Mh. Zitto kuna ukweli gani katika ripoti hii?

Kaka sahau hizo ndoto za mtu kama zito rais, mie ntahama nchi hii kama mtu kama zito ataweza kuwa rais.
Kama Kikwete amekuwa raisi na mmemchagua kwa kura za kishindo ,kwa nini Zitto asiwe raisi?
 
Mkuu mimi sina tatizo la hao jamaa kusaidia wananchi (after all we need more of the same...)

Lakini haya mambo ya kwamba Barrick hailipi kodi zinazopaswa kwa kisingizio kwamba haijapata faida... (kumbuka madini wameshayachimba na by the time wanapata faida watakuwa wameshamaliza madini na kuondoka nchini) Pia hili suala la kuidai serikali mapesa in terms of vat returns....!!!

Umesema kwamba umekuwa mkali (and since umesimamia sheria mpya kuandikwa..) basi mkuu haukuwa mkali enough sababu ungekuwa mkali sana hata ungelazimisha hizi sheria zifanye kazi retrospectively.....

Mkuu najua hii sio kazi yako peke yako lakini tuwe wachungu na mali ambazo wajukuu wametukopesha..., kumbuka na wewe ni kama mlinzi uliyepewa silaha kulinda hizi mali..., anything goes wrong we will all be the ones to blame..., am sure tungekusanya kodi ipasavyo tungeweze kujenga hata University hapo Kigoma....!!
Nimekubaliana na wewe kabisa na suala la kodi limekuwa msimamo wangu kwa muda mrefu. Mchango wangu kwenye Bajeti kuu na ile ya nishati na madini nilisema hili wazi kabisa.

The reference to 'ring-fencing' referred to the paper is the theory I explained to the researcher and it paid off as tulawaka declared profit last year.

I have acted very transparently in this matter, at arms-lenght. Nani kasema corporate social responsibility watu wa kigoma hawana haki nayo?

I have never benefitted personally to any gift given by Barrick or any other mining company in Tanzania.

I am happy msaada walioutoa umewezesha kijiji cha Mkabogo kukamilisha majengo ya shule na hivyo kuwafanya watoto wa kijiji kile na kata ya Kalinzi kupata elimu ya Sekondari.

Wanaotaka kulifanya hili jambo la kisiasa sitawazuia hata kidogo. Lakini naomba lionekane kwa picha pana zaidi. Hata hivyo kama ikithibitika nimefaidika kwa namna yeyote mimi binafsi, nitawajibika
 
Safi sana Zitto kwa kutoa ufafanuzi kwa muda muafaka, lakini kuna swali umeulizwa
kama habari haina ukweli, je upo tayari kumpeleka mwandishi mahakamani kwa kukuchafulia jina?
 
Ninaamini makampuni yana jukumu la kusaidia jamii. Kwamba Barrick walisaidia ujenzi wa shule ya Sekondari Jimboni kwangu, Jimbo ambalo lipo nyuma sana kimaendeleo ni jambo la kushukuru na sioni tatizo lolote la kimaadili.
ZZK utahukumiwa bure kwa watu wasiofahamu nini jukumu la wawekezaji kwa jamii inayowazunguka. Ndo maana mogogoro na wananchi haiishi Geita, Nyamongo Mvomero nk. Pole sana this is Tanzania. Instead of praised and b among tanzanian heroes utakuwa ADUI WA WA TZ.
 
Mm nazani kunamambo mengi yamejifisha na hatuyajui ukweli wake. Hapa sio kusema Zitto kajibu au kajieleza sijui nn, hapa hishu ni kweli kuna uzalendo ambao viongozi hawa wapo teyari kulala njaa na raia au wanaleta longolongo tu hili wapate majina?

Mm nazani bado tz kupata mzalendo kiongozi wa kweli kama hayati Baba wa taifa au Sokoine. Tuache utani na kuwa wafuasi wa vyama bila kujari maslai ya taifa letu. Hapa unakuta huyo huyo anamiliki magari ya kifahari hata kama ni pesa zake bado siomwaminifu kwa taifa.

