Mbilinyi: CCM na Serikali yake ni vurugu
Na Sarah Mossi
WAZIRI wa zamani wa fedha anayeendelea kushika nyadhifa mbalimbali kitaifa kwa sasa, Profesa Simon Mbilinyi, amesema kuna tatizo serikalini na katika chama tawala.
Akizungumza na Rai katika mahojiano maalumu wiki iliyopita nyumbani kwake Upanga, jijini Dar es Salaam, Profesa Mbilinyi alisema inavyoelekea kuna CCM (Chama Cha Mapinduzi) mbili; ile ya zamani na ya sasa ya wanamtandao ambayo itaharibu nchi.
Wamejitahidi (Serikali ya Rais Jakaya Kikwete) kufanya waliyoahidi katika kampeni, ila bado kuna problem ya Chama Cha Mapinduzi na Serikali, hawako pamoja na personality zimeanza kutawala. Siasa hizi zitatupeleka pabaya.
Serikali ifikirie hili kwa kina zaidi na iwe na watu strong (wenye nguvu), isiwe na ideas (mawazo) za zamani za huyu ni mwenzetu, tuseme huyu anaweza. Tukisema huyu ni mwenzetu tutaumia. Hata muundo wa Serikali ni mkubwa kuliko kazi zilizopo, tuna watu wengi wa kufanya kazi lakini kazi hazipo. Central Government (Serikali Kuu) zina matrilioni ya bajeti lakini hazina kazi, kazi zote ziko kwenye district (wilaya).
Kwenye siasakwa uzoefu wangu CCM ina two shadows (vivuli viwili). Kuna chama in tradition (jadi) na chama mtandao. Hizi mbili ziwe pamoja kama ilivyokuwa zamani na chama kifanyiwe ukarabati kifanye kazi kama kilivyokuwa zamani. Sisi wazee tunaona chama hakipo sawa, alisema Profesa Mbilinyi kwa masikitiko.
Alisema changamoto kubwa iliyonayo Serikali sasa ni suala la ukosefu wa ajira, akaonya kwamba yalikuwa makosa makubwa kubinafsisha na kuuza mashirika mengi ya umma, badala ya kukodisha.
Changamoto kubwa ambayo ni ya hatari ni unemployment (ukosefu wa ajira), vijana wengi utawaona ni smart (werevu) lakini hawana ajira. Ajira yenyewe iambatane na structure (mfumo) ya uchumi. Tumefanya makosa makubwa ya kubinafsisha kila sekta lakini bado hazikufanya vizuri. Badala ya kutaifisha tungeajiri wakubwa wenye nafasi waje watuendeshee viwanda vyetu. Tungealika watu waje watusaidie kujiendesha. Kwenye mambo ya simu na posta leo hii tungekuwa na Tigo yetu, Zantel na Vodacom za kwetu. Hawa sasa wana fedha nyingi wanaweka matangazo yao katika kila sekta, hata kwenye michezo wanajitangaza. Tunachotakiwa hivi sasa kuwa na approach (mwelekeo) mpya si ile ya miaka ya 1970. Kilimo kiambatane na viwanda vyake. Tumeuza NBC (Benki ya Taifa ya Biashara) sasa tunaumia, na tuliharibu whole industry (viwanda vyote) tukaviuza badala ya kuleta watu kutusaidia kujiendesha. Tunahitaji viwanda ku absorb young population (kukidhi vijana), alisema. Kuhusu kero za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na mivutano ya CCM na Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Mbilinyi alisema Zanzibar wangeachwa wenyewe bila kuunganishwa na Tanganyika, wangeuana. Kwamba angekuwa yeye enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere angekifanya Kisiwa cha Pemba kuwa ni moja ya wilaya katika Mkoa wa Tanga na Unguja kuufanya kuwa mkoa mmojawapo wa Tanzania.
