Gaijin
JF-Expert Member
- Aug 21, 2007
- 11,812
- 5,286
katika pita pita zangu kutafuta vitabu vinavyohusiana na harakati za kutafuta uhuru Tanzania nimekutana na kitabu hiki UKWELI NI HUU (KUUSUTA UONGO) kilichoandikwa na Amani Thani ambae alikuwa muasisi wa chama cha Zanzibar Nationalist Party. Kitabu hicho amekiandika 1994 akiwa ukimbizi Dubai
kwenye kitabu hicho ambacho kinahusiana zaidi na Zanzibar, magogeni wote wa siasa kuanzia kina Karume, Ali Muhsin, Babu na Nyerere wanatajwa. Sijakimaliza kukisoma lakini muandishi anasema haya ambayo yamenivutia hadi sasa
1) Babu alisomeshwa (short course) na ZNP lakini alikigeuka chama na akataka kishindwe katika uchaguzi.
2) Nyerere alihusika moja kwa moja na maamuzi yaliyokuwa yakifanywa na chama cha Afro Shiraz Party Kabla ya Uhuru (ambayo yalirudisha nyuma upatikanaji wa uhuru wa Zanzibar) na alikuwa miongoni mwa waliokianzisha chama hicho (behind the scenes).
3) Pia amezungumzia suala watu waliokimbia Zanzibar baada ya mapinduzi, kurudishwa kwa nguvu na Nyerere huku akijua kuwa wanaenda kuuwawa.
Kinazungumzia kuhusu mateso ya jela alizokaa muandishi na mambo mengine ....
Sasa najiuliza hivi...
1. hivi Nyerere alihusika kweli au Amezuliwa?
2. Kwa Asilimia ngapi yaliyoandikwa humo yana ukweli wowote?
Hebu nijuzeni kidogo manake wengine historia ya nchi yetu inatupiga chenga
Kitabu hicho kwa kiingereza bofya chini
The Nobility of Zanzibar