizo zitamuweka sawa kila kitu mama na mtoto wake. Hii nchi ni ya ajabu sana ivi watu hawa wanaoitwa madr kukosa uzalendo na kazi zao inakuwaje? Akatumia hizi dawa kwa miezi 3 afya yake ikaimarika na akajifungua mtoto ana kilo4.3 kwa nji ya kawaida bila ya matatizo tunamshukuru mungu. Serikali tunaiyomba iwe inazianglia biashara hizi haramu pia.
Jodari,..kwa heshima na taadhima, haya uliyoandika hapa yanakufanya uonekane chizi...
1. Huduma ya upasuaji ama uzazi kwenye vituo vya serikali ni BURE. Wewe kutokana na kutaka 'better' service na utofauti, ulienda kituo binafsi (umesema mikumi). Yes huduma kwenye vituo binafsi ni ya kulipia. Ni huduma kama ilivyo huduma yoyote ile.
2. Laki sita pia ni hela ndogo sana kwa huduma ya upasuaji wa mke wako. Jaribu tu ku-google bei ya operation kama hiyo nje ya mipaka yetu, kisha urejee na kauli zako. Wangetakiwa wakuambia dola 3000-5000. Si unataka utofauti mzee wangu?
3. Kwamba mtoto ametanguliza miguu wakati wa uchungu??...kisha ukasafiri kwenda dubai, ukarudi ukamkuta hajajifungua wala kupata tatizo jingine ni aina nyingine ya uzandiki. Mwanamke hawezi kuwa kwenye uchungu kwa zaidi ya masaa 24 na mtoto akazaliwa salama,...talking from a proffessional point of view. Huyo mtoto na mama yake usingewakuta.
4. Kwamba maduka na hospitali za hapa kwetu hazina Folic acid???...ina maana kweli kwa kipindi choote cha ujauzito wa mkeo hakupewa FA??..maana hii ni dawa wanayokunywa kila siku tangu siku ya kwanza wakienda Antenatal clinic...sasa kama haipo Tanzania,..alitumia nini kipindi hicho chote??
5. Taarifa tu,..FA sio dawa,..ni Iron Supplement kumsaidia mama awe na kiwango cha kutosha cha damu,..pia inasaidia kupunguza risk ya congenita malformation. Haina kazi nyingine yoyote...waka HAIMGEUZI mtoto aliyekaa vibaya.
6. Kwamba umewanunulia akina dada wengi FA za uarabuni kwa kuwa za hapa kwenu ni unga,...tukuulize tu kuwa wewe ni mganga wa kienyeji??..ulijuaje kama ni hizo FA ndo zimewafanya wajifungue kawaida??..
Wakati mwingine, jaribu kusoma kwanza, una access ya internet,..jifunze, utaonekana mbumbumbu (no harm intended).
Kiukweli uliyoyaandika yanakutia aibu.
Kwa heri