Alisema kwamba kuifanya Zanzibar kuwa mkoa ni suluhu ya kuwaepusha wasiuane kama ilivyokuwa katika miaka ya 1950, wananchi walipouana kwa sababu za kisiasa.
Alionya kuwa migogoro ya kisiasa iliyopo Zanzibar inatokana na kauli potofu za wanasiasa wa visiwa hivyo, ikiwamo kauli inayodaiwa kuwa Zanzibar inanyonywa na Tanzania Bara. Ameshauri kuwapo mjadala mkubwa wa kisiasa Visiwani wa kumaliza mitafaruku, ikiwa ni pamoja na kuwaachia Wazanzibari waamue wanataka nini.
"Tumejitolea (Tanganyika) sana bila kupata kinachotakiwa, lakini sasa wanasema (Wazanzibari) tunawanyonya," alisema Profesa Mbilinyi.
Kuhusu baadhi ya watu na taasisi kutaka Tanzania ijiunge na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC), Profesa Mbilinyi alionya kuwa hayo ni mawazo finyu.
Alisema madai kuwa nchi itafaidika kiuchumi ni kubweteka na ni uvivu, hivyo wananchi wanatakiwa wajengewe mazingira ya kufanya kazi na kuzalisha si kukimbilia kwenye mashirika kuombaomba.
"Chama kinaweza kusaidia katika hili hasa wale wa zamani, lakini hawa wapya si rahisi na kwa sisi wengine hatuna dini, dini zote ni zetu. Ndio, wote wanaoingia huko ni kwa sababu za kiuchumi lakini sisi tufanye kazi, sisi hatuna dini," alishauri Profesa Mbilinyi na kuonya kwamba kuiingiza kwa nguvu Tanzania katika umoja huo hakutasaidia na si vyema kuifanya dini moja kuwa juu ya dini nyingine.
Mjadala wa Tanzania kujiunga na OIC umeibuka tena baada ya miaka mingi kupita pale Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), kutaka kujiunga na jumuiya hiyo katika miaka ya 1980 na kupingwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikidaiwa kukiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
Hoja ya Zanzibar kujiunga na OIC ilikuwa ikitaka kupata ahueni ya kiuchumi kwa maana ya kupata misaada ya kifedha inayotolewa kwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo kwa shughuli mbalimbali za maendeleo.
Wakati huo aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Tanzania, hayati Ahmed Hassan Diria alidaiwa kufanya mipango ya kuiingiza Zanzibar kwa siri katika jumuiya hiyo na kuzua mtafaruku.
Hoja kubwa iliyopigiwa kelele na wananchi ni msimamo wa nchi kwamba Serikali ya Tanzania haina dini isipokuwa watu wake ndio waumini wa dini wanazozipenda. Lakini kikubwa zaidi kilichoafikiwa baadaye ni kwamba iwapo nchi ingetaka kujiunga na jumuiya hiyo, basi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo ina jukumu la kuomba uanachama huo wala si Zanzibar, maana Zanzibar si dola.
Hoja hiyo imeibuka tena hivi karibuni, wakati huu ikianzia kwa upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania karibuni, ambapo viongozi mbalimbali, akiwamo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Naibu Waziri, Seif Idd kusema walikuwa kwenye mchakato wa kujiunga.
Hata hivyo, wabunge waligawanyika, huku waumini wa dini ya Kikristo wakijitokeza waziwazi na kupinga uamuzi huo wa Serikali. Zanzibar nayo imesisitiza kuwa uamuzi wake wa kujiunga na jumuiya hiyo bado upo pale pale iwapo Tanzania itasuasua.
© New Habari
Kama Rangi zitawaumiza tuelezane ili nizitoe au Invisible afanye hivyo.
- Asema zipo CCM mbili, serikalini uwenzetu upo
- Afikiria Unguja ingekuwa mkoa na Pemba wilaya
- Aonya kujiunga OIC ni mawazo finyu na uvivu