Uzalendo kwa Taifa letu - Tanzania

Wapo Wabunge kama wanne vijana zitto yumo na mwenzie December Marope ambao wana ukwasi wa kutisha. Huyo mwingine ambaye hakupewa kura hata moja aana miradi mikubwa sana ndani ya TANESCO ambayo inafahamika. Amewahi kunukuliwa na wafanyakazi wa TANESCO akiomba tenda akiwa mwenyekiti wa kamati fulani la bunge, kwamba angeleta wawekezaji toka India. Wanaokabiliwa na tuhuma nzito ni wale waliochukua uongozi mwezi uliopita.

Wale waliotangulia wako wapi? Waandishi tulijaribu na kupigwa STOP hata kabla ya kuanza. Mtu huyu ana madudu makubwa sana lakini Kila mtu Kimya. Kulikoni?

Sitaji jina kwa sabau thread yangu itaondolewa dakika 20 zijazo, wote mnamjua tu.

Du !!!! vijana tumekosa uadilifu na kwa mtindo huu tunapoteza mvuto kwa jamii yetu na kwa namna fulani ile kauli kuwa vijana ni viongozi taifa la kesho ilikuwa na maana sana. unaweza ona siyo tu february na nyepesi wapo pia akina laini
 
Kwani majina ya wabunge walofanya biashara na TANESCO na wale waliopokea rushwa ni wepi? Majina yao.
 
Unanikumbusha mtu mmoja alisema amefanyiwa vitendo vya hujuma, ushahidi anao lakini haendi polisi wa mahakamani kudai haki yk, anasubiri achokozwe tn, sa wewe unamfahamu af unaogopa kumtaja si bora usingeandika tu tusijue kuwa na wee unafaham , maandshi yk yt hayana mana kwa uoga wako
 
Si umeshasema ni tuhuma? Tuhuma zaweza kuwa wrong.
Nothing to comment!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

 
Vijana!!!!!!!
Msikubali kubadirishiwa story kila siu!!!
Gumzo limekuwa TANESCO!!!!
Hebu jiulizeni, mmeshaenda Kahama kuona madini yanavyosombwa kwenda nje na kubaki handaki???? kila madini yanayopatikana Tanzania mna faida nayo ipi zaidi ya kuona wawekezaji tu!!!!
msikae kubishana na haya mambo unganeni ungeni mkono chama mnachoona kinamwelekeo wa kulinda mali za nchi hii ili siku ya siu utawala urudi kwa wenye mapenzi mema na nchi hii!!
Ama sivo mtabaki kulalamika tu wamekula hapa, wameiba huku, wameibua hiki mradi tu kuwachangany!!
Y babu wa Loliondo mliona yalivyotibua mambo ya msingi????
Tanzania hasa vijana amkeni, mbona vijana bungeni wako wengi na wanafanya vizuri? hata huyo ambaye amesemekana kala kidogo cha TANESCO hebu angalieni tuendako, msianze kutibuliwa kwa hilo mkageuka nyuma! kumbukeni ya mke wa Lutu, aligeuka nyuma na akawa jiwe la chumvi?
Tutakari maendeleo, tufanye kazi kwa bidii katika sehemu tulizopo! wenye nafasi waajirini vijana tuondokane na wapiga debe ili kila kijana apate mahali pa kufanya kazi katika kulinda na kujenga nchi yetu!!!
Vijana nasema tena amkeni fikirini kwa makini! kila ikitokea kitu kinashikiwa bango kusudi mpumbazike msifikirie ya mbee yenye manufaa kwa Taifa. wenzetu tunaowaita "nchi zilizoendelea" wanafanya kazi eti!!
Ukianglia wakati mwingine vijana wanapoteza muda mwingi kulumbana kuhusu timu za mpira za nje tena kwa muda mwingi, hafikrii huo mda angekuwa anafanya kitu cha maendeleo mahali angezalisha vingapi????
neno la Mungu linasema, asiyefanya kazi asile!
Maendeleo yanapatikana kwa kuwajibika!!
Hebu jiulizeni katika haya machache!!!
Cha msungi nasisistiza nchi yetu ni nzuri na in utajiri wa kila namna hao wadosi hamshangai wamekuwa wakija now and then na kutudanganya kama watoto!!!!
Kijna amka Tanzania ni yako, wazee muda wetu umepita wewe una muda mwing wa neema mbele yako usiuchezee!
wabeja
 
Hakuna cha utaifa bana, watu wanataka maisha ya bia na nyama choma,utaifa tuliwaachia kina nyerere,kwa sasa ni kutumikia tumbo tu.
 
