Profesa Safari ang’atuka CUF

Ernesto Che

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,114
293
ALIYEWAHI kupambana na Profesa Ibrahim Lipumba kwenye kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya mwenyekiti wa CUF,
Profesa Abdallah Safari, amejivua uanachama wa chama hicho.

Taarifa ambazo zilipatikana jana na baadaye kuthibitishwa na Profesa Safari, hazikubainisha sababu za kujitoa kwake kwenye chama hicho na kwamba, anapanga kuanika hadharani keshokutwa.

“Pamoja na kwamba zipo sababu za mimi kufikia uamuzi huu, lakini kwa leo (jana) siwezi kueleza chochote zaidi ya kutangaza nimejiondoa CUF,’’ alisema Profesa Safari na kuongeza: “Kesho kutwa (Alhamisi) nitatangaza rasmi azma yangu ya kujivua uanachama wa CUF.’’ Profesa Safari ambaye ni mwanazuoni aliyebobea kwenye taaluma ya sheria, alijiunga CUF mwaka 2005 na Februari 2009, aliwania uenyekiti na Profesa Lipumba akaambulia ushindi kura sita.

Alisema amefikia uamuzi wake huo kwa utashi wake, bila kushinikizwa na mtu. “Napenda wananchi waelewe kuwa uamuzi huu, nimeufikia bila shinikizo lolote,’’ alisema Profesa Safari.

Hata hivyo, Profesa Safari alieleza kuwa pamoja na kung'atuka kwake CUF, ataendelea kuwa mwanasiasa bila kueleza atashabikia chama atakachoshabikia. Uamuzi huo ameufikia ikiwa ni takriban mwaka mmoja na nusu baada ya kuangushwa vibaya kwenye kinyang’anyiro cha uenyekiti wa CUF na Profesa Lipumba aliyepata kura 646.

Kufuatia matokeo hayo, Profesa Safari aliwashtumu wajumbe wa mkutano mkuu kuwa, walimdhalilisha na angeandaa kitabu kueleza udhalilishaji huo. Februari 23, 2009 wakati Profesa Safari akijieleza katika mkutano mkuu wa kuchagua mwenyekiti wa CUF, wajumbe walikuwa wakimzomea na baadaye kumrushia maswali yaliyomtingisha, ikiwamo kumtaka kutaja jina la katibu wa tawi lake. “Nimedhalilishwa; nimezomewa; nimeulizwa maswali ya kipuuzi.

Ule ni uhuni hakuna kitu pale,” alisema Profesa Safari na kuongeza: “Wajumbe wa mkutano mkuu wa CUF wamepotosha na kuharibu maana ya demokrasia ndani ya CUF na kutumia vibaya nafasi hiyo ya kuchagua viongozi.” Alipobanwa kueleza iwapo anafikiria kuwania tena nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama hicho, Profesa Safari alisema hawezi na hana nia ya kuwania uongozi wa chama hicho.

Hata hivyo, taarifa ambazo zilikuwa zikisikika ni kwamba, Profesa Safari alikuwa haelewani na uongozi wa CUF hasa baada ya kuhoji taratibu zilizotumika kati ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume kusaini mkataba wa siri kuunda ya umoja.

Source: MWANANCHI Monday, 17 January 2011 20:12

Maoni yenu wa JF
 
safi sana mkuu usikubali kuburuzwa,simamia haki kwanza chama chenyewe kimepoteza mwelekeo kukubali kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ni nisawa na kusaliti demokrasia
 
What is supposed next move? CCM? Sitegemei hilo kwani ni activist mzuri...
 
wana JF tumemuogopesha Pro. kuja CDM? maana wengi tulishabikia kuwa akija CDM ataondoa ile dhana ya UDINI uliokithiri CDM.

au anatafakari upya?
 
wana JF tumemuogopesha Pro. kuja CDM? maana wengi tulishabikia kuwa akija CDM ataondoa ile dhana ya UDINI uliokithiri CDM.

au anatafakari upya?

Well akija huko anamsubstute Zitto? maana inaonyesha kule anakotoka aliudhiwa kutokana na wajumbe wa baraza kuu kumkataa na kumpa kura 6 sasa huko wajumbe watakuwa tayari kumpa kura nyingi?

Uamuzi huo ameufikia ikiwa ni takriban mwaka mmoja na nusu baada ya kuangushwa vibaya kwenye kinyang'anyiro cha uenyekiti wa CUF na Profesa Lipumba aliyepata kura 646.
 
Sidhani kama atakuja CDM just kutafuta cheo, hata CCM, kama ndivyo is very mistaken
 
CUF Bara in the making!! athari za Mwafaka wa mama karume na Maalimu seif zinaanza kuonekana. Safari hawezi kuacha siasa kamwe, kama harudi CCM na si CUF Bara kuanzishwa, kwa taaluma yake ya sheria, he is going to BAKWATA---dreaming of being kadhi????
 
CUF Bara in the making!! athari za Mwafaka wa mama karume na Maalimu seif zinaanza kuonekana. Safari hawezi kuacha siasa kamwe, kama harudi CCM na si CUF Bara kuanzishwa, kwa taaluma yake ya sheria, he is going to BAKWATA---dreaming of being kadhi????

Tatzizo linalomuondoa kafu si mwafaka ni uongozi kwani huo mwafaka umefikiwa kafu walikuwa tayari wameshampa kura 6. Muhimu ameona hapamfai kama alivyoona Letcia Musori na kuondoka aheshimiwe uamuzi wake full stop!
 
mkuu...post kama hii zipo zaidi ya tatu tangu jumatano kbla hata hajatangaza kujivua uanachama... na amejivua uanachama alhamisi.....
 
Hii taarifa mbona imo humu kwenye jamvi kuanzia juzi....................sasa itakuwaje ni habari mpya.................................
 
PROF. ABDALLAH SAFARI AJIVUA UANACHAMA CUF - Global Publishers



Nadhani msomi huyu amegundua kuwa CUF sio wapinzani tena..

more updates coming, stay tuned.

Kilichomtokea Prof Safari alinyimwa uongozi kama alivyonyimwa fursa ya kugombea ubunge Dr Slaa kwa tiketi ya CCM na kuhamia CDM. Kwahiyo hapo tatizo ni "ulwa" cheo. Nadhani itakuwa jambo la busara atakapohamia asainishane nao MoU wampe madaraka aliasije kukimbia na huko au abaki kwenye taaluma yake.
 
Itakuwa wise akitulia kwanza afikirie nini cha kufanya na wapi pa kwenda, sio kukurupuka. Profesa ni mwanamapinduzi wa kweli hata serikali ikimbania fursa zote.
 
Back
Top Bottom