Uelewe mfumo wa 3-4-3 anaotumia Antonio Conte

Wana JF,

Imekuwa gumzo duniani kuhusu mfumo huu wa 3 - 4 - 3. Mfumo huu si mpya bali ulikuwepo na makocha wengi wanauelewa ila huwa hawapendi kuutumia sababu unahitaji kuwa na wachezaji wenye uwezo ufuatao:

3-4-3.jpg

Mabeki 3
Hawa mabeki 3 lazima wawe warefu na wepesi, wawe na uzoefu na uwezo mkubwa mno wa kucheza mipira hasa ya juu. Kwenye timu ya Chelsea mabeki hawa watatu ni

X3 (Azpilicueta X5 (David Luis) X2 (Gary Cahil)

Viungo 4
X4 (Ngolo Kante) X8 (Nemanja Matic) X7 (Victor Moses) X6 (Alonso)

Viungo hawa 4 wamegawanyika sehemu kuu mbili - 1. Viungo wa kati; 2. viungo wa pembeni.
Viungo wa Kati yaani X4 (Ngolo Kante) na X8 yaani (Nemanja Matic)
Hawa watakuwa na majukumu makubwa ya ukabaji na kuhakikisha wanamiliki mpira ili kuipa timu uwezo wa kwenda mbele kushambulia - X4 atakuwa nyuma kidogo kuhakikisha Ulinzi unaimarishwa na X8 atakuwa mbele kupeleka mashambulizi - hawa watacheza kwa uelewano kwamba kama X4 atakwenda mbele kuongeza mashambuzi basi X8 atarudi kuweka cover nyuma. Mfano ni ile game ya Man U - like goli alilofunga X4 (Ngolo Kante) ni uhakikishio wa ushirikiano wao kwenye kiungo cha Chelsea.

Viungo wa Pembeni yaani X6 (Alonso) na X7 (Super Victor Moses).

X7 (Victor Moses) ni kama amezaliwa upya, pongezi kubwa na Conte kumwezesha Moses kufikia kwenye ubora wake, Huyu atakuwa na majukumu ya Ulinzi upande wa Kulia, atahakikisha anasaidiana kwa kiasi na X2 kuhakikisha eneo lote la kulia ni salama, kama timu haina mpira basi X7 atarudi nyumba upande wa kulia kuhakikisha wapinzani hawapiti kirahsi kufanya maangamizi. Ubora wa mfumo huu utategemea uwezo wa X7 kupanda na kushuka - yaani awe na mapafu ya mbwa kwani kama itatokea akichoka tu ama hayupo kwenye ubora wake basi timu inaweza kupitwa kirahisi mno kupitia upande huu. So far X7 amefanya kazi kubwa mno.

X6 (Alonso); Huyu jamaa ni jembe, yupo kwenye ubora wake timilifu, kazi ya X6 ni kama ya X7 kuhakikisha ulinzi sehemu ya kushoto akisaidiana na X3. Kama timu haina mpira basi X3 atashuka zaidi kuweka cover upande wake huo wa kushoto, na kama timu ina mpira basi atapanda mbele kuongeza mashambulizi.

Washambuliaji yaani X11 (Pedro) X10 (Costa); X9 (Hazard)

X11 (Pedro); kazi yake ni kukimbiza upande huo wa kushoto, wakati timu haina mpira anaweza kushuka hadi eneo la kati kuhakikisha mpira unapatikana kwa haraka, X11 kwenye mfumo huu lazima awe mwenye mbio na kasi na uwezo kwa kuwapita ma-defenders wa timu pinzani walau wawili ama watatu - hili X11 (Pendro) analiweza saana, kukuhakikishia hilo angalia goli alilofunga kwenye game ya Tonteham - aliwageuza mabeki 2 kabla hawajarudi sawa kujua nini kimetokea mpira ulikuwa unaninginia wavuni.

X10 (Costa) Finisher, anatakiwa awe na nguvu za Kichwa, miguu - kuhakikisha anamalizia cross toka kushoto ama kulia - kwa hili X10 (Costa) kalifanya vizuri na mpaka sasa ana magori 10

X9 ( Hazaaaaaard) Huyu na wewe utamalizia - sitaki kusema sana.

Jumuisho.
Je unafikiri Mkwasa sasa ni muda wa kutumia mfumo huu??? je tunao wachezaji wenye uweo huu nchini kwa sifa nilizozitoa hapo juu??

Tujadili kwa hoja!!! namalizia kutoa hongera kwa Conte kuteta starehe siku za weekend kwa washabiki wa Chelsea.
we jamaa ni mshabiki wa chelse tu,hakuna kingine
 
Kumbe Tanzania tuna vichwa timamu kama FUSO????? Hivi kwanini tusimpe huyu fuso team yetu ya taifa aifundishe hata mwezi tu??? I pay tribute to you bro.
 
Chelsea for ever,ila naona siku tukipata forward zenye speed naona tutateseka.
 
Halafu inaonekana kadri wanavyoutumia huu mfumo ndivyo wanavyoanza kuuelewa,na uzuri wa huo mfumo unaenda ukibadirika kutegemea mpira upo wapi.
 
Ubora wa huu mfumo huu:

1. Washambuliaji yaani X11, X10 na X9 mara kwa mara watakuwa mbele hasa pembeni kuwasumbua sumbua mabeki, as resulsts mabeki wanaweza kujikuta wakifanya makosa ama kugokoa.

2. Viungo hawa 4 wanaweza kuongeza upana aka kufungua uwanja

3. Viungo na washambuliaji wanaweza kubadilishana nafasi hasa za pembeni hii kuwapa kazi kubwa mabeki kukabiliana nao. Hapa tumeshaona jinsi Hazard, anavyo switch postions na Pedro ama hata Costa

4. Ulinzi unakuwa madhubuti saha hasa katikati - mmeona jinsi David Luis na Cahil wanavyopiga kazi.

Udhaifu wa mfumo huu:

1. Wachezaji wa kiungo wanaweza kutengeneza gap (nafasi) katikati yao, hasa X7 na X6 wanapocheza nje ya sehemu yao, nafasi kubwa kati yao inaweza kusababisha timu pinzani kuitumia na kuwaadhibu mara moja.

2. Viungo lazima wapande mbele wa uangalifu mkubwa hasa wakati wa ushambuliaji, kama wakijisahau ama kupoteza mpira basi nafasi kubwa itakuwepo kati yao na mabeki, na hii nafasi itatumika na timu pinzani kuwaadhibu aka Counter attack.

Mfumo huu unahitaji nidhamu ya hali juu, kosa moja la mchezaji linaweza kuadhibu timu wakati wowote ule na ndiyo maana makocha wengi hawapendi sana kutumia mfumo huu kwa kuogopa human errors za wachezaji!!
 
n
Van Gaal alichemka Old Trafford kwa sababu hakuwa na wachezaji wanaoendana na mfumo huo
Ni kweli, lakini kiufundi kocha hajitaji kusingizia wachezaji - kocha mzuri anatakiwa awapike wachezaji hao hao waendane na mfumo anaouhitaji yeye ama unaohitajika na Club iliyompa kazi. anaweza kuruhusikiwa kununua not more than 15% to 20% kujazia - lakini Van Gaal alinunua zaidi ya 60% na matokeo yake timu haikupata ubora wowote. Sor far Conte kanunua wachezaji 3 tu classic - Ngolo, Luis na Alonso hata Pound 100 za Progba hawafikii, lakini angalia mziki wanaofanya uwanjani.

Ndiyo maana Conte alipopewa kazi Chelsea hakuruhusu mchezaji kuunzwa ama kununuliwa mpaka afanya kazi kwanza na waliopo!! wote mmeona kwamba kuna Makocha wa vitendo na Makocha wa maneno!!

Makocha wa maneno mengi wao wanapenda kununua wachezaji walio tayari hawana uwezo kwa kuwatengeneza na kufikia ubora unaotakiwa. Kwa sasa natoa hongera kubwa kwa Wenger kwa kazi nzuri ya kutengeneza, Conte pamoja na Semione Diego
 
Ubora wa huu mfumo huu:

1. Washambuliaji yaani X11, X10 na X9 mara kwa mara watakuwa mbele hasa pembeni kuwasumbua sumbua mabeki, as resulsts mabeki wanaweza kujikuta wakifanya makosa ama kugokoa.

2. Viungo hawa 4 wanaweza kuongeza upana aka kufungua uwanja

3. Viungo na washambuliaji wanaweza kubadilishana nafasi hasa za pembeni hii kuwapa kazi kubwa mabeki kukabiliana nao. Hapa tumeshaona jinsi Hazard, anavyo switch postions na Pedro ama hata Costa

4. Ulinzi unakuwa madhubuti saha hasa katikati - mmeona jinsi David Luis na Cahil wanavyopiga kazi.

Udhaifu wa mfumo huu:

1. Wachezaji wa kiungo wanaweza kutengeneza gap (nafasi) katikati yao, hasa X7 na X6 wanapocheza nje ya sehemu yao, nafasi kubwa kati yao inaweza kusababisha timu pinzani kuitumia na kuwaadhibu mara moja.

2. Viungo lazima wapande mbele wa uangalifu mkubwa hawa wakati wa ushambuliaji, kama wakijisahau ama kupoteza mpira basi nafasi kubwa itakuwepo kati yao na mabeki, na hii nafasi itatumika na timu pinzani kuwaadhibu aka Counter attack.

Mfumo huu unahitaji nidhamu ya hali juu, kosa moja la mchezaji linaweza kuadhibu timu wakati wowote ule na ndiyo maana makocha wengi hawapendi sana kutumia mfumo huu kwa kuogopa human errors za wachezaji!!
Hapo umeelezea ubora na udhaifu kwangu mimi naona kama mfumo huu haufai

Kwasababu unakufanya ucheze kwa tahadhali kubwa sana, na ndio maana makocha wengi wanauogopa ijapo kwa Conte anapata matokeo
 
Halafu inaonekana kadri wanavyoutumia huu mfumo ndivyo wanavyoanza kuuelewa,na uzuri wa huo mfumo unaenda ukibadirika kutegemea mpira upo wapi.
safi kabisa mkuu, mfumo huu ni mzuri mno ukieleweka maana unawapa wachezaji wako confidence hata kama wameshafungwa dakika za mapema, wao hutulia na kucheza mpira. Angalia Hazard anavyofanya uwanjani, Costa si yule wa ngumi ngumi tena all these because the players are enjoying their football.

Kwa mfano wanaposhambulia mfumo huu hubadika, X6 na X7 hupanda juu pembeni na kufanya washambuliaji kuwa 5. kukuhakikishia hili angalia vizuri goli alilofunga Victor Moses ile game ya Tonteham.

Pia wanaposhambuliwa mfumo hubadilika haraka sana na kuwa 5 - 4 - 1; hapa X6 (Alonso) na X7( Moses) wanarudi haraka mno kwenye ulinzi; wakati huo huo X11(Pedro) na X9 (Hazard) wana-cover sehemu walioacha X6 na X7.

Kitendo cha kupata mpira tu, wasi wanajipanga haraka sana kwenye hiyo 3-4-3 kama vile wakikimbiza mwizi kimya kimya.
 
Hapo umeelezea ubora na udhaifu kwangu mimi naona kama mfumo huu haufai

Kwasababu unakufanya ucheze kwa tahadhali kubwa sana, na ndio maana makocha wengi wanauogopa ijapo kwa Conte anapata matokeo
kaka hakuna mfumo usio na udhaufu, hata hiyo 4-4-2 inayopendwa na makocha wengi ukiambiwa udhaufu wake unaweza kulia kabisa.
 
Mambo aliyofanya Antonio Conte kabla ya kuanza kuutumia mfumo huu:

1. Alihakikisha ana mabeki wazuri (Athletic defenders) wanaoweza kucheza mipira ya juu na chini wa ustadi mkubwa.
Hapa anawatengeneza vizuri (shaping) kina Luis, Cahil na Azpilicueta.

2. Nidhamu kwa wachezaji wote hasa wa Kiungo unahitajika sana ili kupunguza uwezekano wa kupigwa counter attack, Hapa alimwongeza Ngolo konte na kumrudisha Matic kwenye ubora wake.

3. Wachezaji wa pembeni wenye uwezo mkubwa wa kuwapita mabeki walau wawili ama watatu (Ability to dribble) nakupiga crosses ndani. Hapa alimkuta Hazard, William akasema safi sana, akamtengeneza Moses ambaye alikuwepo kwa mkopo kila mwaka sababu makocha waliopita hawakuweza kujua nini ubora wake.

4. Mwisho kabisa ni kuhakikisha mawasiliano mazuri mno kati ya Mabeki na Viungo - hapa ndipo kwenye siri ya mafanikio.
 
Hhahhhahhhhahahahahaha alafu aliyegongwaa nne yupoo kilelen na kawatoa hapo waliotugonga NNE.....big conte nimekuelewaa sanaa
Unareply kwa nguvu sana cjui ndo mahaba na hyo Chel, msimu huu nan kakufunga NNE!!! Macho yako yana maj mkuu tzama vzur wanachosema wenzio, co gol nne ni nafas ya nne
 
Unareply kwa nguvu sana cjui ndo mahaba na hyo Chel, msimu huu nan kakufunga NNE!!! Macho yako yana maj mkuu tzama vzur wanachosema wenzio, co gol nne ni nafas ya nne
Mimi nia yangu si kuisifia Chelsea HAPANA, lengo langu kuu ni kuwafanya washabiki wa soccer hasa wa Bongo kuulewa vizuri mfumo huu, nini faida na mapungufu yake.

Nimeongelea sana Chelsea sababu ndiyo hasa wanaoutumia mfumo huu tena kwa mafanikio makubwa!!
 
Asante... kwa uchambuzi na jinsi ninavyofahamu ni kuwa Timu ni viungo, kwasababu wao ndo wanaoweza kutoa matokeo ya mchezo

Kwa mfumo huu kama hakuna majeruhi bila shaka Conte atakuwa na nafasi kubwa kutesa na hata ubingwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom