Mundali
JF-Expert Member
- Sep 16, 2010
- 749
- 164
Nadhani mkuu hukunisoma vema, utakubaliana nami kwamba madikteta wengi wamekuwa wakitumia rasilimali za nchi zao kujinufaisha, ilhali wakiacha watu wao katika lindi kubwa la umasikini. Tofauti ya Dikteta huyu na wengine ni kwamba pamoja na madhambi yake lakini sehemu kubwa ya rasilimali za nchi yake alizizitumia kuboresha maisha ya watu wake. Kumbuka maendeleo ni maendeleo ya watu na si Mabarabara ya hewani n.k. Udikteta wake kimsingi ulikuwa dhidi ya wapinzani wake na uadui wake ilikuwa dhidi ya mataifa ya magharibi. Hakukubali rasilimali za nchi yake kuporwa kwa kubadilishana na vyandarua. Na kwa kukufumbua macho ndugu yangu huo ndio udikteta wa Mugabe pia. Ni dikteta kwa sababu alirudisha ardhi kwa wananchi toka kwa wazungu waliomiliki 75% ya ardhi yote.@Mundali. Ebu usituaibishe kama sisis wote ni masikini wa akili. Hizo pesa zilizofanya mambo yote ni za Libya siyo za familia ya Gaddafi. Hiyo siyo hisani ni wajibu wa kiongozi/mtawala yeyote atakaye itawala Libya. Utajiri mkubwa wa mafuta na gesi ilionao Libya na population ndogo ya wananchi wa Libya hayo aliyofanya Gaddafi siyo miujiza,ni miujiza kwa watu wenye akili za kimasikini kama sisi. Binafsi sijaona mabarabara wala majumba mazuri na ya kuvutia ktk Libya kama zilivyo nchi nyingine za Kiarabu zenye utajiri wa mafuta kama Kuwait,Falme za Kiarabu na Saudi Arabia.
Kama kweli hawa jamaa wanapigania demokrasia ya kweli Kibaki na JK wasingekuwa madarakani (Wote EA tunajua ukweli huu).
Hila za magharbi siku zote zimekuwa ni devide and rule, walimwita Saddam anasaidia ugaidi, akaitwa dikteta akanyongwa na watu wake (vibaraka wa marekani), deal ilikuwa reserve ya mafuta. Leo kiko wapi? Siera Leone wameuwana kwa ajili ya Diamond, pesa ya mmarekani victim Charles Taylor. Congo mpaka leo wako vitani (mkono wa mmarekani), deal dhahabu. Na hata hapa JK asingekuwa mtu wao, wangetafuta vibaraka wengine wakawapatia silaha na fedha na tungeuwana tu. Tena hapa wana interest chungu nzima. Hatuyaoni sababu viongozi wetu na sisi wenyewe ni "YES SIR".
AM STANDING TO BE CORRECTED, COL. M. GADAFFI IS A HERO HE FOUGHT FOR HIS COUNTRY AND HE DIED IN HIS COUNTRY FIGHTING!