Zijue faida za Mmea wa Mlonge, Jitibu magonjwa 300 kwa kutumia mlonge

Nilisoma mahali unatakiwa kutumia punje 3 za mbegu asubuhi, 3 mchana na 3 usiku na ikiwa baada ya kushiba.
 
Huwa tunasikia zina faida, japo nimegundua kuwa sikumbuki hata faida zenyewe. Ila una moyo mdau, kuguguna mbegu viganja viwili bila kujua faida kwanza....
 
Yaani mshua kanambia ile dawa aliyokuwa ananywesha kuku ni dawa ya mlonge,nikamuuliza umepata wapi akanambia eti mti uliopo nyuma ya nyumba ndo mlonge.Hata nilikua siujui

Naanza rasmi kutumia kesho na kupanda mingine mingi.
 
Kila sehemu ya mti wa mlonge ina matumizi na maandalizi tofauti na sehemu nyingine. Mfano, maua yanamaandalizi tofauti na kutibu tatizo tofauti na mizizi ama magamba ya mti huo.. Hivyo, mwongozo unaouomba hapa unategemea sehemu ipi ya mti wa mlonge unataka kuiandaa, na kwa ajili ya kutibu nini..
 
Kama upo arusha nenda pale makumbusho kuna watu wana banda lao wanauza, kama sikosei sh 5000/= kwa pakiti sikumbuki ni gm ngapi!
na kwa Dar es salaam wapo kariakoo soko kubwa kubwa ukiulizia mle ndan utaoneshwa ni elfu 5000 pia gm250
 
huu mlonge upo kkoo wakuu mbegu, majani na unga ni vizur tutumie vitu vya asili
 
Mlonge au Moringa ni miongoni mwa miti muhimu kuliko yote duniani. Mti huu ukuao haraka hupandwa katika maeneo mengi na hutumika kama chakula cha binadamu, lishe ya mifugo, tiba mbadala na kusafisha maji.

Karibu kila sehemu ya mti wa Mlonge inatumika au inalika kama chakula. Majani ndio sehemu kuu ya mti wa Mlonge, unaweza kuyala yakiwa mabichi au yakiwa yamepikwa kama mboga yoyote ya majani, na pia unaweza ukayakausha na kuyahifadhi kama unga-unga kwa miezi mingi huku ukitumia kama kiungo kwenye mboga na mchuzi.


Baadhi ya kazi chache za mlonge ni pamoja na:

Huongeza vitamini zote mhimu mwilini
Hutibu vidonda vya tumbo
Hudhibiti sukari
Huongeza SANA kinga ya mwili (CD4)
Hutibu homa za mara kwa mara
Huondoa uvimbe tumboni na mwilini
Hutibu fangasi
Huondoa wasiwasi kwa mgonjwa
Huzuia saratani ya tumbo
Huongeza utowaji wa maziwa kwa mama
Huondoa malaria
Huondoa sumu mwilini kwa haraka sana


Kuona picha na maelezo mengine zaidi yatakayokushangaza kuhusu mlonge na namna ya kuutumia, bonyeza hapa Maajabu ya Mlonge
 
Afrika tuna hazina kubwa sana ya miti itoayo dawa lakini tunaipuuzia kwa kuendekeza usasa. Ukitaka kujua faida za dawa za asili kawaulize Wachina Na Wakorea.
 
Afrika tuna hazina kubwa sana ya miti itoayo dawa lakini tunaipuuzia kwa kuendekeza usasa. Ukitaka kujua faida za dawa za asili kawaulize Wachina Na Wakorea.
Ni kweli ndugu yangu yaani hatujipendani,hatupendi hazina tuliyopewa na Mungu na hatujiamini kabisa.Kwa kweli kama kuna mtu aliyetuloga basi anajua kuloga.Ee Mungu naomba uturehemu kwani rais wetu na waziri mkuu walisema hawajui kwa nini sie ni maskini.
 
weka picha ya mlonge wengine hatuuujui,bubu siku hizi umekuwa mganga

images2.jpg

kwa hisani ya #Team weka picha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom