KIUNGO wa kimataifa wa Brazil,
Deangelis Gabriel Barbosa (27)
aliyekuwa akisubiriwa kwa
hamu hatimaye amewasili jijini
Tanga na kupokewa kwa
shangwe na viongozi pamoja na
mashabiki wa Coast
Barbosa aliwasili Jumamosi jijini
Tanga akiwa na mkewe Zaira
Caroline na mtoto wao Lara
Barbosa na kutambulishwa
rasmi kwa waandishi wa habari
jana katika makao makuu ya
klabu hiyo yaliyopo barabara ya
12 .
Mbrazil huyo alisema amefurahi
kufika Tanzania mkoa wa Tanga
amefurahishwa na mapokezi
mazuri pamoja na kuahidi
kukata kiu ya mashabiki wa
klabu hiyo.
�Mimi na mke wangu
hatukutegemea kupata
mapokezi makubwa namna hii,
ninachoahidi ni kwamba
nitajitahidi kwa kiasi cha uwezo
wangu kuiletea mafanikio kwa
timu yangu ya Coastal Union,�
alisema Barbosa.
Akizungumza wakati
akimtambulisha, Makamu
Mwenyekiti wa Coastal Union,
Steven Mnguto alisema tayari
klabu yake ipo katika hatua za
mwisho za kukamilisha kibali
cha kumuwezesha kuchezea
Coastal Union.
�Barbosa amesaini mkataba wa
mwaka mmoja na ataanza
kuonekana uwanjani hivi
karibuni kwani tupo katika
hatua za mwisho za kukamilisha
vibali vya kumuwezesha
kufanya kazi nchini, lakini vibali
vingine kama ITC tumepata,�
alisema Mnguto.
Alieleza kufurahishwa na ujio wa
Barbosa na kusisitiza kuwa
amewasili wakati muafaka
kwani Coastal Union inamhitaji
kiungo mshambuliaji kama yeye.
Barbosa ametokea timu ya New
Road ya Nepal aliyojiunga nayo
mwaka 2010 pia amewahi
kucheza Paham Footbal Club,
Flamengo, Santa Cruz zote za
Brazil na Churchill Brothers ya
India, Maruinense pamoja na
Sport Club ya Jiji la Paulo Afonso