Shairi: UKUTA UKUTA!

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298
UKAWA UKUTA.

1)hi ndio khasara yake,gari kukosa kioo.
Lione gari ndo lake,siyo waseme ni ndio.
Acha wafie kivyake,jicho ona chungulio.
Kuwa ukawa ukiwa,kuta litawa mkia.

2)maneno mengi kapuni,alifuta kwa fagio.
Hata na wake mtani,kamchapa kwa pambio.
Mwisho kiganja shavuni,mushi kashika chinjio.
Kuwa ukawa ukiwa,kuta litawa mkia.

3)toyo hipiti barini,hata daraja la nguo.
Wiki mwashinda chumbani,kisha mwaleta chekeo.
Nazi ituapo chini,dafu halina kileo.
Kuwa ukawa ukiwa,kuta litawa mkia.

4)hata chozi la kambale,halichujwi kwa chujio.
Vipi kuta kute mbele,unatenda jaribio.
Wewe shiba matembele,nyusi hifungwi banio.
Kuwa ukawa ukiwa,kuta litawa mkia.

5)huyo ndie baniani,dawa yake ni zomeo.
Umemuweka shambani,atavuna na kombeo.
Tembo haishi majini,kobe hafungwi koleo.
Kuwa ukawa ukiwa,kuta litawa mkia.

Shairi= UKAWA UKUTA.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Facebook page=Idd ninga mashairi.
 
Back
Top Bottom