Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Huwa tunashuhudia vituko vingi vinavyotokana na uhusiano au ndoa. Hebu fikiria kwamba umemchoka mpenzi wako na unamwambia au kumwonyesha kwamba, humtaki tena, wakati yeye anahisi na kuamini kwamba, bado anakutaka.
Kwa kuona mwenzako anakutaka bado wakati wewe humtaki, unaanza kufanya visa. Hebu chukulia kwamba, unamwambia huyo mwenzako kwamba, una mwanamke mwingine, au unajidai kumuomba radhi kwamba, umefanya mapenzi nje, juzi au jana ili akasirike na kuondoka, lakini yeye hajali na ndiyo kwanza anajaribu kuhalalisha kitendo chako hicho na kukuhakikishia kwamba amekusamehe. hamna shida mume wangu mpenzi nimekusamehe, najua ni shetani amekupitia tu, kwani sio tabia yako kabisa kunisaliti . Atasema hivyo akimtetea mume mzinifu.
Unadhani utafanyaje?
Kumbuka kwamba, kuna watu wengi sana ambao huwafanyia visa wapenzi wao ili wachoke na kukereka sana na hatimaye kuamua kuondoka. Kuna wakati visa hivyo hufanikiwa na kuna wakati hugonga ukuta kwani mpenzi anakuwa havijali. Hebu tujiulize kwa dhati, inasaidia nini kama tumechokwa na sisi kuendelea kungangania kwa wale tunaowaita wapenzi wetu. Kuna wakati wanaume au wanawake huamua kuwauwa wapenzi wao ili kuwa huru kutoka kwao. Wanaambiwa kwa kauli, sikutaki, halafu wananza kufanyiwa visa, lakini wamo tu, hawataki kuondoka. Hatimaye, mtu anaamua kuuwa kabisa.
Kuna wakati mpenzi anaambiwa kabisa na mwenzake kwamba hatakiwi, lakini yeye anasema, tutabanana humu humu hatoki mtu hapa. Bila shaka hiki ni kichaa cha aina fulani. Mtu akishasema sikutaki, maana yake hakuna tena kinachoweza kuwaunganisha, yaani hisia za upendo. Kulazimisha kuishi na mtu asiyekutaka ni kujifanya mtumwa bila sababu. Inabidi tuamke na kuwa sisi kamili kabisa.
Ndoa za Kiislamu zina uzuri mmoja .. mke au mume akimwambia mwenzake sikupendi au sikutaki tayari ndoa hiyo inahesabika kuwa batili. Bila shaka huu ndio ukweli ambao inabidi tuukubali kwa mkabala wa hisia na tabia za binadamu. Kulazimisha kuishi na mtu asiyekupenda ni kujiingiza matatizoni