SoC04 Uboreshaji wenye kuleta unafuu wa usafiri kwa watoto wa kitanzania (wanafunzi) na chakula mashuleni kote

Tanzania Tuitakayo competition threads

Skythelimit

Member
Jul 19, 2023
35
63
Awali ya yote nipende kutoa shukurani za kipekee kwa uongozi wa JF na wahisani wengine kuwezesha jukwaa hili kuwa kitovu cha mawazo mapana ya kuijenga nchi yetu ya Tanzania.

Nikienda kwenye mada ya namna ya kuboresha sekta ya usafiri ili iweze kuleta wepesi kwa watoto wa kitanzania kupata huduma hiyo pasipo mawaa yoyote.

Kwa wenyeji wa mikoa mikubwa nikimaanisha majiji na manispaa, mtaungana nami namna wanafunzi wa kitanzania wanavyoteseka barabarani ifikapo asubuhi watakapo kwenda mashuleni na jioni warudipo makwao.
Kwenye vyombo vya usafiri hasa hasa daradara, makonda huwakatalia kupanda kwenye gari zao, kukabana nao na matusi juu kwa "wakusoma" jina maarufu wanalowaita wanafunzi hao.

Adha watoto wa kitanzania (wanafunzi) wakutanayo barabarani:
  1. Watoto kukataliwa kupanda magari na hivyo kufika mashuleni kwa kuchelewa.
  2. Wakifika mashuleni saa 2 hadi saa 3 kwa kuchelewa wanakutana na adhabu kali kutoka kwa walimu wao.
  3. Shuleni wanatoka saa 8 au saa 9, nyumbani wanafika saa 12 au saa moja usiku kwa sababu tu, Makonda wanawakataa kwenye magari yao kwa kuwa mida hiyo ya jioni huwa ina wateja wengi wanaorudi majumbani mwao.
  4. Udumavu wa ubongo kwa watoto kutokana na mateso wanayopata kutokana na usafiri ambapo madhara yake yanakuja kuonekana kwenye ujana wao, wanakuwa ni vijana wasio jali utu na ubinadamu kwa wengine na hivyo matendo ya ukatili wa kijinsia kuongezeka katika jamii.
Kipi serikali ifanye ili kuboresha usafiri wa umma kwa wanafunzi:
  1. Serikali ianze mchakato wa upatikanaji wa magari ya umma kwa ajili ya kubeba wanafunzi wa kitanzania hasa mida ya asubuhi na jioni wanapotaka mashuleni.
  2. Najua unaweza kujiuliza serikali hii maskini inawezaje kununua magari ya umma kwa ajili ya wanafunzi tu!
  3. Jibu ni jepesi tu kupitia UPUNGUZAJI WA KODI kwa daradara maalum zitakazo wabeba wanafunzi hao kila siku za shule.
  4. Kitakacho fanyika ni kuwa TRA na mamlaka za Halmshauri zitaandaa mpango wa NUSU KODI kwa daradara zote zitazobeba wanafunzi wa kitanzania.
  5. Lakini kwa coaster na hiace zitakazo ingizwa kutoka nje, bandarini kwa ajili ya kutoa huduma hiyo maalum kwa wanafunzi nazo itabidi zipunguziwe kodi (import duty) ili zije zitekeleze mpango huu vizuri.
  6. Hii NUSU KODI ipo kwamba; kama daradara ilikuwa inatakiwa kulipa 100,000 kwa mwezi kwa mamlaka za mapato za halmashauri na TRA sasa itapaswa kulipa Tsh 50,000 tu kwa mamlaka hizo ili itoe huduma safi kwa wanafunzi wa kitanzania.
Mfumo daradara hizi maalum utakazo tumia ili kuboresha huduma hii ni:
  1. Daradara hizi maalum zitajisajiri kupitia mamlaka maalum ya usafiri kwenye halmashauri husika ili zipewe route ya kupita kwa ajili ya wanafunzi wote kila eneo.
  2. Daradara hizi zitapakwa rangi maalum ya NJANO kutoka chini kwenye maatairi hadi kwenye laini ya madirisha ya daradara hiyo. Hii ni kwa ajili ya kutofautisha daradara hizi maalumu za wanafunzi na daradara nyingine.
  3. Bei ya wanafunzi katika daradara hizi itabaki ile ile shs. 200.
  4. Kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 3 asubuhi, na mchana kuanzia saa 8 hadi saa 12 jioni huo ni muda wa wanafunzi katika daradara hizo. Hivyo Trafiki watasimamia hilo, mida hiyo wakikutwa abiria wa kawaida kwenye daradara hizo watalimwa faini. Hatutaki wanafunzi wa kitanzania wapate usumbufu kisa usafiri.
  5. Tofauti na mida tajwa hapo juu, daradara hizo zitaendelea kubeba abiria wa kawaida kwa ajili ya kujiongezea vipato vyao binafsi.
Tuhamie namna ya upatikanaji wa chakula bora kwa wanafunzi wote wa shule za umma.

