Wanasayansi nchini Marekani wametengeneza roboti inayofanana na mende

Primier

Member
Dec 16, 2015
86
14

9e23461c6.jpg


Roboti inayoiga Mende
Wanasayansi nchini Marekani wametengeneza roboti inayofanana na mende ambayo inaweza kutumiwa kuwaokoa watu kunapotokea tetemeko la ardhi.

Watafiti wanasema roboti hiyo inatumia mbinu zinazotumiwa na mende kutembea kwenye nyufa kupenya vifusi na kuwaokoa walionaswa katika maporomoko.

Wanasayansi hao wanasema kuwa endapo roboti hiyo inawezavishwa kamera kisha ikatumwa kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka inaweza kurahisisha uchunguzi wa usalama wa vifusi kabla ya makundi waokoaji kuingia.

Ukubwa wa roboti hiyo ni sawa na kiganja cha mwanadamu.

Image copyright Tom Libby Kaushik Jayaram and Pauline Jennings
Image caption Watafiti wanasema roboti hiyo inatumia mbinu zinazotumiwa na mende kutembea kwenye nyufa
Roboti hiyo inaweza kupenyeza katika mianya midogo maradufu ama nusu wa ukubwa wake.

Miguu yake inapanuka kama vile mende.

Utafiti huo umechapishwa katika jarida la kisayansi lijulikanalo kama ''Proceedings of the National Academy of Sciences''.
 
Wanasayansi nchini Marekani
wametengeneza roboti inayofanana na mende ambayo inaweza kutumiwa kuwaokoa watu kunapotokea tetemeko la ardhi. Watafiti wanasema roboti hiyo inatumia mbinu zinazotumiwa na mende kutembea kwenye nyufa kupenya vifusi na kuwaokoa walionaswa katika maporomoko. Wanasayansi hao wanasema kuwa endapo roboti hiyo inawezavishwa kamera kisha ikatumwa kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka inaweza
kurahisisha uchunguzi wa usalama wa vifusi kabla ya makundi waokoaji kuingia. Ukubwa wa roboti hiyo ni sawa na kiganja cha mwanadamu. Roboti hiyo inaweza kupenyeza katika mianya midogo maradufu ama nusu wa ukubwa wake. Miguu yake inapanuka kama vile mende. Utafiti huo umechapishwa katika jarida la kisayansi lijulikanalo kama ''Proceedings of the National Academy of Sciences''. Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom