Unajua kwanini mapenzi ya mbali hayadumu?

Kasuku Mdogo

Member
Jun 2, 2016
14
23
Wengi wetu hujiuliza kwa nini maisha ya mapenzi ya mbali huwa hayafiki mbali na kubaki wa kijiuliza tatizo ni nini? Wakati mwingine watu huanza kuulizana mchawi ni nani katika mapenzi yao. Laa hasha! Huenda mchawi wa mapenzi yako ni wewe mwenyewe lakini hujui kwa sababu hakuna mtu ambaye ameshawahi kukueleza jambo hili na lile ndio tatizo.

Hata hivyo hakuna kumbukumbu ambazo zinaonesha ni kwa asilimia ngapi ambazo wapenzi wanapenda kuwa mbali mbali japo mazingira mara nyingi ndio huwa chanzo.

Katika tafiti mbali mbali zinaonesha kwamba umbali humaliza kabisa mapenzi ambayo wapenzi wengi wenye malengo ya kufika mbali huwakuta.

Lakini zipi sababu mbalimbali ambazo ukizichanganua utajua kwa nini mapenzi mengi ya mbali hayadumu.

Wivu

Wivu huwa ni chachu ya kupima upendo lakini ukizidi pia huwa tatizo. Wivu wa mapenzi ukizidi husababisha kutokuaminiana kwani kila mmoja kwa wakati wake tofauti huhisi mwenzake anamsaliti, mara nyingi hali kama hii humfanya mmoja wapo kati ya wapenzi hao wawili kuona kama mwenzake ameshamchoka na anamtafutia sababu. Ni vyema kuwa na wivu kiasi kwa mpenzi wako.

Mawasiliano

Mawasiliano huimarisha mapenzi na hufanya wahusika kujihisi wapo pamoja. Inapotokea kuwa na ufinyu wa mawasiliano ndipo hali ya mapenzi ya upande mmoja hupungua na kuhisi kwamba tayari mwanamke/mwanaume tayari ameshapata mwingine wakumfanya asifanye mawasiliano ya mara kwa mara.

Ugomvi

Magomvi ya mara kwa mara hufanya mmoja wenu ahisi kuchoka na mahusiano. Inapotokea sababu za ugomvi ambao unahisi unaweza kuwa chanzo cha kuvunja mahusiano yenu ni afadhali ukazizuia na kutafuta siku nyingine ya kutatua tatizo hilo.

Kutojali

Hii mara nyingi imetajwa sana kuwa ni chanzo cha mapenzi ya mbali kuvunjika kwa sababu tofauti mfano mpenzi wako alipokuwa karibu ulikuwa ukimpatia huduma mbalimbali kama zawadi n.k. Lakini anapokuwa mbali unajisahau hali hii humfanya mpenzi wako ajiulize kulikoni?

Usikivu

Nayo ni sababu ambayo ukiwauliza wengi wao ambao walikuwa na uhusiano wa mbali ukavunjika lazima atakulalamika kwamba alikuwa hanisikilizi nacho mwambia. Mfano alitaka kutoka kwenda ‘out’ na wenzake nikamnyima lakini hajanisikiza hivyo hanifai.

Hizi huenda zikawa ni baadhi ya sababu ambazo wapenzi wengi ambao mapenzi yao hayajafanikiwa kama jinsi walivyo hitaji wamekumbana nazo.

Ili kuepuka changamoto za kutengana na mtu ambaye unamuhitaji katika maisha yako ni vyema ukaanza kujifunza pole pole kutoka kwake ili siku ukiwa mbali naye ujue kipi mwenzako anapenda na kipi hakipendi mnapokuwa mbali.
 
Hata nucleus ya atom huzivuta zaidi electron zilizo karibu yake huku zile za mbali kutoka kwenye nucleus zikiwa loose. Hivyo mpenzi wa mbali atakuacha tu kwani kutakuwa na mtu aliye karibu yake zaidi na atakaemvutia zaidi pindi wewe uko mbali nae na hapo ndo mwanzo wa kupigwa chini.
 
Sasa na hii halu ya baba jesca jaman lazm wote msaidiane kutafuta km kazi zimewafanya muwe mbali ndo inakuaje apo..uhesabu tu apa sina changu mapema
 
Distant love na mume/ mke wa mtu ndo kabsaaaa. kwanza no night calls
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom