Tuchangie kwa nguvu zote hoja kwamba Serkali inao uwezo wa kuwalipa Madaktari Mshahara wanaodai

Udhaifu wa Kikwete ndio unafanya rasilimali zetu ziibiwe na serikali ishindwe kutimiza wajibu wake ikiwemo kuwalipa madaktari mishahara stahiki; hivi leo kama zingerudishwa hizo fedha walizotuibia na kuzificha huko nje ;je tungeshindwa kuwahudumia wananchi wetu kama wanavyostahili?Inakuwaje kwanza mpaka serikali inaachia fedha nyingi namna hiyo zinaibiwa, kama sio mipango wanayoisuka wao wenyewe?
 
Hata kama haukufikia wanaoudai, mimi ningeshauri angalau 1.6m, kwa kuanzia. Hivi kweli mtu kasoma miaka mitano. Intern mwaka mmoja; jumla miaka 6. Kazi yenyewe unaifahamu risk zake; anaanzia mshahara wa sh. 900,000 ikikatwa kodi labda anabakiwa na sh 700,000, akikatwa PSPS mfuko wa jamii labda unabaki 500,000. Hapa hajalipa nyumba ambayo hana wala hapewi. hapo hajapeleka mtoto shule, hapo hajala chakula akiwa kazini na familia wanangoja...Akija kurudi mtaani aliokuwa anawaacha kwa mbali darasani wanabadilisha gari moja hadi lingine, eti kwa sababu yuko TRA, Benki kuu nk. Hana nafasi ya kufanya chochote cha ziada kwa sababu ya kazi yao, wanashinda wodini. Mimi sio daktari lakini; surely this is not fair.

Mkuu mshahara wa laki 900000 gross Net yake ni 730000 mkuu pamoja na makato yote ya msingi kama PAYEE&SDL pamoja na PENSIONS lakini kama kuna vi chama vya madaktari nk makato yanaweza kufika hata 600000/=
 
Ebu tuambie uongo huo upo wapi? ni uongo Madaktari hawataki 7,700,000 kwa mwezi? Serikali hawana uwezo wa kulipa hiyo mishahara subirini Chadema wachukuwe nchi mtawalipa hata milioni 20 kwa mwezi.

Muulize baba yako kama serikali haina uwezo wa kuwalipa madaktari, hizo pesa mnazoiba na kuziweka huko ughaibuni zinatoka wapi? Hizo hizo mnazoiba ndio zingetumika kuwaletea waTanzania maisha bora!! Lakini kwa vile nyie ni vilaza mnafikiri mkiiba basi nyingine zitakuja kama mvua kumbe ndio mnawaumiza wadanganyika!!
 
Kazi za serikali si kulipa madk tu.Ratio ibaki ile ile 2:1 ,miaka 3 sisi makapuku na wao miaka 6. Wanajeshi wako kwenye hatari zaidi hata watu wa bima hawawataki wanalipwa sh ngapi.
 
Mkuu mimi sio Daktari lakini nadhani wanastahili walipwe kiasi hicho naamini inawezekana.

1. Kwanza ni watu ambao hawana muda maalumu wa kufanya kazi, muda wowote wanaitwa kuokoa maisha yetu bila kujali kama amelala au la.

2. Miaka ambayo anakua amespendi chuo akijifunza na pia na aina ya masomo yenyewe, inatosha kumtofautisha na fani nyingine

3. Kama wanasiasa ambao hawana impact na uhai wetu wanalipwa zaidi ya hapo, kwa nini ishindikane kwa madaktari?

4. Kama kweli serikali haina fedha hiyo, viongozi wake wanatoa wapi fedha ambazo wanafanya kufuru ya starehe ya kutembelea magari ya gharama na fedha wanazoficha nje ya nchi?

5. Kodi ambazo tunakatwa wananchi wanazipeleka wapi? Najua jibu ni kua zinasaidia maendeleo ya nchi, lakini tujiulize uwiano wa fedha zinazokusanywa na maendeleo vinalingana?

6. Kama hatuwezi kuwalipa madaktari kiasi hicho, kwa nini wamekua wakisapoti posho za wabunge zisizo na tija?

7. Kama kweli hali ni ngumu kwa serikali yetu, mbona haianzi kuonyesha kwa vitendo kwa kuanza na wao wenyewe? Naamini hata baba au mama kama hana hela, motto utagundua tu. Huwezi kumuona baba anashinda Bar na mama full matanuzi halafu akwambie hali ni ngumu. Nadhani motto utaona hilo ni change la macho!

Hayo ni mawazo yangu tu
 
Kama JK angekuwa jasiri na mtu anayesimamia kile anachoamini, siku moja aitishe mdahalo na watu wengine wakiwemo wanasiasa na wataalamu wa kiuchumi (nikiwemo mie) na mada iwe "iwapo serikali inayo au haina uwezo kuwalipa madaktari mshahara wanaodai."

Hawezi kuwa na ubavu wa kujibizana ki-hoja katika mdahalo wenye mada ya namna hiyo, yeye kazoea kuhutubia wazee tu wa Dar wasiojua kitu (wanakubali hata fisadi kuwa mwenyekiti wao!) ambao huwa tayari kumpigia makofi kwa lolote analosema.

Aidha anapenda tu kubwabwaja katika speech zake za kila mwezi ambako hakuna mtu wa kumuuliza!

I dare him aitishe mdahalo -- yeye si anajidai kujua kila kitu? THUBUTU!!!!!!
Kwenye kutaka kusaidiwa tu ufahamu hivi tuna madktari wangapi na haya madai yao unaya kadiria ni shillingi ngapi kumbuka mishahara ya 7,700,000 ni makadirio ya chini maana kuna call allowance ya laki 350,000 atujui dokta kwa mwezi anaitwa mara ngapi wala hatujui senior doctors wana demans mshahara gani tuongeze na marupurupu yao.

Halafu kuna suala la kuwajengea hizo nyumba za grade A wakati yote hayo yanatimizwa. Mimi sibishii argument yako hila naomba tu mwangaza wa rough estimate. Kumbuka raisi kesha sema sasa wanalipa mishaara ya umma 48% katika bajeti na lengo lao ni kurudi hadi 35% (kwa ufahamu kuna haja ya kutenga hela kufungua milango mengine hili kupunguza wafanyakazi serikalini) hebu wewe kama mchumi imara niweke sawa kidogo nione mbadala yako msaada tutani na figures and facts would be appreciated.

By the way CCM imezeeka na imechoka hilo silibishii
 
Back
Top Bottom