Abdulhalim
Platinum Member
- Jul 20, 2007
- 17,193
- 3,011
Abdulhalim,
Mimi ni mpentekoste,
Ndugu yangu Abdulhalim, haikusaidii kuendelea kutetea dini ambayo msingi wake si katika Neno la MUNGU. Fungua moyo wako kwa utayari wa kutaka kuujua ukweli ili Roho wa MUNGU aweze kukusaidia kuujua huo ukweli ili uweze kuufuata. I used to be a faithful RC member lakini nilijiachia kwa MUNGU anifundishe zaidi na sikuwa tayari kung'ang'ania dini. Na kweli neema ya wokovu ilifunuliwa kwangu nikaokoka na sasa nafurahi ndani ya YESU.
Sikiliza maneno haya ya YESU yanaweza kukufungua macho.
Matthew 15 (Amplified Bible)
6So for the sake of your tradition (the rules handed down by your forefathers), you have set aside the Word of God [depriving it of force and authority and making it of no effect].
7You pretenders (hypocrites)! Admirably and truly did Isaiah prophesy of you when he said:
8These people draw near Me with their mouths and honor Me with their lips, but their hearts hold off and are far away from Me.
9Uselessly do they worship Me, for they teach as doctrines the commands of men.
Karibu ndugu yangu katika wokovu tujiunge pamoja katika safari ya kwenda mbinguni.
Mazee kwanza futa mawazo kuwa nitaacha kuwa muumini wa kikatoliki.. Suala la wewe kuuacha ukatoliki wako haliingii ktk huu mjadala, huo ulikuwa uamuzi wako na katu hauwezi kutumika kama reference. Dhihirisha hoja kwa hoja, na wala usitegemee kuniletea lundo la vifungu ulivyovikariri kuni-convince..i know what i believe na niko very comfortable na imani yangu ya kumfuasa Kristu..hilo la kwanza. Tuwe focused kwenye hoja, mahubiri hapa si mahala pake.
Pili nataka tuongelee hili suala la kulazimisha kila kitu lazima kiandikwe kwenye Bible..Labda hapa twende taratibu tuone maandiko yanasemaje?
Tukisoma aya ya mwisho kabisa ktk injili ya Yohana Mtakatifu sura ya 21 aya ya 25 tusoma, nanukuu:
John 21:25. And there are also many other things which Jesus did, the which, if they should be written every one, I suppose that even the world itself could not contain the books that should be written. Amen
Unaweza pia kutembelea zaidi John 20:30, etc..
Hapa tunasoma kuwa sio kila kitu alichofanya Bwana Yesu kimewekwa kwenye maandishi,(Bible) Pia inasisitizwa kuwa kilichopo kwenye maandishi ni kidogo mno na kisichopo kwenye maandishi (Nje ya Bible).
Pili,ukisoma historia inayoelezea jinsi gani Bible imeweza kuwa ktk hali yake ya sasa kwa maana ya mkusanyiko wa vitabu, utakuta kuna vitabu kadhaa vilikuwepo kipindi hicho lakini havikuweza kukubalika kwa sababu moja au nyingine kuwemo ndani ya Bible. Hivi pia ni vyaweza kuwa vyanzo vizuri vya habari za Yesu.
Tatu, kama tunavyoamini kuwa Kanisa la Mungu li hai kama alivyo Kristu mwenyewe, hivyo basi Roho Mtakatifu bado anafanya kazi yake kwa ari ileile kama ilivyokuwa siku ya Pentekoste..Kazi za Roho Mtakatifu ni pamoja na kulifunza kanisa na ndio maana Kanisa lina document literature yake ktk kutoa muongozo wa kiroho..hiki pia ni chanzo kingine cha mafundisho ya Kanisa Katoliki...
Nimeshatoa vyanzo vitatu hapo juu, jinsi gani tunaweza kupata maneno ya Mungu. Ukitazama hapo utagundua kuwa hoja kuwa eti wakatoliki wanafuata maagizo ya kibinadamu si tu haina mashiko bali ni kichekesho. Ndugu kumbuka kuwa Yesu aliweka msingi wa Kanisa, hakuweka msingi wa Bible, Bible si kila kitu ..bali kanisa ndilo, maana humo ndimo watu tunapata wokovu.. Kanisa la kwanza liliandika Injili 4 na sio Maandishi ya Injili yaliyoweka Kanisa..hivyo ni vyema ukaelewa misingi hii bila kufanya uelewa wa kinyumenyume.
Kama kuna la ziada unakaribishwa nimejitahidi kuweka in summary tu.
Wakatabahu.