Jana nilikuwa kunduchi salasala kwenye kumbukumbu ya mwaka mmoja tokea kifo cha profesa Jwani Mwaikusa aliyeuawa kwa kupigwa risasi katika mazingira ya kutatanisha nyumbani kwake kama mnakumbuka wadau.
Katika maongezi ya hapa na pale nikapata kuambiwa kuna watuhumiwa walikamatwa wamewekwa ndani, na kesi inaendelea.
Cha kushangaza tokea wakamatwe na kesi kuanza sasa ni mwaka mmoja, hiyo kesi hata mahakama kuu haijafika, bado ipo Kisutu kwa hivyo inatajwa na kuahirishwa tu hata kusikilizwa bado haijaanza kwani kesi za mauaji husikilizwa mahakama kuu.
Hii ina maana upelelezi bado haujakamilika sijui, hivi katika mazingira haya kuna haki kweli au maigizo?
Na sababu ya mauaji yale mpaka leo ni giza nene kwa mujibu wa wanafamilia.
Wadau hebu tuchangie mawazo kwenye hili.