BansenBurner
JF-Expert Member
- Feb 16, 2015
- 6,812
- 5,765
Ndio nchi pekee inayoongoza kwa hifadhi za wanyama na mlima mrefu lakn 80% ya raia wake hawajawah hata kuona simba au swala"
Karibuni wadau tuichambue hii TANZANIA yaani TANGANYIKA (TANGA (Jahazi) + NYIKA yaani JAHAZI NYIKANI) na ZANZIBAR (Zengi(mtu mweusi) + Barr (pwani) yaani Mtu mweusi maeneo ya pwani)
ONGEZEA CHOCHOTE KATIKA LIST HII
1.Zao la katani/MKONGE(white gold) lilipandwa kwa mara ya kwanza afrika nchini Tanzania. lililetwa baada ya mjerumani researcher kuiba (alichukua kinyume na sheria) miche 1000 Mexico kuja TZ kupitia Hamburg ujerumani. ilifika bandari ya tanga miche 63 tu mingine ilikufa njiani. Ndio chanzo cha katani afrika na kuifanya TZ duniani kuwa nchi ya pili nyuma ya Brazil kwa kuzalisha katani.
2.Mti ghali na wenye thamani kabisa kuliko yote duniani MPIGO unapatikana Tanzania.
3. Wimbo wa taifa "Mungu ibariki afrika" ulikuwa ni wimbo wa Kizulu ".Nkosi sikelel' Afrika ". mwaka 1873 mwalimu Enock santonga wa africa kusini aliutunga. lengo ilikuwa ni kutunga wimbo wa Shule aliyokuwa anafundisha. Leo hii tunauimba sio sisi tu bali S/Africa, Zimbabwe,...
4.Kaa/Crab (coconut crab) mkubwa na mtamu kuliko wote (kwa mujibu wa walaji) dunia nzima anapatikana Tanzania maeneo ya Chumbe kisiwani zanzibar.
5: Katika list ya makabila 10 Maarufu Afrika nzima, Wamasai ni wa Pili na wachaga wanashikilia nafasi ya 10.
6: Zanzibar ndio ilikuwa ya sehemu ya kwanza kuanza kutumia TV zenye rangi afrika nzima mwaka 1974. wakati Television ya kwanza kwa bara ilianza mwaka 1994 sababu inasemekana ilikuwa ni kupingwa na mwalimu Nyerere.
wasandawe
waadzabe
7:Kama ilivyo marekani Wahindi wekundu, Makabila mawili Waadzabe na wasandawe ndio wakazi halisi wa tanzania. Wengine wote tulihamia miaka zaidi ya 2000 iliyopita. kuna tuliotoka Africa Magharibi (wabantu), Africa kusini, Kaskazini sudan,ethiopia na sehemu nyingine mbalimbali africa. mfano WaDatoga na wengine waarusha waliingia kutoka mipakani mwa ethiopia na sudan kati ya miaka 2900 hadi 2400 iliyopita kutokana na ushahidi wa kiachiolojia. Tusibaguane tuwaheshimu hawa wadau wawili.
8:Tofauti na mchi kama ISrael au Libya ambapo jangwa ni asilimia kubwa sana Nchi yetu tanzania ni ya 31 kwa ukubwa duniani. lakini 38% ya nchi au ardhi imetengwa kama hifadhi na haitumiki kwa uzalishaji isipokuwa utalii.
9:Tanzania ina sehemu mbili za muhimu katika jiografia ya africa. Point ndefu kabisa afrika ni mlima kimanjaro kileleni(yaani kama tukiiminya afrika na ukasimama kilimanjaro utaiona afrika yote) na point ya chini kabisa ipo katikati ya ziwa Tanganyika. Mlima kilimanjaro mchakato wa kuanza kwake ulisababisha uwepo wa ziwa tanganyika, edward na kivu.
10:Kikosi maalumu ya wanajeshi wa tanzania kilichopo CONGO, kiliingizwa katika list ya SPECAIL FORCES bora kabisa (most elite) 35 duniani . list hii iliongozwa na US NAVY SEAL, Brittish SAS, HUNTMEN CORPS danish special forces.
11: Kulingana na National Illigation MASTER plan ya 2002, eneo la kilimo hapa kwetu linalofaa kwa umwagiliaji ni HECTA MILLIONI 29.4, lakini eneo ambalo hadi june mwaka 2011 limekuwa likitumika kwa kilimo HIKI ni HECTA LAKI TATU ELFU KUMI NA MIASABA AROBAINI NA TANO sawa na asilimia 0.01.
Tanzania ni nchi yenye amani, maziwa ya maji fresh, mito mikubwa, na ardhi kubwa kabisa inayofaa kwa kilimo, na nguvukazi kubwa kabisa, lakini inaagiza mchele, mpunga, sukari, nyanya nje ya nchi
RUDIA KUSOMA VIZURI MKUU. NI MTI MOST EXPENSIVE DUNIA NZIMA. KAMA UNAPATIKANA KWINGINE VIZURI POINT NI GHARAMA YA HUU MTI DUNIANI NA UHABA WAKE.Samahani mkuu, Mpingo unapatikana Tz tu, au nimesoma vibaya uzi wako?
UKO SAHIHI MGENIHamna kitu hapo
Nchi pekee kutokuwa na Rais kwa miaka 10 (2005-2015)
utakuwa na utani na watu wa msoga wewe teh teh tehNchi pekee kutokuwa na Rais kwa miaka 10 (2005-2015)