Tatizo la kupata choo kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation). Fahamu chanzo na tiba yake

Nina tatizo la kupata choo mara chache naweza pitiliza siku mbili hata tatu bila kupata choo, ila chakula nakula kama kawaida. Je? nisaidieni sijui tatizo nn? na nilitatueje?
 
Baadhi ya mambo yawezayo kukusaidia ni pamoja na kufanya mazoezi mara kwa mara, kunywa maji mengi, kula vyakula vyenye roughage mfano mboga za majani nk. Hayo yasipokusaidia nenda hospitali.
 
Sina ushaidi wa ki science ila mahindi ya kuchoma malaini niliambiwa ni dawa safi sana na nilipotumia mkuu The results was Good
 
Kunywa maji glas 2 asubuhi wakati wa kuamka, nusu saa kabla ya meal kunywa glas 1, kabla ya kwenda kuoga kunywa glas 1, kabla ya kulala kunywa glas 1. Hii inasaidia kusafisha digestive system na kukinga dhidi ya heart diseases. Pia kula vyakula vyenye lougheges kama alivyochangia mdau hapo juu. Ikiambatana na tumbo kuuma, kutapika na kuto jamba kabisa nenda hospitali yawezekana ikawa intestinal obstruction. Pole
 
nina tatizo la kupata choo mara chache naweza pitiliza siku mbili hata tatu bila kupata choo, ila chakula nakula kama kawaida....Je? nisaidieni sijui tatizo nn? na nilitatueje?

Thats normal, na sidhani kama una tatizo lolote. one can go up to five-six days na still ni kawaida. Depends na chakula unachokula na kazi unayofanya, and the rate of body utilization of food, mahitaji ya mwili.
ni hali ya kawaida. Kama kuna shida nyingine sambamba na inayoshabihiana na hiyo nenda muone mganga.
 
Nashukuru sana kwa ushauri mzuri nilioupata kutoka kwa wana JF
kwani ni matumani yangu Muda si mrefu mambo yatakuwa sawa kwani
nimeshaanza kuufanyia kazi.
Asanteni sana
 
hamna cha kuanza kufanyia kazi.we kunywa juice ya ukwaju bilauli 2 asubuhi,2mchana,2jioni.halafu kesho yake njoo useme.
 
nina tatizo la kupata choo mara chache naweza pitiliza siku mbili hata tatu bila kupata choo, ila chakula nakula kama kawaida....Je? nisaidieni sijui tatizo nn? na nilitatueje?

natamani ningekuwa wewe. Sikipendi hicho choo.
Matunda + maji yanasaidia.
 
nina tatizo la kupata choo mara chache naweza pitiliza siku mbili hata tatu bila kupata choo, ila chakula nakula kama kawaida....Je? nisaidieni sijui tatizo nn? na nilitatueje?

tatizo la kukosa choo linasababishwa na mambo haya,ukosefu wa wanga,ukosefu wa matunda,kukosa maji,kutokufanya mazoezi,hofu,figo,damu kupungua,mimba nk.jicheck upungufu upo wapi?
 
...Juice ya Ukwaju ni dawa nzuri: Fanya hivi: Nunua kilo moja ya Ukwaju, chemsha maji masafi then tia ukwaju ndani ya hayo maji moto, then chuja hayo maji ktk chombo safi ubaki na juice yake hasa ule uji uji. kunywa glasi ya maji, then kunywa glasi moja ya juice ya ukwaju, kunywa tena glasi ya maji then kunywa glasi mbili za juice ya ukwaju na malizia na glasi moja ya maji. baada ya nusu saa utaharisha sanaaaa.
 
Huo ushauri woote unafaa na ni mzuri,,,lakin juise ya ukwaju jibu lake ni fasta fasta ,,ukinywa mara moja unajisaidia na uzuri wake utajisaidia uchafu woooooooote hata ule wa akiba wote utatoka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom