Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,147
- 30,495
BI. TITI MOHAMED, JULIUS NYERERE, OSCAR KAMBONA NA MAMA MARIA
Picha hiyo hapo chini inamuonyesha Bi. Titi akizungumza na nyuma yake amekaa Julius Nyerere, Oscar Kambona na Mama Maria Nyerere.
Hii ni miaka ya mwanzo ya uhuru 1960s hata Azimio la Arusha bado.
Kwa nini nimelitaja Azimio la Arusha?
Nimelitaja Azimio la Arusha kwa sababu ni uamuzi muhimu kwa ile fitna iliyokuja kuikumba nchi na pia kujenga uadui kati ya viongozi hawa ukimtoa Mama Maria.
Baada ya Azimio la Arusha Kambona alipokimbilia uhamishoni Uingereza Nyerere alimshambulia hadharani kwa maneno makali na kwa lugha nzito na kumpa jina shida kutamkwa kinywani.
Bi. Titi na Nyerere mwaka uliofuatia lakini katika faragha walipambana.
Katika ugomvi huu Tewa Said Tewa alikuwapo.
Tewa alikuwa President wa East African Welfare Society (EAMWS) na Bi. Titi Vice President.
Ugomvi ulihusu kupigwa vita EAMWS.
Hisani na wema wa miaka mingi ulitoweka vitisho vikatawala.
Hii ni timu ya TANU ya 1954 iliyopigania uhuru wa Tanganyika.
Katika hao aliye hai ni Mama Maria peke yake.
Kila niangaliapo picha kama hizi fikra zangu huenda mbali nikakumbuka walikotoka viongozi hawa na mwisho wao ulikuwaje.