Huu uumbe wa huyo wabeja umenikumbusha ktu!!
Vijana angalieni saana pi wizara ya afya, ni wizara inayotunza na kudumisha afya zetu tangu mtoto akiwa tumboni hadi uzee!
Wizara inajitahidi kusomesha lakini haiangalii hao wanaosoma wanafanya yale waliyosomea??? anliyesomea kuhudumia wazazi anawekwa kwenye wodi ya majeruhi, aliyesomea watoto anawekwa wodi ya watu wazima, aliyesomea wenye matatizo ya wenye ugonjwa wa afya ya akili anapelekwa kliniki ya watoto na akina mama, nayo ni tatizo, nyie pekee mkikaa sawa kwa kusoma alama za nyakati mambo yote yatakaa sawa. Kweli kuna haja ya kuangalia maswala yote kwa uakini mkubwa mkiendekeza yanayoibuliwa mtakuwa mnaibiwa ufahamu wenu na nchi itazidi kudorola!!
Huyo wabeja naona ana kitu cha msingi tutafakari kwa umakini
Mimi ni Mtanzania ninaye ipenda saana nchi yangu, najivunia kuwa mtanzania nasikitika wanaoiongoz Tanzania hawaoni uzuri wa nchi yetu au wanajipenda wao tu yaani are selfish au hawaoni wanachi wanavyoteseka!! hebu tusaidiane kufumbua macho wapenda nchi!
Jane Nyanda
 
wenzako wanaheshimu misemo ya kiswahili kama "Chukua Chako Mapeme" a.k.a CCM
 
UZALENDO WETU NA MAPENZI YETU KWA VYAMA VYA SIASA.

Dunia imeagana na nyonga, inakwenda mbio sana. Kuna mambo unatamani yasimame kama yalivyo, yasibadilike. Lakini katu haiwezekani. Kuna watu unatamani waishi milele, lakini bahati mbaya au nzuri tuliumbwa kwa udongo na tutarudi kuwa udongo. Leo nimewakumbuka sana watu wanne maarufu ambao dunia ina rekodi zao.

Che Guevara, mwanamapinduzi kutoka Argentina anabaki kuwa mtu wa pekee sana katika ulimwengu huu. Huyu hakuwa tu mzalendo kwa taifa lake, bali uzalendo wake ulivuka mipaka. Che alikuwa mzalendo wa dunia. Mapenzi gani haya! Che aliiacha nchi yake na familia yake, na kuungana na Fidel Castrol kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu. Kwa Che ,kauli ya binadamu wote ni sawa, ilikaa moyoni mwake. Nakumbuka maneno mazito aliyoyazungumza wakati anaagana na pacha wake, Fideral Castrol. Nimekumbuka maneno yenye hisia kali, yaliyo kwenye barua ambazo alikuwa anamwandikia mke wake.Mwisho wa safari wake iliishia Bolivia.

Kuna huyu W.P.Botha, Rais wa Kwanza wa serikali ya kibaguzi ya Afrika Kusini. Wakati anahutubia baraza lake la mawaziri tarehe 18/08/1985, alisema kuwa binadamu wote, haimaanishi kwamba Waafrika (watu weusi) wako sawa na wazungu. Hii inabaki kuwa hotuba mbaya zaidi katika ulimwengu wa ubaguzi. Pamoja na maneno hayo kuwa makali sana, kuna ukweli kwa baadhi ya mambo. Kwa Wazungu (Afrika Kusini), Botha alikuwa mzalendo. Alikuwa tayari kulinda masilahi ya watu wake kwa namna yoyote.

Mwana Halisi wa Afrika, Patrice Emery Lumumba, kabla hajafariki (akiwa anashikiliwa na watesi wake) alimwandikia barua mke wake. Ile barua ilikuwa na hisia kali sana. Ulikuwa ujumbe mzito sana kwa nchi yake, kuliko hata familia yake. Baadaye Lumumba alitolewa roho kwa namna isiyosimulika. Patrice Lumumba anabaki kuwa mzalendo halisi katika harakati za kuikomboa Zaire (sasa DRC) na Afrika kwa ujumla. Hata upande wa pili, wanaamini kwamba waliomuua Lumumba walikuwa wazalendo.

Angalia usaliti alioufanya Compaure kwa nchi yake na kwa comrade Thomas Sankara. Sankara alionyesha mwanga kwa nchi yake na kwa Afrika. Kasi yake iliwatisha sana wazungu na vibaraka wake. Ndipo wazungu wakaunda mpango wa kumuua Sankara kwa kushirikiana na vibaraka kama Blaise Compaore.

Hapa ndipo nachanganyikiwa kuelewa maana halisi ya neno Uzalendo. Neno hili linatamkwa sana kwenye majukwaa ya siasa na wanasiasa. Pamoja na kwamba, neno hili linatumika sana, lakini ukweli ni kwamba linatumika kulingana na masilahi ya anayelizungumza. Nini maana halisi ya uzalendo kwa vitendo? Mipaka ya uzalendo iko wapi? Mtu kuipenda sana nchi yake, ndio uzalendo? Tunapimaje kwamba mtu anaipenda sana nchi yake? Tuchukue mfano wa Che, Sankara na Lumumba kuwa ndio maana halisi ya uzalendo?

