Biashara ya Kutoa Mikopo (Microfinance): Hatua, Taratibu za Kufuata na Ushauri wa Uendeshaji

Hapa pana hela ila tabu yake vikwazo ni vingi mimi nimejikuta napenda kufanya kwa kutoa training na wakopeshane wenyewe mimi wanilipe usimamizi tu na report hivyo nakuwa sichukui risk kubwa.
 
Hizi MFI zitafungwa zote muda si mrefu!! Utapeli na wizi wa mchana umezidi kwa walala hoi.Nakwambia with MFI Mtanzania hatakomboka hata kidogo,Kwani ni kunyonyana kwa kwenda mbele.My take anzisha bureua de Change kwani hizi life span yake ni kubwa.Lkn MFI ni biashara ya msimu tu kwa Tanzania.

Wazo zuri. Je, Bureau de change kunataratibu gani zinahitajika kuanzisha?
 
asante nitaku-pm mkuu, ila unakosea kusema mimi sina Tsh 50m mbona kwa wabonge wengi ni hela ya kawaida tu

No bank uwezi aanzisha kwa milion 50 tu la sivyo zingekuwa kama chungu kila mtu angekfungua, ni BILION 5 minimum deposit uweke BOT then ndo uwe na hela nyingine ya majengo, mishahara , wafanyakazi. n.k na mpka uje ufike point ambayo matumizi yatakuwa sawa na mapao itachukua si chini ya miaka mitano hii ni kutokana na utafiti wangu kwa maana nyingine utakuwa unaendesha bank kwa matumizi > mapato for not less than 5 yrs.

Kwa Mtanzania wa kawaida kuanzisha bank ni ngumu unless vigogo ndo maana karibu mabank inchi ni ya wazungu wanokuja na mitaji mikubwa sana.
 
Hapo umenigusa mkuu, Hebu nipe utaratibu wa kuanzisha Bureau de change kama unaufahamu.
Sharti la kwanza ambalo najua ni ngumu kwako na kwangu ni lazima uweke BOT Million 400 then ndo uanz iyo burea de change.
 
Unaweza kuanzisha SACCOS, au Financial NGO au kampuni financial institution kama FINCA kati ya zote hizo rahisi kuanzisha ni SACCOS ukitaka kuanzisha Benki lazima uwe na Sh. 50 million
sidhani kama unazo. Ukitaka ushauri zaidi nipigie 0755394701 au nipm

Hapo kwenye bold,sijakuelewa mkuu.
 
Jamani bado hatujapata jibu la kiasi kinachotakiwa kuweka bot, ili mtu uweze kuanzisha microfinance? Naitamani sana hii biashara wakuu!
 
''Microfinance yangu''. Kazi kweli kweli nenda BRELA kasajili kampuni inayotoa mikopo midogo midogo. Ila punguza ubinafsi nashauri jiunge na watu wengine maana kwa mtazamo wangu wewe sio practitioner wa microfinance kabisa.

Nashangaa mtu mmoja ataanzishaje SACCOS? Hii ni member based. Idadi ya chini ya wanachama ni 10 kwa work place SACCOS na nadhani 20 kwa SACCOS ya mtaani. Nitumie sms kama unataka maelezo zaidi ya kihalisia.
 
Kintinku, mimi nahitaji kufahamu zaidi kuhusu deposit ya kuanzisha microfinance bana! hayo mambo ya saccos nawaachia wenyewe.

Chonde chonde, mwenye kufahamu jamani atujulishe hapa!
 
jamani bado hatujapata jibu la kiasi kinachotakiwa kuweka bot, ili mtu uweze kuanzisha microfinance? naitamani sana hii biashara wakuu!

Hakuna hela ya kuweka BOT. Wewe jifanye ni NGO ya kuwawezesha maskini, period. Trust me.
 
kintinku, mimi nahitaji kufahamu zaidi kuhusu deposit ya kuanzisha microfinance bana! hayo mambo ya saccos nawaachia wenyewe.
chonde chonde, mwenye kufahamu jamani atujulishe hapa!

Niko kwenye hii field, naijua vizuri, nacho weza sema ni ujasiri tu, na inalipa kwa sana.
 
Wadau wenzangu hapa JF kina Babalao na wengineo naomba mnisaidie ili niweze kuanzisha Microfinance yangu Dsm ninatakiwa niwe na nini, na utaratibu gani nifuate.

Mkuu, kwa ufahamu wangu.

Microfinance haiwi Governed na BOT kwa sababu haichukui customer deposits, inakopesha tu.

Taratibu za kuanzisha:
- Register kampuni kwa njia ya kawaida kabisa (peleka Memarts BRELA, pata TIN number toka TRA..etc)..lawyer mzuri anakufanyia hivi vyote kwa cost isiyozidi 1m

- Pata leseni kutoka wizara ya viwanda na biashara (Sio BOT!!!)

Anza biashara.

As far as I know, hakuna minimum capital inayotakiwa, wala deposit huko BoT kwa sababu risk ni ya pesa zako mwenyewe na sio za kuchukua kwa wananchi. Hapo baadaye unaweza kuzishawishi benki zikakukopesha pia kama biashara nyingine.
 
Hakuna hela ya kuweka BOT...wewe jifanye ni NGO ya kuwawezesha maskini..period..trust me

Mkuu, maofisa wa TRA hawatanisumbua? na kusema tu ni ngo ya kuwawezesha maskini, hakutakua na vikwazo kwenye usajili?
 
Tunaweza kukusaidia. sisi ni kampuni inaitwa Right Business Consultancy na tuna deal na consulting and business support services kwa ajili ya Microfinance institutions and entrepreneurs so nadhani ungetu contact we would help you on that.

Our contacts: Right Business Consultancy
2nd floor, biashara complex, Mwananyamala, kinondoni
email: rightbusinessconsultancy@yahoo.com
 
Habari, ni vyema mkaweka dondoo za msingi mf, minimum unatakiwa uwe na kiasi gani? Au ni vitu gani vya msingi unatakitiwa kwanza kuwa navyo. Thanks
 
Back
Top Bottom