Huwezi sema watu waache kuchukua posho wakati ww unapata pesa sehemu nyingine, Je wakati unaingia bungeni kipindi cha kwanza ukuona hizo posho sio halali kwenu?

Mm ninamtazamo tofauti sana na nitapigania msimamo wangu hadi kufa kwangu. Ushauri kwa wavijana watz wenzangu TUACHANE NAKUFAGILIA VYAMA BALI TUNATAKIWA KUMWANGALIA MTU MWENYEWE USONI KWAMBA HUYU JAMAA TUKIMPA UONGOZI ATATUPELEKA WAPI?

Nawasilisha.
 
Nadhani maelezo yako yanatoa mwanga kwa kiasi fulani lakini pia yanaweza kupwaya katika maeneo fulani fulani.

Kama nimeelewa hii article vizuri ni kwamba 'author' anauliza Zitto wa 'pre-mabati toka Barrick ndiyo huyo huyo wa after-mabati? Na chimbuko la swali lake (kama nimeelewa vizuri) anaangalia 'ukali' wako kwa hawa Barrick kabla hakujawa na huu msaada kwa shule ya jimboni kwako na sasa.

Na katika kujenga hoja yake nadhahi mwandishi atakuwa amejiuliza je, unaridhika na mchango wa Barrick kwa sasa? Kama hauridhiki kwa nini hauko 'vocal' kama ulivyokuwa huko nyuma? Na katika kupekuwa ndio 'author' akaja na hii theory ya msaada toka Barrick na 'supposedly' upole wako siku hizi. Nadhani hii ndio hoja ya kujadili.

Ukali? Ukali wa namna gani sasa? Nilikuwa mkali kwenye mkataba wa Buzwagi. Hapajasainiwa mkataba mwingine wa madini toka Buzwagi. Kuna sheria mpya ya madini. Tulawaka wameanza kulipa kodi, resolute wameanza kulipa kodi.

Bungeni, hili Bunge la juzi tu nimetaka kuwe na windfall tax kwenye madini (hotuba yangu ipo zittokabwe.com).
Bungeni katika hotuba ya Wizara ya Nishati na Madini nimemtaka Ngeleja atoe notice kwa mining companies kuhusu new royalty rates waanze kulipa.

Hotuba yangu ipo katika blog yangu zittokabwe.com! Ukali upi unaousema sasa?
Lakini jambo la muhimu sana kujua katika siasa, a politician grows. I do. I must graduate from being a divisive figure to a uniting figure.

I must understand the sector and engage them. I have been doing that. Siwezi kuwa mpayukaji tu.
 
Zitto
Sasa kulikuwa na ulazima gani wa kupeleka msaada kwenye jimbo lako ambalo liko km 600 kutoka mgodini ilihali kuna majimbo mengi tu Shinyanga hayana sekondari. Na mbona baada ya msaada huo umekuwa kimya sana juu ya sekta ya madini tofauti na kipindi cha nyuma. Je hilo halikuwa jaribio la kukunyamazisha.

Naomba majibu sahihi, halafu mkuu mbona hujibu maswali yangu?
 
Last edited by a moderator:
Ili mradi watoto/vijana wetu wanasoma sekondari sina mgogoro. Je kuna bakshishi yoyote walikupa hawa jamm. Please declare interest if any. Maana ni mbunge pekee uliyekataa posho ya vikao(sitting allownce). Please clarify.
 
Hili ndio tatizo wabunge wanapotaka kuwa watendaji. Lazima wajikute wameingia kwenye mitego ya kupewa chambo

 
Ili mradi watoto/vijana wetu wanasoma sekondari sina mgogoro. Je kuna bakshishi yoyote walikupa hawa jamm. Please declare interest if any. Maana ni mbunge pekee uliyekataa posho ya vikao(sitting allownce). Please clarify.

Sijawahi kupokea zawadi ya aina yeyote kwa kampuni yeyote ya madini. Hata suala hili la CSR mimi ndio nilireveal kwa mtafiti huyu kuonyesha mifano ya miradi wanayotoa na kukosoa mtindo huu badala ya kulipa kodi stahili.

Nimekuwa wazi kabisa katika jambo hili. Sikushika hata senti ya fedha hizi. Nilikagua mradi huu na watoto wanasoma. Suala la kodi katika sekta ya madini ( ambalo nimeliandikia katika dissertation yangu ya Masters of Law and Business Bucerius Law School, Hamburg) ni suala ambalo nimeendelea kulisemea kila wakati.

Hoja zangu Bungeni zinapatikana katika blogu yangu Zitto na Demokrasia
 
Zitto una bahati umekuja mapema kujibu hoja, la watu wangeshatoa hukumu usiku huu
Tuna tatizo watanzania, tuhuma zinaaminika sana na kwa haraka kuliko ukweli.
Nahisi tumewatuhumu na kuwahukumu watu wengi sana bila kuwa na ushahidi wa kutosha.
 
Ukali upi unaousema sasa?
Lakini jambo la muhimu sana kujua katika siasa, a politician grows. I do. I must graduate from being a divisive figure to a uniting figure. I must understand the sector and engage them. I have been doing that. Siwezi kuwa mpayukaji tu.

On the red, I get you Zitto, hata mimi siku hizi nimepunguza sana ku-argue, it just came, naturally. Uzee dawa. he he he heeee...
 
Sasa kulikuwa na ulazima gani wa kupeleka msaada kwenye jimbo lako ambalo liko km 600 kutoka mgodini ilihali kuna majimbo mengi tu Shinyanga hayana sekondari. Na mbona baada ya msaada huo umekuwa kimya sana juu ya sekta ya madini tofauti na kipindi cha nyuma. Je hilo halikuwa jaribio la kukunyamazisha.

Naomba majibu sahihi, halafu mkuu mbona hujibu maswali yangu?

We mbona mtu wa ajabu sana, kama wabunge wa shinyanga wamelala kuomba msaada, unataka Zitto awaombee.......?
 
Kaka sahau hizo ndoto za mtu kama zito rais, mie ntahama nchi hii kama mtu kama zito ataweza kuwa rais.


Mamanalia yawezekana utahama inchi akija mtu kama Zitto... But fortunately hutakua na haja ya kuhama for Zitto ni Zitto na there is no other; Hivo akija atakuja yeye mwenyewe na sio kama yeye... for bora yeye kuliko hata Slaa... Apart from hao una mtu ambae wewe unaona atafaa?? Naomba tu usije toa ahadi ya Kujitoa kafara kama Zombe - Be careful what you wish for...
 
Lakini jambo la muhimu sana kujua katika siasa, a politician grows. I do. I must graduate from being a divisive figure to a uniting figure. I must understand the sector and engage them. I have been doing that. Siwezi kuwa mpayukaji tu.

Mkuu I think the old Zitto is more effective... (hii nchi tulipofikia hatuwezi kwenda ki-diplomasia pekee..) bila kupiga kelele na kila mtu akasikia mambo hayaendi.., kwahiyo sioni tatizo la ku-fight on both fronts..., through media and anything at your disposal... Hivi vita haviwezi kushindwa kwa njia moja pekee..

Wengi we dont know that we dont know.... (hatujui kama tunaibiwa...) kwahiyo mnaojua inabidi mtuambia na mpige kelele na sio kwenye Blog pekee (sababu watanzania wengi hawana access na hii anasa ya internet).., kwahiyo mkuu please dont loose your character in the name of growing up...
 
Maeneo yanayozunguka mgodi ni lazima yanufaike na migodi hiyo.How comes Geita to North Kigoma Hon Zitto?Kwa kuzingatia historia yako na Barrick haukuona kuwa hata kama ni kweli msaada wa kawaida utachukuliwa ni some sort of kukunyamazisha?
 
Back
Top Bottom