Katikati ya hii tafakuri, nikakumbuka tukio moja. Mwaka 2007, kulikuwa na fukuto la Mkataba wa Buzwagi. Zitto Kabwe aliadhibiwa vikali, kwa kusema waziri wa nishati wakati huo, alisaini mkataba wa Buswagi Hotelini Londoni. Zitto kabwe aliitwa majina yote mabaya. Msaliti na mtu aliyekosa uzalendo. Kesi kama hizo zimejitokeza sana katika nchi yetu. Lakini mwisho wa siku inathibitika kwamba yaliyokuwa yanasemwa ni kweli. Katika hali kama hiyo, nani anakuwa mzalendo, aliyesaini mkataba ambao hauna masilahi kwa nchi au aliyefichua siri hiyo?.

Baada ya hapo, nimegundua kwamba tunatumia neno UZALENDO vibaya. Tunatumia neno hili, kwa masilahi binafsi (mara nyingi). UZALENDO au UTAIFA hauwezi kumilikiwa na mtu mmoja. Kila mtu anaweza kuwa mzalendo au vinginevyo kwa nafsi yake. Kila mwananchi anawajibika kuhakikisha nchi inakwenda mbele kimaendeleo. Maendeleo ya nchi hayawezi kuletwa na mtu mmoja.

Sambamba na hilo, UZALENDO lazima uambatane na ukweli. Kwa bahati mbaya sana, nchi za ulimwengu wa tatu, mambo ya ubeuzi ndio hupewa kipaumbele. Wakati mwingine unashindwa kuelewa nani mzalendo hasa, kati ya serikali na vyama vya upinzani. Kuna wakati inachanganya sana. Kama usipokuwa makini unaweza kujikuta unaegemea upande mmoja. Ni mambo gani wapinzani wanatakiwa kuyasema, na ni yepi hawatakiwi kusema? Je, kama kumetokea ubadhirifu wa mali za umma, vyama vya upinzani vinatakiwa kusemea wapi? Nini nafasi ya wananchi katika hilo? Kunyamaza kimya ndio uzalendo? Au kusema ndio usaliti au kinyume chake? Tatizo liko kwenye nini? Namna ya kusema au jambo lenyewe?.

Kuna hili, suala la vyama vya siasa. Neno vyama vya siasa nalo linachanganya. Kama utaita chama tawala, hapo ni sawa. Ni neno linaloeleweka. Lakini ukiita “chama cha upinzani” kuna ukakasi. Sijui kama tulikuwa tayari kuwa na neno “vyama vya upinzani”. Watu wengi wanaelewa kwamba vyama vya upinzani ni uhaini. Ili kutenda haki, pande zote mbili hazielewi maana ya siasa za vyama vingi. Upinzani wanaelewa kwamba kila wakati ni kupinga tu, hata kama kuna jambo jema linafanywa na serikali. Serikali yenyewe haivielewi kabisa vyama vya upinzani. Kila linalosemwa na upinzani inaonekana ni uchochezi na usaliti. Hapa neno uzalendo ndipo linajitokeza sana.

Kibaya zaidi watu wako tayari kupigana kwa ajili ya vyama vyao kuliko hata Taifa lao. Jamii imegawanyika katika makundi mawili. Kijani au magwanda!Hata jambo linalohusu Taifa/Nchi linajadiliwa katika mlengo wa vyama. Neno uzalendo hutumika kulinda masilahi ya chama badala ya Taifa. Tanzania hatuna tatizo la ukabila. Badala yake tuna tatizo la kupenda sana vyama vya siasa kuliko nchi/Taifa. Nikitazama mbele naogopa sana. Kizazi kijacho kitakuwa hatari sana, kama hili tatizo halitatuliwa.

Tuweke masilahi ya nchi/taifa mbele kuliko vyama vyetu. Sisi sote tuna wajibu wa kuona nchi yetu inasonga mbele. Uzalendo wetu uwe kuipenda nchi yetu. Kuipenda nchi yetu, ni pamoja na kutimiza wajibu wetu, ikiwa ni pamoja na kusema ukweli. Unafiki na uzalendo havifungamani. Kusema ukweli ni pamoja na kuipongeza serikali inapofanya vizuri, na kuikosoa inapofanya vibaya. Hata upande wa pili, tuwapongeze wanapofanya vizuri na tuwakosoe wanapofanya vibaya. Huu ndio uzalendo wa kweli.

“Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa, hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe. Hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao. Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu. Uliumbwa kwa udongo, unarudi tena kuwa udongo kwa udongo, mavumbi kwa mavumbi”.Walazwe mahala pema peponi wote waliokufa wakitetea nchi zao (Che, Lumumba, Amical Cabral, Samora Machel, John Garang, Kwame Nkurumah, n.k).
 
Hii nchi imekuwa ya ajabu sana kiasi unaweza tamani ukamate watu uwafunge mpaka kiama. Taifa linapita nyakati ngumu ktk kuimarisha uchumi wake ambao wakubwa walisha gawana nakutaka kutusulubu.

Sasa Mzee wa watu anasimamia masilahi mapana ya taifa hili ili vizazi vijavyo visije sema hawa wazee walikuwa wajinga kiasi gani leo majinga machache yalio zowea kula pasipo kutoka jasho wanasimama nakumkatisha tamaa Rais wetu kweli kweli jamani hivi tunafuwatilia mataifa ya jirani na africa wanavyo lia hivi kweli tunapata wapi ujasiri kumng'ong'a Rais alie jitoa kwa watu wake.

Hivi mnafikiri mtaishi milele?
Leo ngoja niwaambie kuwa huo ukuwadi wenu ukifanikiwa hata nyie hamtofaidika na mali ya dhuluma mtakayo ipata mnafikiri mnamchafuwa Rais ila wote mtakuwa uchi na mtajutia dhambi ya usaliti tunamuitaji sana huyu Rais nakuliko aina hii ya ukosoaji bora kukaa kimya au kushauri.

Hii ni laana kwa taifa nawaambia choz lake haliwezi kuwaacha salama na wala kama taifa hatuwez kuwa salama ndio maamuz ni magumu ila ktk hali ya sasa let us unity as Tanzanian.
I thank you
 
Mkuu usiumize Sana kichwa, serikali ipo kazini, vigogo wote na akina Zitto & Co LTD na takataka zote mpaka za Jamii forums zinazojaribu kuiyumbisha serikali zipo kwenye list ya follow up matata Sana.Huu mchezo hauhitaji hasira ila nakuhakikishia katika System za serikali ambazo sio za kuchukulia poa mojawapo ni ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,. mpaka June mwakani utakuwa umeelewa ninachomaanisha hapa leo,hakuna jiwe juu ya jiwe litakalosalia kinachotafutwa ni namna ya kudeal na mmoja baada ya mwingine kulingana na uzito wake.Wazungu wapo kazini ila sisi tupo DK 5 mbele yao sababu ni nchini kwetu.TAKE IT FROM ME.
 
Nadhani watu wanashindwa kutambua thamani ya walichonacho kwa sababu hawafahamu maana ya UZALENDO. Tunaomba msaada udadavue nini maana ya UZALENDO na yupoje ambaye si mzalendo na yule ambaye ni mzalendo. Asante..baada ya hapo nadhani watakuwa wakimuunga mkono Mwenyekiti wetu kama tufanyavyo sisi
 
Hii nchi imekuwa ya ajabu sana kiasi unaweza tamani ukamate watu uwafunge mpaka kiama. Taifa linapita nyakati ngumu ktk kuimarisha uchumi wake ambao wakubwa walisha gawana nakutaka kutusulubu.

Sasa Mzee wa watu anasimamia masilahi mapana ya taifa hili ili vizazi vijavyo visije sema hawa wazee walikuwa wajinga kiasi gani leo majinga machache yalio zowea kula pasipo kutoka jasho wanasimama nakumkatisha tamaa Rais wetu kweli kweli jamani hivi tunafuwatilia mataifa ya jirani na africa wanavyo lia hivi kweli tunapata wapi ujasiri kumng'ong'a Rais alie jitoa kwa watu wake.

Hivi mnafikiri mtaishi milele?
Leo ngoja niwaambie kuwa huo ukuwadi wenu ukifanikiwa hata nyie hamtofaidika na mali ya dhuluma mtakayo ipata mnafikiri mnamchafuwa Rais ila wote mtakuwa uchi na mtajutia dhambi ya usaliti tunamuitaji sana huyu Rais nakuliko aina hii ya ukosoaji bora kukaa kimya au kushauri.

Hii ni laana kwa taifa nawaambia choz lake haliwezi kuwaacha salama na wala kama taifa hatuwez kuwa salama ndio maamuz ni magumu ila ktk hali ya sasa let us unity as Tanzanian.
I thank you
Nadhani we ndo kuwadi usiejua maana ya uzalendo. Kwa mfano sheria ya pension kwa wastaafu ina lengo la kumsaidia hao mnawaita wanyonge au kumkandamiza? Wazalendo nchii ni wananchi tuz viongozi wengi ni matapeli wanajificha kwa majina ya uzalendo
 
Back
Top Bottom