Matumizi ya mbegu za mbarika (mnyonyo) kiafya

Sizinga

Platinum Member
Oct 30, 2007
9,101
6,027
Mnyonyo ni mbegu zinazotokana na mti wa Mbarika. Sasa mwenye kujua zaidi atuhabarishe, manake hizi mbegu mi nasikia ni zaidi ya dawa!!

Kwa niliyoyasikia hasa toka kwa wazee wa zamani ni haya, naomba kujua ufafanuzi kwa mwenye kufahamu zaidi manake inaweza kusaidia wengi:

- Kwanza inatumika kama kinga dhidi ya pepo mbaya. (Majini na mashetani)
- Kipindi mtoto anapozaliwa, baada ya zile siku 40, nasikia anapakwa haya mafuta ya mnyonyo kichwani halafu ndo ananyolewa nywele(kwa baadhi ya makabila), nasikia ni kinga flani dhidi wa watoto.
- Inazuia kupata mimba kwa wadada. [Mbegu moja ukiinywa basi mwaka 1 hautashika mimba, ukinywa 2 basi yrs zitapita bila ujauzito]
- Ni dawa nzuri kwa magonjwa mbalimbali hasa ukichanganya na miti shamba mingine.
- Kikubwa nasikia inarespond 'Positively' ukiipa 'commands' na matokeo utayapata. Yaani ukiiambia kitu flani uakaweka na vitu flani basi utapata feedback kupitia hizo mbegu.

Mwenye kuzijua kiundani naomba ufafanuzi wa hilo plz. MziziMkavu, LIKUD
 
Last edited by a moderator:
Mnyonyo ni mbegu zinazotokana na mti wa Mbarika. Sasa mwenye kujua zaidi atuhabarishe, manake hizi mbegu mi nasikia ni zaidi ya dawa!!

Kwa niliyoyasikia hasa toka kwa wazee wa zamani ni haya, naomba kujua ufafanuzi kwa mwenye kufahamu zaidi manake inaweza kusaidia wengi:

-Kwanza inatumika kama kinga dhidi ya pepo mbaya.(Majini na mashetani)
-Kipindi mtoto anapozaliwa, baada ya zile siku 40, nasikia anapakwa haya mafuta ya mnyonyo kichwani halafu ndo ananyolewa nywele(kwa baadhi ya makabila), nasikia ni kinga flani dhidi wa watoto.
-Inazuia kupata mimba kwa wadada.[Mbegu moja ukiinywa basi mwaka 1 hautashika mimba, ukinywa 2 basi yrs zitapita bila ujauzito]
-Ni dawa nzuri kwa magonjwa mbalimbali hasa ukichanganya na miti shamba mingine.
-Kikubwa nasikia inarespond 'Positively' ukiipa 'commands' na matokeo utayapata. Yaani ukiiambia kitu flani uakaweka na vitu flani basi utapata feedback kupitia hizo mbegu.

Mwenye kuzijua kiundani naomba ufafanuzi wa hilo plz. MziziMkavu, LIKUD
Mbegu za mnyonyo huruhusiwi kula mbegu mbili unaweza kufa wakati wowote ukila mbegu za mnyonyo zaidi ya moja.

FAIDA MBALIMBALI ZA MTI WA MNYONYO

myonyo.jpg


Mti wa mnyonyo una faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Karibu kila kitu kinachopatikana kwenye mmea wa mnyonyo kina faida za kiafya kwa mwanadamu.

Majani ya nyonyo ni tiba ya kifua kikuu na mizizi yake ni dawa ya mafindofindo, kuungua, macho yanjano, uvimbe, koo, kisonono na kaswende.

Kikonyo chake ni dawa ya kwikwi.

JINSI YA KUTUMIA MMEA WA MNYONYO KUJITIBU MAGONJWA & MATATIZO MBALIMBALI YA KIAFYA.


i. Kwikwi :
Jaza maji kwenye kikonyo, mpe mgonjwa anywe kila baada ya dakika 3 mpaka kwikwi iishe.

ii. Kuungua :
Meza punje za mti wa nyonyo kwa maji kiasi cha glasi moja kwa siku kwa muda wa siku tano.

iii. Kutibu miguu inayo uma :
Tumia majani kwa kufungia miguu inayouma.

iv. Maumivu Ya Mgongo :
v. Majani yake ukiyapasha moto yafaa kukanda mgongo wenye maumivu.


vi. Kutibu Kaswende na Kisonono :
Ponda mizizi ya mti wa mnyonyo, kisha chemsha na tumia kunywa glasi moja mara mbili kwa siku kwa muda wa siku saba.


vii. Kuondoa Kondo La Nyuma :
Mizizi ya mti wa mnyonyo ikitafunwa na mama mjamzito yafaa kwa kutoa mfuko wa uzazi ( kondo la nyuma ) kwa urahisi na usalama zaidi.


Myonyo/Mbarika (Castor)

Mnyonyo (KiSwahili) Erand (KiHindi) Kastorka (KiRusi) ni mmea wa jamii ya Mbono Kaburi, kwa jina la kitaalamu Japtropha - nitauzungumzia siku zijazo.

Baadhi ya faida za mnyonyo na mazao yake.
Mbali na kuweza kutumia mnyonyo kama uzio hai, njia hii inaweza kutumika kwa wale wasio na eneo kubwa la shamba ndiposa wakapata faida zake kama ifuatavyo:


Majani ya mnyonyo yanaweza kutumika kama tiba ya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB), kukanda (massage) ili kuondoa maumivu na majani haya yakifungwa kwenye mguu unaouma huleta nafuu hasa kwa maumiviu yanayokuja baada ya kuteguka, pia hutumika kutibu uvimbe kwa wanyama.

Mizizi ya mnyonyo huweza kutumiwa kama dawa ya mafundo fundo, uvimbe, kuungua, macho ya manjano, kuumwa koo na magonjwa ya kuambukiza ya kisonono na kaswende. Ukijaza maji baridi kwenye kikonyo cha mnyonyo na kumpa mtu mwenye kwikwi kila baada ya dakika mbili au tatu hivi, mara nyingi huondoa usumbufu unaoletwa na kwikwi.

Mbegu/Punje/Tunda/Njugu

za mnyonyo zikimezwa na maji bilauri moja kila siku kwa muda wa siku tano huweza kutibu maumivu yaliyosababishwa na kuungua. Vile vile, mbegu hizi huweza kusagwa na kisha kuenguliwa mafuta kwa ajili ya kulainisha mashine na mitambo viwandani.


Mbegu za mnyonyo kabla ya kukomaa
Mafuta yatokanayo na mbegu za nyonyo mfano Ricinoleic Acid, Oleic Acid, Linoleic Acid nk hutumika kutibu ugonjwa wa wa jongo (rheumatism) unaowakumba watu wengi wanaoishi maeneo ya miinuko na baridi, pia hutibu ugonjwa wa mifupa ujulikanao kwa jina la kitaalamu kama arthritis na gauti.Mafuta ya mnyonyo pia yanaweza kutumika kama njia ya

kupanga uzazi
kwani yana kiasi fulani cha sumu ya protini ijulikanayo kitaalamu kama ricin ambayo ikitumiwa kwa kiasi kidogo huharibu utungo, huweza pia kutumiwa kama mafuta ya kupaka ama losheni katika sehemu za siri ili kuua mbegu za uzazi za kiume wakati wa tendo la kujamiiana. zazi wa mpango.

Tahadhari:

Mnyonyo ni mti wenye sumu inayoweza kuua binadamu au wanyama endapo itatumika kuzidi kipimo.
  • Mazao yoyote yatokanayo na mnyonyo huhatarisha au/na kuharibu mimba na hata kuweza kusababisha kifo cha mjamzito, hivyo, matumizi yake lazima yawe ya uangalifu mkubwa.
    Mafuta ya Ricinoleic acid yanayopatikana kutokana na mnyonyo vile vile yanaweza kutumika kurekebisha hedhi (mzunguko wa damu ya mwezi kwa wanawake) ikiwa mzunguko umechelewa ama kusimama katika umri usiotarajiwa. Huweza pia kupunguza maumivu makali yanayotokea wakati wa hedhi.

    Mafuta ya mnyonyo yanayojulikana kitaalamu kama Undecylenic Acid huweza kutumika kutibu magonjwa mbalimbali ya ngozi na vidonda vinavyosababishwa na bakteria ama ukungu (fungus).
Mbegu za mnyonyo baada ya kukomaa

mbegu za mnyonyo.jpg


Akina mama wanao nyonyesha
pia wanaweza kutumia mafuta baridi ya mnyonyo kiasi kidogo ili kuepuka madhara ya mafuta hayo kwa mtoto, kumbuka hapo awali nimeandika kuwa mafuta haya yakitumiwa kwa kiwango kikubwa ni sumu kuongeza wingi na mtiririko rahisi wa maziwa

Mnyonyo unaweza pia kuwafaa watu wanaoishi na VVU (Virusi Vya UKIMWI) kwani mafuta yake ni sumu ya kuua vimelea vya magonjwa kama vile bakteria na ukungu (fungus)




mnyonyo.jpeg




        • Kupakaza: Chukua kipande cha nguo ama kitambaa, kisha kiloweke kwenye mafuta ya mnyonyo ndipo ufunge katika kiwiko ama eneo lenye maumivu ama kidonda. Vinginevyo, chukua kiasi cha mafuta na kupaka eneo linalohusika mfano, penye kidonda, kuugua ama pakaza kichwani au juu ya tumbo wakati wa maumivu ya hedhi nk. Unaweza kuacha kwa muda wa saa moja kabla ya kunawa ili uipe ngozi muda wa kunyonya kiasi cha mafuta. Unaweza kujifunga kitambaa hicho tumboni ama mgongoni kama kibwebwe na kuendelea

mafuta ya mnyonyo.jpg


        • na shughuli za kawaida
          Kunywa: Chemsha mbegu chache za mnyonyo pamoja na maji na maziwa kisha unywe kiasi kidogo kadiri ya nusu hadi bilauri moja ya ujazo wa mili lita mia mbili na arobaini.Kusafisha utumbo: Kunywa mafuta ya mnyonyo vijiko viwili vikubwa vya chakula asubuhi, kisha pumzika kwa saa mbili ndipo unywe maji glasi mbili na endelea kunywa maji glasi moja kila baada ya saa moja.
 

Attachments

  • mbegu za mnyonyo.jpg
    mbegu za mnyonyo.jpg
    91.4 KB · Views: 1,120
asante sana kwa ufafanuzi mkuu MziziMkavu

kuna sehemu nimeona hayo matumizi ya mnyonyo juu ya kinga ya kupata mimba kama njia ya uzaz wa mpango,kwa maelezo inaonyesha kama itatumika tofauti na kiwango kinacohitajika ni sumu na huenda kifo.maelzo niliyoyasoma huko yalikuwa kama ifuatavyo unakula mbegu mbili siku ya kwnza ya period,mwezi unaofuata unameza mbegu moja siku ya kwanza ya period na utakuwa unameza kila mwezi hadi siku au mwaka utakaoamua kubeba mimba ndo utaacha kumeza

sasa mkuu umesma mtu akila mbili anaweza kufa...kwa hiyo ni hatari kwa watumiaji .naomba maelezo sahihi jinsi ya kuitumia hii ili isilete madhara
 
Last edited by a moderator:
asante sana kwa ufafanuzi mkuu MziziMkavu

kuna sehemu nimeona hayo matumizi ya mnyonyo juu ya kinga ya kupata mimba kama njia ya uzaz wa mpango,kwa maelezo inaonyesha kama itatumika tofauti na kiwango kinacohitajika ni sumu na huenda kifo.maelzo niliyoyasoma huko yalikuwa kama ifuatavyo unakula mbegu mbili siku ya kwnza ya period,mwezi unaofuata unameza mbegu moja siku ya kwanza ya period na utakuwa unameza kila mwezi hadi siku au mwaka utakaoamua kubeba mimba ndo utaacha kumeza

sasa mkuu umesma mtu akila mbili anaweza kufa...kwa hiyo ni hatari kwa watumiaji .naomba maelezo sahihi jinsi ya kuitumia hii ili isilete madhara
Kula mbegu 1 kwanini ule mbegu 2? Mkuu ICHANA
 
Last edited by a moderator:
Mmea huo kitaalamu unaitwa Riccinus communis na matumizi yake hasa hutumika kufungua tumbo kama mtu hapati choo yaani (constipation)!kwa madukani ulizia Castor oil
 
Mi najua mbegu moja kila baada ya kumaliza hedhi,ni kinga ya ujauzito ila sio watu wote zinawakubali, kuna watu wachache zimewakataa na wameshika mimba
 
Mi mnyonyo umenikataa. Nilikuwa nameza mbili kila baada ya kumaliza period. Nilitumia vzr kwa miez 7, ghafla nikajikuta nna mimba. Nimekata tamaa kabisa na uzazi wa mpango asilia. Mnyonyo ndo ilikuwa tumaini langu la mwisho. Nafikiria kufunga nikijifungua. Ingawa habari ni nyingi juu ya kufunga kwa umri mdogo. Nna miaka 31. Natarajia mtoto wa nne, thanks to njia za asili.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Ngoja nikajaribishe kutumia mnyonyo maana daah!!! Itanisaidia uzazi na afya kiujimla
 
Mi mnyonyo umenikataa. Nilikuwa nameza mbili kila baada ya kumaliza period. Nilitumia vzr kwa miez 7, ghafla nikajikuta nna mimba. Nimekata tamaa kabisa na uzazi wa mpango asilia. Mnyonyo ndo ilikuwa tumaini langu la mwisho. Nafikiria kufunga nikijifungua. Ingawa habari ni nyingi juu ya kufunga kwa umri mdogo. Nna miaka 31. Natarajia mtoto wa nne, thanks to njia za asili.
Unapatikana wapi huo mnyonyo naomba nisaidie jinsi ya kuupata
 
Mkuu mimi nimewahi kutafuna mbegu 4 za mnyonyo, madhara niliyopata ni kuharisha kama siku moja hivi. Je kuna madhara mengine ya muda mrefu?
Mbegu za mnyonyo ukila zaidi ya mbegu 1 unaweza kufariki dunia wewe una bahati kuharisha lakini sio nzuri kula mbegu za mnyonyo zaidi ya moja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom