Ufisadi ATCL: Mkurugenzi wa Fedha, Steven Kasubi asimamishwa kazi

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,976
SERIKANI imebaini wizi wa takribani shilingi Milioni 715 katika Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kupitia kampuni ya Wakala wa ukatishaji tiketi ya Salama World Travel iliyopo visiwa vya Komoro.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ,Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa ameeleza kuwa wizi huo umefanywa kwa kushirikiana na wafanyakazi wa shirika hilo.

“Kufuatia upotevu huo Serikali imechukua hatua thabiti ikiwemo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa ATCL Bw.Steven Kasubi ili kupisha uchunguzi utakaofanywa na kikosi cha polisi kitengo cha usalama mtandaoni ili kubaini mtandao mzima uliohusika ” alisema Prof.Mbarawa.

Aidha aliongeza kuwa kwa utaratibu wa kawaida wa shirika hilo wakala anapewa ruhusa ya kuuza tiketi za ndege kuanzia kiasi cha shilingi milioni 15 tu na pale anapomaliza mauzo anarudisha fedha kwa shirika na baadaye kupewa ruhusa tena.

Prof.Mbarawa anasema kwa sasa wameanza na shirika la Ndege la Tanzania kwa kwa lengo la kulifufua kwa kununua ndege mpya na kuwa na wafanyakazi wachapakazi na waadilifu.

“Siku mbili zilizopita nilifanikiwa kukutana na menejimenti ya ATCL na kubaini mapungufu mengi na hivyo kuamua kuyafanyia kazi kwa kuhakikisha shirika hii linarudi kutenda kazi kwa udhabiti kwa kuwashughuikia wale wote wanaoenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma” alisema Prof.Mbarawa.

Vilevile aliongeza kuwa Serikali imemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) kufanya uchunguzi kwa mawakala wengine wote wa Shirika hilo kubaini kama fedha za uuzaji wa tiketi hizo zinarudishwa kama inavyotakiwa.
 
Kama hukuweza kutajirika kwa njia ya mkato wakati wa utawala wa Awamu ya Nne, basi bahati yako haiwezi kurudi tena katika utawala wa Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli!

Inafahamika rasmi Visiwa vya Komoro ni pango la waficha pesa duniani. Hata hii kampuni inayojiita Salama World Travel ukichunguza kwa makini kuna uwezekano mkubwa itakuwa inajihusisha na Money laundering.
 
Waziri wa ujenzi,uchukuzi na mawasiliano Mh.Prof Makame Mbarawa amemsimamisha kazi meneja wa fedha wa shirika la mdege la taifa ATCL Bw.Steven Kasubi kwa kuhusika na upotevu wa fedha zaidi ya million 700,
Source Clouds FM.
 
Hayo majipu uchungu ndio yalisababisha tushindwr kwenye Airline competitive Grid ukanda wa Afrika Mashariki na kusini pumbafyuuu
 
HIZI FEDHA ZINAZOSABABISHA WATU WASIMAMISHWE NI ZA MAMA NTILIE WANAOLIPISHWA KODI, WAFANYAKAZI AMBAO MISHARA YAO HAIKUTANI, WAJASILIAMALI NA WATAFUTAJI WANAOJITESA MITAANI ILI ANGALAU TAIFA LIPATE CHOCHOTE CHA KUJIENDESHA.

KWA NINI INAKUWA NI RAHISI KUSIMAMISHA WATU KAMA HAWA WABINAFSI NA KATILI KULIKO KUWAFANYA WARUDISHE PESA ZETU TENA NA RIBA WAKATI KIFUNGO KINAMGONJEA?. HII NI KUHAMASISHA WIZI.
 


Mkuu tangu tuingie ubia na wale boers basi tumeyumba sana angalau sasa tutaingia barabarani kushindana hata na Ethiopia airline, Kenya nayo tiamaji tia maji
ngoja tununue Airbus 320 wataisoma namba majirani
Mkuu Tusubiri Budget mpya tuone mambo yatakuaje
Haya mambo ya OC kwakweli yapungue sasa pesa ziende kwenye miradi hatuwezi kufika namna hii.
 
Hivi, atcl wana ndege ngapi na hufanya safari zake wapi? Nikijibiwa hilo jibu na hili; Kama shirika halikuwa na ndege wakala walikuwa na kazi gani? Huu no aina nyingine ya wizi. Serikali isiishie tu kusimamisha Bali ishitaki na kufilisi Mali zote walizo Nazo wote watakaokutwa na hatia tupate nusu hasara. Vinginevyo naiona Sanaa katika utendaji wa serikali.
 
Serikali imebaini wizi wa takribani shilingi Milioni 700 katika Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)
Kupitia kampuni ya Wakala wa ukatishaji tiketi ya Salama World Travel iliyopo visiwa vya Komoro.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi,Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa ameeleza kuwa wizi huo umefanywa kwa kushirikiana na wafanyakazi wa shirika hilo.
#TujipuUchungu #MajipuBadoSana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom