Unaona wenzetu wanavyotii na kuheshimu sheria? Ukiwa unayo nyumba yako hasa kama wewe ni mkazi wa the old city, ukitaka kuikarabati basi huna budi kuwasiliana na idara ya mambo ya kale ili waje wasaidiane na wewe kuchimba kwa wao kutumia taratibu zao za kitaalamu ili wakigundua vitu vifaa vya kale vinavyohusiana na historia ya Jerusalem waweze kuhifadhi. Sio sisi majengo yote ya zamani yaliyojengwa na Mjerumani ambayo yanamilikiwa na NHC na akina Manji yanabomolewa tu kama kazi mbele kwa mbele. Ah nchi yangu Tanzania. Haijui kabisa kuhifadhi hsitoria, Hatujui kabisa.
Hivi ni wangapi leo wanaojua kuwa Kibasila alikuwa chifu wa Wazaramo alieuwawa na Wajerumani kwenye mti ambao ulishakatwa siku nyingi na manispaa ya Ilala kukabidhi eneo ambalo sasa linatumiwa na wamachinga. Liko nyuma tu iliyokuwa Air Msae na KAMATA. So sad. Nobody and nobody cares at all.Nobody