Chakula ni muhimu sana kwa maendeleo ya wanafunzi wanapokowepo mashuleni. Usahihi wa majibu ya wanafunzi inategemeana pia ni kwa namna gani ubongo wake unapata chakula kwa muda muafaka wa kula.
Sasa hilo limekuwa changamoto kwa shule nyingi za umma, watoto hawapati chakula na wanasoma kwa muda mrefu sana huku wakibebeshwa mizigo mizito ya madaftari. Sidhani kama viongozi wetu wa serikali wanaweza kuvumilia watoto wao wasome bila kula katika shule wanazowalipia bei kubwa huko kwenye International schools.

Lakini tukumbuke mamlaka na uongozi hauangalii historia ya shule alizopitia kama International au KAYUMBA, kutoka shule yeyote mtu anaweza kuwa kiongozi wa taifa hili. Sasa tunatengeneza taifa la namna gani kama viongozi wetu wajao leo wanashinda njaa mashuleni bila kula! Tunategemea kupata viongozi wa namna gani? Si ni ongezeko la viongozi njaa na CHAWA ambao baadae wanatusumbua wananchi kwenye media kwa kusifia kila jambo ilimradi mkono uende kinywani!? Ukiangalia kwa makini vijana CHAWA wa zama hizi, ukirudi nyuma kwenye historia ya usomaji wao utagundua kwamba wote wamesoma St. Kayumba ambapo chakula shuleni kwao ilikuwa hawapati na hivyo njaa ile imeathiri ubongo wao hadi kwenye utu uzima wao.

Kipi serikali ifanye ili kuwezesha upatikanaji wa chakula kwa wanafunzi wote hasa wa shule za umma msingi na sekondari:
  1. Mbinu muhimu sana ni hiyo ya kucheza na mifumo ya kodi kwa kuwapunguzia kodi watoaji wa chakula mashuleni.
  2. Shule ambazo hazina majiko, zitenge hata madarasa shuleni kwa ajili ya kuwa majiko kwa ajili ya chakula cha watoto shuleni hapo.
  3. Makupuni kama MANJIS GAS, TAIFA GAS, au MERU GAS wapewe punguzo la kodi kwa wao wakifanikisha usimikaji wa mifumo ya majiko ya gasi mashuleni.
  4. Makampuni na wafanyabishara wahimizwe kuandaa mpango wa kulisha mashule, TRA iweke namna ya kuwapunguzia kodi makampuni hayo kwa kujirishisha kwamba misaada yao ya chakula imefika katika shule husika.
  5. Halmashauri kupitia kamati ya chakula mashuleni itahakikisha kila shule inapata mgao wa chakula kulingana na akiba iliyopo.
  6. Saa 7 kamili mchana masomo yata stop ili watoto wapate chakula cha mchana hadi saa 8:20 baada ya hapo watarudi darasani kumalizia vipindi double (dk 80) vya mwisho.
  7. Kwenye huo mulo wa wanafunzi, serikali itaandaa bajeti ya kulisha walimu wake nchi nzima ili kuendana na utoaji wa elimu pasipo kusumbuliwa na njaa. Na jua kuna mambo mengi muhimu walimu wa Tanzania hawapati ili siamini kwamba serikali inaweza kushindwa kuwapa hata pesa ndogo posho ya chakula kwa walimu ili waweze kutengeneza kizazi kijacho kilicho bora zaidi.
  8. Wazazi wa wanafunzi watapaswa kuchangia shs 5000 kwa mwezi kwa ajili ya kufanya huduma hii ya chakula iwe endelevu kwa wanafunzi wote. Hiyo ela itatumika kulipa wapishi watakao kuwa wanawapikia wanafunzi hao huko shuleni.
Faida ya uboreshaji huu wa usafiri na chakula kwa wanafunzi wa kitanzania:
  1. Ufaulu kuongezeka kwa sababu vile vipindi vya asubuhi walivyo kuwa wanavikosa, sasa watakuwa wanaviwahi kutokana na uwepo wa daradara hizo maalumu.
  2. Uelewa na maarifa ya wanafunzi wa kitanzania kuongeza maradufu kwa sababu sasa watoto wana hakika ya kupata chakula shuleni na hivyo akili zao kutulia kuhusu darasani.
  3. Idadi ya wanafunzi mashoga, machawa, wadangaji n.k itapungua kwa sababu wengi wao adha ya usafiri na njaa ndio huwapelekea kutumbukia kwenye matendo hayo.
  4. Uhakika wa kupata viongozi walio sahihi kwa ajili ya kusukuma maendeleo ya nchi yetu kwa sababu wataguswa na namna wananchi na serikali yao ilivyo waangaikia kwa makuzi yao yaliyo bora.
Maboresho hayo mashuleni yaendane sambamba na uboreshaji sera ya elimu kwa ajili ya kuwaingiza watoto wa mitaani hasa wa kwenye mastendi kurudi kwenye vituo vya elimu kwa ajili ya kupata elimu na maitaji yao.
Viongozi kuacha hawa watoto kwenye hali ngumu za maisha huku tukiacha nature ndio iamue hatma ya maisha yao itatugharimu sote kwa sababu watoto hao wa kimaskini, mitaa inawanywesha sumu na kutokuwa watu wanaojali juu ya jambo lolote.

Hivyo adui akiamua kutumia kundi hili la vijana waliotelekezwa toka zamani huko mashuleni kwenye makuzi yao wanaweza wakauwash moto nchi yetu hii nzuri Tanzania ikawa aikaliki. Watanzania, viongozi tuifikirie Tanzania yetu nzuri ijayo kwa kuwa hudumia watoto wetu wote walioko mashuleni kwa usawa na haki ili kama taifa tuje tujivunie watoto wetu wakipewa majukumu makubwa. Tusifikirie tu watoto wetu ila tutambue na tuone kwamba kila mtoto wa mtanzania mwenzako ni wako pia.

Utamkuza mtoto wako huko magetini kwenye mbwa wakali lakini siku akikua na kujitambua ana kuletea mkwe kutoka st. Kayumba ambayo mzazi halikuwa tegemeo lako. Hivyo tuboreshe hizo st. Kayumba ili vijana wengi walio bora watoke katika shule hizo ili watufae hata wakiwa viongozi wetu muda huo tukiwa tumezeeka.
 
  1. Serikali ianze mchakato wa upatikanaji wa magari ya umma kwa ajili ya kubeba wanafunzi wa kitanzania hasa mida ya asubuhi na jioni wanapotaka mashuleni.
  2. Najua unaweza kujiuliza serikali hii maskini inawezaje kununua magari ya umma kwa ajili ya wanafunzi tu!
  3. Jibu ni jepesi tu kupitia UPUNGUZAJI WA KODI kwa daradara maalum zitakazo wabeba wanafunzi hao kila siku za shule.
  4. Kitakacho fanyika ni kuwa TRA na mamlaka za Halmshauri zitaandaa mpango wa NUSU KODI kwa daradara zote zitazobeba wanafunzi wa kitanzania.
Hapa umeicheza vizuri, naona kama imewafaidisha wote. Mabosi, wanafunzi hadi walipakodi wote wame 'win'. Safi

Ukiangalia kwa makini vijana CHAWA wa zama hizi, ukirudi nyuma kwenye historia ya usomaji wao utagundua kwamba wote wamesoma St. Kayumba ambapo chakula shuleni kwao ilikuwa hawapati na hivyo njaa ile imeathiri ubongo wao hadi kwenye utu uzima wao.
Tunahitaji utafiti hapa. Unaweza kuta hawa ST. Kayumba uzalendo ukawa juu sana tu ukilinganisha. Lakini kinadharia, mzuri zaidi atakuwa ni yule amepita sehemu zote mbili International na Kayumba. Uzoefu muhimu bro. Mleta mada hapa sikupingi wala sikubali ila nasema tunahitaji utafiti.

Wazazi wa wanafunzi watapaswa kuchangia shs 5000 kwa mwezi kwa ajili ya kufanya huduma hii ya chakula iwe endelevu kwa wanafunzi wote. Hiyo ela itatumika kulipa wapishi watakao kuwa wanawapikia wanafunzi hao huko shuleni
Naipenda sana mifumo ya uchangiaji gharama. Inaongeza uwajibikaji na uwajibishaji kwa pande zote. Kitendo tu cha mzazi kusema mtaani kwamba 'Nimetoa hela yangu, msiniambie chakula hakipo' ina kamsukumo kazuri sana kwenye ajenda.
 
Awali ya yote nipende kutoa shukurani za kipekee kwa uongozi wa JF na wahisani wengine kuwezesha jukwaa hili kuwa kitovu cha mawazo mapana ya kuijenga nchi yetu ya Tanzania.

Nikienda kwenye mada ya namna ya kuboresha sekta ya usafiri ili iweze kuleta wepesi kwa watoto wa kitanzania kupata huduma hiyo pasipo mawaa yoyote.

Kwa wenyeji wa mikoa mikubwa nikimaanisha majiji na manispaa, mtaungana nami namna wanafunzi wa kitanzania wanavyoteseka barabarani ifikapo asubuhi watakapo kwenda mashuleni na jioni warudipo makwao.
Kwenye vyombo vya usafiri hasa hasa daradara, makonda huwakatalia kupanda kwenye gari zao, kukabana nao na matusi juu kwa "wakusoma" jina maarufu wanalowaita wanafunzi hao.

Adha watoto wa kitanzania (wanafunzi) wakutanayo barabarani:
  1. Watoto kukataliwa kupanda magari na hivyo kufika mashuleni kwa kuchelewa.
  2. Wakifika mashuleni saa 2 hadi saa 3 kwa kuchelewa wanakutana na adhabu kali kutoka kwa walimu wao.
  3. Shuleni wanatoka saa 8 au saa 9, nyumbani wanafika saa 12 au saa moja usiku kwa sababu tu, Makonda wanawakataa kwenye magari yao kwa kuwa mida hiyo ya jioni huwa ina wateja wengi wanaorudi majumbani mwao.
  4. Udumavu wa ubongo kwa watoto kutokana na mateso wanayopata kutokana na usafiri ambapo madhara yake yanakuja kuonekana kwenye ujana wao, wanakuwa ni vijana wasio jali utu na ubinadamu kwa wengine na hivyo matendo ya ukatili wa kijinsia kuongezeka katika jamii.
Kipi serikali ifanye ili kuboresha usafiri wa umma kwa wanafunzi:
  1. Serikali ianze mchakato wa upatikanaji wa magari ya umma kwa ajili ya kubeba wanafunzi wa kitanzania hasa mida ya asubuhi na jioni wanapotaka mashuleni.
  2. Najua unaweza kujiuliza serikali hii maskini inawezaje kununua magari ya umma kwa ajili ya wanafunzi tu!
  3. Jibu ni jepesi tu kupitia UPUNGUZAJI WA KODI kwa daradara maalum zitakazo wabeba wanafunzi hao kila siku za shule.
  4. Kitakacho fanyika ni kuwa TRA na mamlaka za Halmshauri zitaandaa mpango wa NUSU KODI kwa daradara zote zitazobeba wanafunzi wa kitanzania.
  5. Hii NUSU KODI ipo kwamba; kama daradara ilikuwa inatakiwa kulipa 100,000 kwa mwezi kwa mamlaka za mapato za halmashauri na TRA sasa itapaswa kulipa Tsh 50,000 tu kwa mamlaka hizo ili itoe huduma safi kwa wanafunzi wa kitanzania.
Mfumo daradara hizi maalum utakazo tumia ili kuboresha huduma hii ni:
  1. Daradara hizi maalum zitajisajiri kupitia mamlaka maalum ya usafiri kwenye halmashauri husika ili zipewe route ya kupita kwa ajili ya wanafunzi wote kila eneo.
  2. Daradara hizi zitapakwa rangi maalum ya NJANO kutoka chini kwenye maatairi hadi kwenye laini ya madirisha ya daradara hiyo. Hii ni kwa ajili ya kutofautisha daradara hizi maalumu za wanafunzi na daradara nyingine.
  3. Bei ya wanafunzi katika daradara hizi itabaki ile ile shs. 200.
  4. Kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 3 asubuhi, na mchana kuanzia saa 8 hadi saa 12 jioni huo ni muda wa wanafunzi katika daradara hizo. Hivyo Trafiki watasimamia hilo, mida hiyo wakikutwa abiria wa kawaida kwenye daradara hizo watalimwa faini. Hatutaki wanafunzi wa kitanzania wapate usumbufu kisa usafiri.
  5. Tofauti na mida tajwa hapo juu, daradara hizo zitaendelea kubeba abiria wa kawaida kwa ajili ya kujiongezea vipato vyao binafsi.
Tuhamie namna ya upatikanaji wa chakula bora kwa wanafunzi wote wa shule za umma.

Chakula ni muhimu sana kwa maendeleo ya wanafunzi wanapokowepo mashuleni. Usahihi wa majibu ya wanafunzi inategemeana pia ni kwa namna gani ubongo wake unapata chakula kwa muda muafaka wa kula.
Sasa hilo limekuwa changamoto kwa shule nyingi za umma, watoto hawapati chakula na wanasoma kwa muda mrefu sana huku wakibebeshwa mizigo mizito ya madaftari. Sidhani kama viongozi wetu wa serikali wanaweza kuvumilia watoto wao wasome bila kula katika shule wanazowalipia bei kubwa huko kwenye International schools.

Lakini tukumbuke mamlaka na uongozi hauangalii historia ya shule alizopitia kama International au KAYUMBA, kutoka shule yeyote mtu anaweza kuwa kiongozi wa taifa hili. Sasa tunatengeneza taifa la namna gani kama viongozi wetu wajao leo wanashinda njaa mashuleni bila kula! Tunategemea kupata viongozi wa namna gani? Si ni ongezeko la viongozi njaa na CHAWA ambao baadae wanatusumbua wananchi kwenye media kwa kusifia kila jambo ilimradi mkono uende kinywani!? Ukiangalia kwa makini vijana CHAWA wa zama hizi, ukirudi nyuma kwenye historia ya usomaji wao utagundua kwamba wote wamesoma St. Kayumba ambapo chakula shuleni kwao ilikuwa hawapati na hivyo njaa ile imeathiri ubongo wao hadi kwenye utu uzima wao.

Kipi serikali ifanye ili kuwezesha upatikanaji wa chakula kwa wanafunzi wote hasa wa shule za umma msingi na sekondari:
  1. Mbinu muhimu sana ni hiyo ya kucheza na mifumo ya kodi kwa kuwapunguzia kodi watoaji wa chakula mashuleni.
  2. Shule ambazo hazina majiko, zitenge hata madarasa shuleni kwa ajili ya kuwa majiko kwa ajili ya chakula cha watoto shuleni hapo.
  3. Makupuni kama MANJIS GAS, TAIFA GAS, au MERU GAS wapewe punguzo la kodi kwa wao wakifanikisha usimikaji wa mifumo ya majiko ya gasi mashuleni.
  4. Makampuni na wafanyabishara wahimizwe kuandaa mpango wa kulisha mashule, TRA iweke namna ya kuwapunguzia kodi makampuni hayo kwa kujirishisha kwamba misaada yao ya chakula imefika katika shule husika.
  5. Halmashauri kupitia kamati ya chakula mashuleni itahakikisha kila shule inapata mgao wa chakula kulingana na akiba iliyopo.
  6. Saa 7 kamili mchana masomo yata stop ili watoto wapate chakula cha mchana hadi saa 8:20 baada ya hapo watarudi darasani kumalizia vipindi double (dk 80) vya mwisho.
  7. Kwenye huo mulo wa wanafunzi, serikali itaandaa bajeti ya kulisha walimu wake nchi nzima ili kuendana na utoaji wa elimu pasipo kusumbuliwa na njaa. Na jua kuna mambo mengi muhimu walimu wa Tanzania hawapati ili siamini kwamba serikali inaweza kushindwa kuwapa hata pesa ndogo posho ya chakula kwa walimu ili waweze kutengeneza kizazi kijacho kilicho bora zaidi.
  8. Wazazi wa wanafunzi watapaswa kuchangia shs 5000 kwa mwezi kwa ajili ya kufanya huduma hii ya chakula iwe endelevu kwa wanafunzi wote. Hiyo ela itatumika kulipa wapishi watakao kuwa wanawapikia wanafunzi hao huko shuleni.
Faida ya uboreshaji huu wa usafiri na chakula kwa wanafunzi wa kitanzania:
  1. Ufaulu kuongezeka kwa sababu vile vipindi vya asubuhi walivyo kuwa wanavikosa, sasa watakuwa wanaviwahi kutokana na uwepo wa daradara hizo maalumu.
  2. Uelewa na maarifa ya wanafunzi wa kitanzania kuongeza maradufu kwa sababu sasa watoto wana hakika ya kupata chakula shuleni na hivyo akili zao kutulia kuhusu darasani.
  3. Idadi ya wanafunzi mashoga, machawa, wadangaji n.k itapungua kwa sababu wengi wao adha ya usafiri na njaa ndio huwapelekea kutumbukia kwenye matendo hayo.
  4. Uhakika wa kupata viongozi walio sahihi kwa ajili ya kusukuma maendeleo ya nchi yetu kwa sababu wataguswa na namna wananchi na serikali yao ilivyo waangaikia kwa makuzi yao yaliyo bora.
Maboresho hayo mashuleni yaendane sambamba na uboreshaji sera ya elimu kwa ajili ya kuwaingiza watoto wa mitaani hasa wa kwenye mastendi kurudi kwenye vituo vya elimu kwa ajili ya kupata elimu na maitaji yao.
Viongozi kuacha hawa watoto kwenye hali ngumu za maisha huku tukiacha nature ndio iamue hatma ya maisha yao itatugharimu sote kwa sababu watoto hao wa kimaskini, mitaa inawanywesha sumu na kutokuwa watu wanaojali juu ya jambo lolote.

Hivyo adui akiamua kutumia kundi hili la vijana waliotelekezwa toka zamani huko mashuleni kwenye makuzi yao wanaweza wakauwash moto nchi yetu hii nzuri Tanzania ikawa aikaliki. Watanzania, viongozi tuifikirie Tanzania yetu nzuri ijayo kwa kuwa hudumia watoto wetu wote walioko mashuleni kwa usawa na haki ili kama taifa tuje tujivunie watoto wetu wakipewa majukumu makubwa. Tusifikirie tu watoto wetu ila tutambue na tuone kwamba kila mtoto wa mtanzania mwenzako ni wako pia.

Utamkuza mtoto wako huko magetini kwenye mbwa wakali lakini siku akikua na kujitambua ana kuletea mkwe kutoka st. Kayumba ambayo mzazi halikuwa tegemeo lako. Hivyo tuboreshe hizo st. Kayumba ili vijana wengi walio bora watoke katika shule hizo ili watufae hata wakiwa viongozi wetu muda huo tukiwa tumezeeka.
Kupata chakula ni vyepesi sana kama srikali itafanya hivi
Magereza yote kuyasupply vifaa vya kilimo nya kisasa na pembejeo mahabusu kulima na kutengeneza maghala kila wilaya hakika hakutakuwa na njaa Tanganyika milele with umeagiliji
 
Hapa umeicheza vizuri, naona kama imewafaidisha wote. Mabosi, wanafunzi hadi walipakodi wote wame 'win'. Safi

Tunahitaji utafiti hapa. Unaweza kuta hawa ST. Kayumba uzalendo ukawa juu sana tu ukilinganisha. Lakini kinadharia, mzuri zaidi atakuwa ni yule amepita sehemu zote mbili International na Kayumba. Uzoefu muhimu bro. Mleta mada hapa sikupingi wala sikubali ila nasema tunahitaji utafiti.

Naipenda sana mifumo ya uchangiaji gharama. Inaongeza uwajibikaji na uwajibishaji kwa pande zote. Kitendo tu cha mzazi kusema mtaani kwamba 'Nimetoa hela yangu, msiniambie chakula hakipo' ina kamsukumo kazuri sana kwenye ajenda.
Hakuna elimu ya bure chief wazazi inabidi waambiwe ukweli tuachane na siasa kwenye maisha ya wanafunzi
 
Back
Top Bottom