Power Mabula: Mtu aliyetikisa enzi zake!

Naombeni mnikukmbushe, hivi mzee mwinamila alikua nani vilee, hilo jina nalikumbuka.
Marehemu Mzee Mwinamila (Mzee Saleh Ramadhan Mwinamila), alikuwa ni kiongozi wa kikundi cha ngoma, kilichojulikana kwa jina la 'Hiari ya Moyo'. Iki kikundi kilianzishwa mwishoni mwa miaka ya 1950, nazani mwaka 1957 kama nakumbuka historia vizuri. Na ni ngoma za kabila la watu wa Tabora (Wanyamwezi). Iki kikundi kilikuwa kama kikundi cha kitaifa, serikali ndio walikuwa wakiwapa pesa na kikitumbuiza kwenye dhifa mbali mbali za kitaifa.
 
Nakumbuka kulikuwa na magwiji wa nyimbo zenye maadili sana kipindi icho, Mzee mwingine ni Mzee Makongoro na nyimbo zake.

Kuna huu naukumbuka beti zake chache... unaitwa "Madereva",

Unaanza hivi..."Mtikisiko wa Wimbi, Maji Ya Kipwa Kimbia, Ukimsifu Mgema Tembo ulitia Maji... Madereva wenye fujo yafaa kuwakimbia.

Kibwagizo: Dereva kalewa pombe! haa! Sawa hiyo!?
Waitikiaji: Haataa, hiyo si sawa dereva wacha vituko!

Nyingine:
Kuleni kuku, mayai, mboga, samaki, maziwa, Na kujenga nyumba safi pa kulala pawe bora!
 
Nimekumbuka beti moja ya wimbo wa Mrehemu Mzee Mwinamila:

Upo hivi... "...Twaimba nyimbo…! Twaimba nyimbo mwisho wake tutakufwa lofwa...!

Sikumbuki tena muendelezo wake.

(hapa alikuwa na maana wanaimba nyimbo lakini matokeo yake mwisho watakufa masikini/lofa).

Na ni kweli, waimbaji wengi wa zamani na hata wa siku hizi mwisho wake wana sahaulika na wanakuja kuwa omba omba.
 
Hata mimi nakumbuka sana huyu PAWA MABULA miaka ya 1985 hadi 1992 alikuwa akiwika tu,ila tangu nyakt ile mpk hv ndiyo nimekuja kumsikia humu jamvini. Ila nafikiri ile fani atakuwa ameacha bila shaka na anaweza akawa miaka hii ni mzee sana. Mwenye kumjua a2juze zaidi wanaJF.
 
Duh! umenikumbusha mbali kweli enzi za shule ya msingi.
Pia kulikuwa na profesa mmoja wa kihindi anakupa ndizi waila halafu anapasua tumbo live na kutoa ndizi iliyoliwa sijui walikuwa wanatudanganyaje? mazingaombwe ya zawadi za biskuts, chupi na vitu kibao watoto mnapewa duh kazi kweli

Duuh, umenikumbusha mbaali! Huyu jamaa nilimwona shule ya msingi, akapotea kwa muda mrefu, nikaja kumwona tena shule ya sekondari. Alikuwa na mtindo wa kuwapaka poda 'subjects' wake na pia kuwapiga vibao.
 
Mmenikumbusha mbali wakuu! "Enzi za wewe ni nani?" - "Mimi ni chipukizi wa TANU/Mapinduzi" ...
Enzi hizo baada ya mechi kali za ligi kuu, ikifika saa mbili kasorobo ya usiku masikio ya wengi ktk redio (RTD). Watangazaji wanaanza kwa mafumbo, mf, "Huko uwanja wa Taifa, mla ni mla leo, mla jana kala nini?". Au "Jangwani/Msimbazi kwaenda kilio". Hapo wengine wanaanza kushangila, wengine wananyongea.
 
Very interesting, nimewahi kumshuhudia miaka ya 1982/3 nikiwa primary Singida mjini huyu bwana alikuwa mwanajeshi, alikuwa na uwezo wa kuvuta magari mawili kwa kuyazuia yasiondoke kwa kutumia mikono yake, magari yakiwa yanakwenda pande tofauti yeye akiwa katikati na kweli magari yalikuwa hayaondoki. Yalikukuwa yakiishia kuunguruma tu bila kufanikiwa kuondoka!!
 
Umenikumbusha enzi za mapawa na maprofesa (wanamazingaombwe). Power Mabula was one of my favourite, kulikuwa na power mwingine anaitwa Power Ngeta, huyu akija tulikuwa tunaimba "Power! Ngeta! Super! Kibongeeee!" Sijui yuko wapi naye huyu.

Kuna dogo tulikuwa tuko naye darasani alikuwa ni fundi wa kutengeneza mihuri (inayogongwa mkononi kama unatoka nje mara moja na utarudi), basi wale maprofesa wakija dogo naye anatengeza na kutugongea mikononi watu wanaotaka kuingia bila kulipia. Baadae ukitoka unampa shilingi 5 au unamnunulia vipande vya mihogo. Tulikuwa tunainjoi sana maisha yale.

dah pawa super kibonge. Niliwahi kupewa ndizi na professor Singila nikainya wee nililia hadi home.
 
Ki ukweli Power Mabula ameokoka na yupo Tabora ndiko anakofanyia shughuli zake hy alikuwa mwalimu wa mazoezi ya kunyanyua vitu vizito kwa br wangu
 
Kweli bwana umetukumbusha mbali maana hata mimi nilimshuhudia kipindi hicho nikiwa Njombe nilikuwa nasoma Mpechi shule ya msingi ingawa sikumbuki jina la uwanja lakini ilikuwa karibu kabisa na mahali tulipokuwa tunaishi.

Kwa kweli maisha ya kizamani yalikuwa na raha yake tulikuwa tunachakachuliwa viini macho hatuoni halafu wenyewe tunafurahi, maisha yalikuwa na amani. Siku hizi tunachakachuliwa mioyo na macho yanaona, Maisha yamekuwa hayana amani na machungu kuangalia ni wapi tunakokwenda.
 
Jamani naomba kujuzwa, wakati nakua kulikuwa na simulizi za mtu aliekuwa anajulikana kama Power Mabula ambae alikuwa anasifika kwa kufanya mazingaombwe mfano walisema eti alikuwa na uwezo wa kulala barabarani gari ikamkanyaga lakini akatoka ni mzima na pia alikuwa na uwezo wa kunywa ndoo nzima ya maji na stori nyingine za namna hiyo. Hivi ni kweli huyu mtu alikuwa anaishi Tanzania yetu hii au zilikuwa ni stori tu na kama alikuwepo kuna mtu aliwahi kumuona live na akashuhudia matukio yake.
 
Huyo jamaa alikuwepo kweli, mimi nilimshuhudia maranying, alikua nauwezo wakuvuta gari yoyote kwa meno, watu walikua wanaweza kutwanga mahind makavu yakiwa kwenye kinu juu ya kifua chake mpaka yaka koboka, aliweza kuzuia gali mbili na pikipiki mbili visiondoke kwa wakati mmoja, hakika alifanya mambo mengi makubwa sana yakushangaza, ilikua burudanikubwa kwa watazamaji wa malika yote.
 
Dah kweli mwana we wa juzi, alikuwepo bana, sisi wa miaka hiyo tumemuona actualy mambo ya upawa ndio ilikuwa fashion miaka hiyo
 
umenikumbusha mbali sana mkuu! huyu bwana alikuwa mkali sana mambo ya u-power...sijui kapotelea wapi!
 
yap Power Mabula kipindi hicho akija shuleni kiingilio shilingi hamsini..
unatetemeka kweli kabla hata hajaanza kuonyesha mazingaubwe yake...
That guy was genius .. I'm not too sure if he's still alive tho....
 
Wadau mmenikumbusha mbali kweli,.ni kweli huyu mtu alikuwepo na alifanya hii miujiza yake kama kuzuia gari na kutwanga kinu,Power huyu Mabula ambaye alikuwa mwanajeshi,alikuwa jirani yetu,maeneo ya Kijitonyama,mtaa wa bakery,au mtaa wa Mzee Juba,kwa wale wenyeji watakuwa wanaufahamu..
Mwaka jana 2011,June nilibahatika kumwona wilayani Kilindi,eneo la Songe,sasa hivi ni Mchungaji anatangaza injili na ana kanisa lake..
 
Back
Top Bottom