Biashara ya Saccos

Naomba anayejua ni process gani, na ni wapi na document pamoja na vitu vitu gani vinavyohitajika ili kufungua SACCOS anielekeze hapa jukwaani.
Natanguliza shukran

Nenda makao ya wilaya ulipo na onana na afisa ushirika utapata maelezo na forms
Kuanzisha saccos ni wilayani
 
salaam ndugu wana jamii!

Mimi ni kijana, napenda kuwa mjasiria mali kwa kukuza uchumi wangu na jamii kwa ujumla.

Kwa kushirikiana na vjana wenzangu, tumeamua kuanzisha kikundi chetu cha biashara.

Je, ni taratibu gani tupaswa kuzifuata ili kusajili jina la kikundi chetu cha biashara ili kiwe na utambuzi wa kisheria?
1.tunatakiwa tuwe na nini/vigezo
2.tunatakiwa tuende kwa nani (ngazi za kiutawala serikalini).
 
LIMENSE IYO LIKITONTA!
kama unataka kampuni nenda BRERA au Kama ni SACCOS muone Afisa ushirika karibu yako kwani mpo wapi!
 
Inategemea unataka kusajili nini. Kama ni chama cha ushirika au ...? Vikundi kama vikundi vinasajiliwa idara ya mambo ya ndani. Ukifika hapo watakueleza vigezo vya kufuata. Lakini kwa nini msianze kufanya hicho mnachotaka kufanya bila kujisajili? Andaeni sheria au katiba ambayo kila mtu ataifuata mkianisha madhumumuni ya kuanzisha hicho kikundi, mantaka kufanya nini, mtakifanyaje hicho mlichodhamiria na sheria ndogo ndogo ambazo kila mtu atafuata. Mkisimia katiba yenu mtafanikiwa.
salaam ndugu wana jamii!

Mimi ni kijana, napenda kuwa mjasiria mali kwa kukuza uchumi wangu na jamii kwa ujumla.

Kwa kushirikiana na vjana wenzangu, tumeamua kuanzisha kikundi chetu cha biashara.

Je, ni taratibu gani tupaswa kuzifuata ili kusajili jina la kikundi chetu cha biashara ili kiwe na utambuzi wa kisheria?
1.tunatakiwa tuwe na nini/vigezo
2.tunatakiwa tuende kwa nani (ngazi za kiutawala serikalini).
 
Mimi nilikuwa afisa ushirika nimekuwa kiongozi na mwanzilishi wa saccos kwa miaka 20. Sasa hivi natoa ushauri wa biashara NGO na SACCOS. SACCOS kirefu chake ni Savings and credit cooperative society. Kiswahili ni chama cha ushirika cha akiba na mikopo. naomba nikupe habari kamili katika taarifa hii hapa chini ili ujue nini unachotafuta kwenye SACCOS na historia yake. Kwa kifupi unataka kuanzisha asasi ya kifedha endelea kusoma mchakato unaohitajika

Watu wengi wanafikiri kufanya biashara ya fedha au kuanzisha taasisi za kifedha ni kazi ngumu. Hali siyo hivyo katika dunia ya sasa. Mfumo wa kifedha ninaozungumzia hapa siyo benki kubwakubwa za biashara. Ninazungmzia benki ndogondogo za wananchi, vikundi au vyama vya ushirika vinavyoendesha asasi za kifedha. Asasi hizi zinaitwa SACCOS au SACCA, SACCOS ni vyama vya ushirika vya akiba na mikopo na SACCA ni NGO zinazotoa huduma za kifedha. Kati ya asasi hizi SACCOS ndiyo ambayo ni rahisi kuanzisha. Historia ya vyama vya ushirika vya akiba na mkopo inanzia kipindi cha mapinduzi ya viiwanda huko Ulaya kutokana na ugumu wa maisha na ugumu wa upatikanaji wa mikopo toka benki kwa wanyonge, watu hawa wafanyakazi na wakulima wadogowadogo waliamua kuungana na kuchangisha fedha kidogokidogo na kisha kuanza kukopeshana. Hali hii hata hapa kwetu Tanzania iko hivyo. Wale wanyonge, wakulima na wafanyakazi siyo rahisi kupata mikopo benki. Hawawezi kukopa toka Benki kutokana na masharti magumu wanayowekewa na Benki. Suluhisho la Kujikwamua kiuchumi kwa wanyonge ni kuanzisha SACCOS. Mfumo huu wa SACCOS unaweza kuanziswa sehemu ambapo kuna mkusanyiko wa watu wanaofahamiana na wanafanya shughuli zinazofanana, kwa mfano wafanyaazi wa kampuni au ushirika fulani, wafanyabiashara wa sehemu fulani, wakulima wa vijiji fulani au waumini wa dhehebu au dini fulani wakiwa na nia hiyo wataitisha mkutano ambao utasimamiwa na Afisa Ushirika na kupitisha azimio la kuanzisha SACCOS. Watatuma maombi ya kusajili SACCOS na kuanza kuchangishana. Baada ya kupata usajili, kutoa mikopo kutahitaji subira kidogo ili mikopo itolewe baada ya chama kuwa na akiba ya kutosha baada ya kukusanya akiba ikianzia miezi mitatu hadi sita.

Mikopo inayotolewa itatozwa riba ya silimia 2.5 na inaweza kuwa ni ya dharura kwa ajili ya biashara, ujenzi, ufugaji na kilimo na kadhalika. Vyama hivi vimewasaidia sana wanachama wake kujikwamua kiuchumi. Faida ya kuvianzisha ni kwamba SACCOS inaweza kukopa toka Benki kama imesajiliwa na kutoa mikopo kwa wanachama wake. SACCOS ina wafundisha wanachama wake kuwa na tabia ya kuweka akiba. Zikiendeshwa kwa makini na uaminifu mkubwa SACCOS zinaweza kugeuka na kuwa Benki kamili na kumiliki vitega uchumi kama majego na magari na pia kutoa ajira. Matatizo ya biashara hii ni kukosekana kwa uaminifu kwa wanachama na viongozi katika masuala ya uendeshaji na utoaji mikopo, hivyo kufanya vyama hivi kutokuwa na maendeleo. Ufumbuzi wa matatizo ya SACCOS ni kutoa elimu ya ushirika ili kuwe na mwamko wa wanachama katika kusimamia uendeshaji wa vyama hivi.

Kwa ushauri zaidi nipigie 0755394701

Zainab Tamim, pitia hapa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom