Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,997
- 1,163
Umeneno vema Mkuu Pasco. Tatizo lililopo ni kuwa watu wanashindwa kuyazungumzia matatizo wanayotaka yatatuliwe. Labda walifanya hivyo lakini hawakufanikiwa na sasa wanaanza kutafuta visingizio. Kama hawajui basi wanapaswa kuambiwa kuwa wanaiharibu hoja yao ya msingi ya kutaka kero za muungano ziangaliwe na kutatuliwa ipasavyo, si kwa kuleta kisingizio kuwa Muungano si halali. Kama Muungano si halali wanapaswa wajiulize wao wanazungumza kutoka kwenye paltform gani?Mzee Mwanakijiji, ni bahati mbaya sana, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, hauna mkataba wowote in a real sense ya mkataba wa kimataifa kati ya mataifa mawili huru. Tukishakubaliana kwamba hakuna mkataba kabisa, hapo ndipo ilegitimacy ya muungano ilipoanzia. Kilichopo sio mkataba wa Muungano bali ni makubaliano ya muungano, not a contract but only agreement just like MOU.Pamoja na kutokuwepo huo mkataba, mimi ni muumini wa Pan-Africanism kuwa Waafrika ni wamoja ila ni wakoloni ndio wamekuja kutuwekea mipaka. Hakuna ubishi Wahaya wanabelong chini ya Kabaka Empire enzi za Interlucustrine Kingdom ambapo kina Mkama Rumanyika were part and parcel, bali ni mkoloni ndiye aliyekuja kupiga mipaka wahaya kujikuta wako huku na Waganda kule, sawasawa na Wamasai wa Kenya na Uganda ni wale wale.Hatuhitaji paperwork documents be it hati au mkataba kuonyesha tumeungana, kama yalivyo mapenzi ya kweli toka enzi za mababu, hatukuhitaji hati/cheti cha ndoa kuthibitisha mapenzi na ndoa ni mpaka waipokuja wazungu na macheti yao.Hivyo Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulizaa Tanzania, hauhitaji paper work be it hati/mkataba ili kuuhalalisha, hata pale Nyerere na Karume waliposemezana tuu wao kwa wao ilitosha bila kuandika chochote popote. Tatizo hizi zote mbili zilishakuwa nchi huru kwa mujibu wa wazungu, mambo yanakwenda kwa hati na maandishi na ikibidi wananchi washirikishwe kitu ambacho hakikufanyika kwa mujibu wa taratibu.Kwa maoni yangu, Wanzanzibari ni wanafiki wa hali ya juu sana, kama waliukubali Muungano bila kuleta fyoko fyoko yoyote, iweje leo wakapitisha kura ya maoni kuulizia jambo dogo jema la kuwaletea umoja miongoni mwao, na wasitake kutumia fursa hiyo ya kura ya maoni kuwauliza Wanzanzibari jambo kubwa kama hili la Muungano na nchi nyingine?!.