Shairi: Tatizo La Muafrika

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298
TATIZO LA MUAFRIKA.

1)tulivyofanywa watumwa,tulikuwa hatuoni.
Wajinga waliotumwa,walipita baharini.
Ingawa mengi yasemwa,hatuyaweki kichwani.
Tatizo la muafrika,achukia sura yake.

2)hatujali rangi zetu,ndo kwanza twabaguana.
Hatuvijali vya kwetu,kwa nguvu twaumizana.
Iko wapi mila yetu,mbona tunachukiana.
Tatizo la muafrika,achukia sura yake.

3)demo zetu ni ghasia,alishayasema maembe.
Mengi mkamzushia,mkamuona mzembe.
Ona tunavyoumia,kwa lipi di tujipambe.
Tatizo la muafrika,achukia sura yake.

4)kwingine kuna baridi,Afrika yashikwa vita.
Tumekuwa wakaidi,kwa hilo hatujasita
Tumezizika juhudi,kwa mara elfu na sita.
Tatizo la muafrika,achukia sura yake.

5)njaa zetu za ajabu,iweje ziwe kichwani.
Wakati wale mababu,zao ziliwa tumboni.
Hatuna wala sababu,ni akili tu hazioni.
Tatizo la muafrika,achukia sura yake.

Shairi=TATIZO LA MUAFRIKA
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Facebook page=Idd ninga mashairi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom