WAHENGA: Ushawahi kukwea mabasi ya Reil Way?

babukijana

JF-Expert Member
Jul 21, 2009
13,113
16,021
Sipati picha enzi hizo tulivyojazana humo loh, lakini kufika ni salaama kabisa hata ichukue wiki uhai upo.

1607321681960.png
 
sipati picha enzi hizo tulivyojazana humo loh,lakini aah kufika ni salaama kabisa hata ichukue wiki uhai upo.

Ndio basi nililopanda wakati naenda kuanza form one kule Iringa. Nakumbuka siku hizo tunasafiri usiku! Aaaah, kweli tumetoka mbali!
 
Mabasi ya relwe kwa sana, Dar Iringa, We acha tu , Enzi hizo tunasafiri usiku.
 
Ilikuwa Dar - Mbeya lazima utumie like 20 to 24 hrs. lakini hakukuwa na ajali za mara kwa mara kama sasa.
 
Kwi kwi kwi!
Relwe Mbeya ilikuwa pale Uhindini, pembeni kidogo ya ile round about.
safari toka Dar mpaka Mbeya mnalala njiani, nakumbuka watu wanasafiri na sufuria za wali na kuku wa kukaanga, kweli maisha haya jamani.
pale Kitonga unashika roho mkononi, kweli tumetoka mbali.
 
Nimesafiri sana na Relwe kati ya Njombe Iringa Dom Babati enzi hizo toka nikiwa mdogo,nakumbuka yalikuwa na first class toka kwa driver mpaka mlango wa abiria kulikuwa namlango tena.na nauli tofauti.walikuwa wanakeep time kama ndege aaaaa haiwezi kurudi tena.kulikuwa pia na KAMATA unakumbuka mdau?
 
zaidi ya kamata kulikuwa na kwacha pia.
 
View attachment 8949
sipati picha enzi hizo tulivyojazana humo loh,lakini aah kufika ni salaama kabisa hata ichukue wiki uhai upo.

Nyerere alikuwa na mawazo mazuri sana! Ila utelezaji ndiyo ulimshinda. Ndio maana hata yeye mwenyewe aliwahi kutamka kwamba kila anaposoma tena kitabu cha Azimio la Arusha, haoni pabovu.

Angalia hata leo kwenye nchi zilizoendelea kuna uwiano wa hali ya juu katika miundombinu ya usafiri. Yaani kwenye vituo vikubwa vya mabasi ya abiria wa mjini lazima kuna kituo cha treni la abiria wa mjini. Kwenye kituo kikubwa cha mabasi na treni ziendazo nje ya mji, kuna kituo pia cha mabasi na treni zinazozunguka ndani ya mji.

Sasa ukuangalia Relwe, walikuw na utaratibu huo, pale Itigi kulikuwa na mabasi ya Relwe ya kwenda Singida mjini na yalikuwa hayaondoki mpaka treni ifike ili abiria waunganishe! Na tiketi nadhani ilikuwa ni moja!

Kama mfumo huo ungeendelezwa sasa hivi tungekuwa mbali sana! Inasikitisha sana kuona mambo yote mazuri hayapo tena katika nchi hii. Ukiangalia usafiri wa mabasi ndani ya jiji la Dar miaka ya 80 ulikuwa bora zaidi kuliko ilivyo sasa.
 
nyerere alikuwa na mawazo mazuri sana! Ila utelezaji ndiyo ulimshinda. Ndio maana hata yeye mwenyewe aliwahi kutamka kwamba kila anaposoma tena kitabu cha azimio la arusha, haoni pabovu.

Angalia hata leo kwenye nchi zilizoendelea kuna uwiano wa hali ya juu katika miundombinu ya usafiri. Yaani kwenye vituo vikubwa vya mabasi ya abiria wa mjini lazima kuna kituo cha treni la abiria wa mjini. Kwenye kituo kikubwa cha mabasi na treni ziendazo nje ya mji, kuna kituo pia cha mabasi na treni zinazozunguka ndani ya mji.

Sasa ukuangalia relwe, walikuw na utaratibu huo, pale itigi kulikuwa na mabasi ya relwe ya kwenda singida mjini na yalikuwa hayaondoki mpaka treni ifike ili abiria waunganishe! Na tiketi nadhani ilikuwa ni moja!

Kama mfumo huo ungeendelezwa sasa hivi tungekuwa mbali sana! Inasikitisha sana kuona mambo yote mazuri hayapo tena katika nchi hii. Ukiangalia usafiri wa mabasi ndani ya jiji la dar miaka ya 80 ulikuwa bora zaidi kuliko ilivyo sasa.

masaki kweli umenena lililo la maana.
Tatizo ni kwamba watawala wetu hawa na maafisa wa mipango miji wamegubikwa na rushwa.
Nafasi zao na taaluma zao zinaendeshwa na wale watoao mpunga.
Na watoao mpunga hawana long term plans... Wanataka hela nyingi ya mkupuo.
Habari ndio hiyo... Hatari ndiyo hiyo
 
Nini kifanyike?
 
Enzi izo nshawai pakizwa umo kurudi DSM,usafiri ulikuwa wa taabu sana.
Barabara ilikuwa hovyo na magari vimeo but hajari zilikuwa nadra
 
ngoma ikipigwa gia ndani abiria wote mna vibrate,nakumbuka siku moja nikiwa mdogo tumetoka mbeya tunaenda singida,ilibidi basi lingine tuunganishe iringa linalokatiza mtera kwenda dom,alikua mgambo yule sijui askari,eti karuhusu familia yangu yote iingie kasoro mimi,kisa sikukielewa ila tu nilimuona mdingi anakomaa nae sana,kidogo amtoe roho jamaa,hata hivyo niliingiziwa dirishani kisha nikapeta hadi dom.
 
Yalikuwa na utaratibu mzuri sana, mkitoka Dar likifika morogoro linafanyiwa check-up, baada ya hapo tena linafanyiwa check-up Mikumi, Iringa gari linabadilishwa kama safari ni ya Mbeya, hakukuwa na chinja chinja kama ilivyo leo, natamani yarudi tena, bora uchelewe lakini ufike salama
 
Pale Iringa kuna nyumba nyingi sana za wafanyakazi nafikiri hapo ndipo palikuwa makao makuu ya haya mabasi
 
Nimesafiri sana na Relwe kati ya Njombe Iringa Dom Babati enzi hizo toka nikiwa mdogo,nakumbuka yalikuwa na first class toka kwa driver mpaka mlango wa abiria kulikuwa namlango tena.na nauli tofauti.walikuwa wanakeep time kama ndege aaaaa haiwezi kurudi tena.kulikuwa pia na KAMATA unakumbuka mdau?
hivi kwanini picha za mabasi ya KAMATA hazipo?! inasikitisha sana
 
Back
Top Bottom