Mama Rwakatare aichongea JamiiForums

Mimi sina uhakika sana na ukweli wa habari hii kwa sababu mletaji hakutaja source ili tupime credibility yake lakini kama ni kweli serikali ina mpango huo hautafanikiwa kwa sababu zifuatazo:

-1. Itakuwa inapambana na matokeo ya maendeleo ya technolojia na utandawazi kitu ambacho watu walioelimika kama waisrael, walio matajiri kama wachina na wamarekani wameshindwa kupingana navyo wakaamua kukubali yaishe.

2. Watumiaji wa mtandao huu siyo watu wajinga wajinga kama serikali inavyofikiri hivyo hata mtandao huu ukifungwa ni raisi sana wao kuwasiliana kwa njia nyingine ambayo hata mkono wa serikali houwezi hata kuufikia.

3. Kuhusu hoja ya mmiliki wa mtandao huu mimi kama mwanachama kipenzi sijawahi hata siku moja kuwaza wala kutamani kujua mwanzilishi wala mmiliki ila kwa sasa nafahamu kwamba wamiliki ni sisi wanachama na kwamba hata serikali.

Bunge au CCM wakianzisha mtandao unaokata contrutive issues kama huu mimi nitajiunga haraka na nipo tayari kuchangia ada za uendeshaji kila mwezi achilia mbali hii Jf ambayo maskini wa mungu sijawahi kuombwa mchango hata mbuni tangu nijiunge humu kulaaaaaleki !!!!!!.

Mtu msomi hatishiwi nyau bana!!!!
 
hongera zake mama lwakatare umepata na wewe nafasi ya kuzungumziwa jf....lakin jf ni level nyingine kabisa kama akina lowasa wamechemka utakuwa wewe
 
Kama huo ndo upeo wake alionao ninapata wasiwasi kama ndo kiongozi hata hao wanaomwongoza waanze kujipanga upya kutafuta mwelekeo mpya
 
Wana JF kutokana na mtandao huu wa kijamii kuibua na kueneza siri za Serikali Wabunge wa CCM wameridhia Mtandao huo ufungwe kama ilivyokuwa Ze Utamu na Mtoa Hoja ni Mchungaji Getrude Lwakatale,Leo pia kapeleka swali lake Bungeni,pia imeonekana mtandao huu ni wa CHADEMA..
Nawasilisha.....

Mh!, Mchungaji, Dr. Mama Lwakatare, (Mb)
 
Sijawahi kumsikia huyu Mchungaji akikemea ufisadi, leo hii anataka kunyamazisha watu kwa faida ya nini? Anamwakilisha nani huyu mama? Mchungaji gani anayanyamiza watu wasikemee maovu?
Kazi kubwa ya wachungaji wote ni kukusanya sadaka!!
 
kwa nini haitakiwi na Magambaz? Tutumie busara kutafakari ili tupate jibu inawezekana na sisi wana JF tuna matatizo. Lakini kweli sometimes baadhi yetu wanakwenda nje ya maudhui ya JF. Sasa kama utaanza kusema fulani mjinga, Kilaza, kubeza kitu kitu na mambo kama hayo hayo, kweli tunakuwa hatuko tena kwenye lengo la kukosoa, kuboresha, kushirikisha ili mwisho wa siku maendeleo kwa watanzania.
Kumwambia mtu kuwa ni kilaza ni sehemu ya kukosoa..........critique.
 
mtu atapimwa kwa umakini wa hoja zake.kuifunga jamii forum ni kukiuka katiba ya Tanzania inayotoa uhuru wa kutoa mawazo
 
jamani hyu mama sio king'asti kweli?. kuifungia hawawezi sanasana nashukuru atakua ameitangaza vya kutosha ndani na nje ya Tanzania. imeundwa tume ikiongozwa na mkama lakini wameshindwa kuifungia seuse huyu labda aifungie kwa maombi.
 
Hivi huyo Dr. MCh. Mh. Getrude Rwakatare huo U-Dr wake ni wa nini? MD au PhD? Ninapata wasiwasi na thinking capacity yake. Hivi kweli dunia ya leo kweli unaweza kuifungia mitandao ya kijamii?

Kuna Mbunge mwingine wa viti maalum wa CCM, Munze Tambwe aliwahi kulishauri bunge kwamba wapuuzie habari zote zinazotolewa WikiLeaks na JF kwasabu ni za uongo na uchochezi. Badala ya kuomba JF lifungiwe kwanini basi Mch. Rwakatale asiipuuzie JF? anakuja kufanya nini huku JF?

Halafu eti huyu ndiye Mchungaji wa Kondoo wa bwana, mnaosali huko kweli mna matatizo vichwani mwenu.

Ndiyo maana katika wale isinashari (kumi na wawili) hakuwemo hata Mwanamke mmoja, I believe Yesu alikuwa ana maana yake na wala sio kwamba hakuwaona wanawake kipindi hicho.
 
Back
Top Bottom