Kwanini maeneo haya yalipewa majina ya hivi?

Keko Magurumbasi
Magomeni
Afrika sana
Sinza Mori
Sinza kwa Remmy
Sinza Palestina
Mwenge
Mbezi Louis
Africana
Kijitonyama
Ubungo Kibangu
Ubungo Maziwa
Manzese
Tandale
Temeke
Kunduchi
Kimanzichana
Mbagala
Salasala
Kibamba
Kibamba Magarisaba
Kibaha
Buguruni
Kinondoni
Madale
Bunju
Boko
Tegeta
Goig
Makonde
Jogoo
Mabibo
Masaki
Oysterbay
Gongo la mboto
Ukonga
Kipawa
Chanika
Kigamboni
Mwanakwerekwe
Mkunazini
Mbagala Charambe
Shekilango
Sinza Mugabe
Sinza Mapambano

Chang’ombe
Ilala
Ilala Boma
Kurasini
Makumbusho
Victoria
Mikocheni
………..na maeneo mengineyo wenye kujua maana yake waweke hapa tuelimike na kujua maana ya sehemu tunazoishi
Kunduchi-kuna kichaa mmoja alikuwa anatembea uchi maeneo yale,so ndio wakabatiza jina hilo!!
 
Bagamoyo - watumwa kutoka bara walikuwa wakifika hapo wanajua hakuna kurudi tena bara so wanabwaga mioyo yao, pakaitwa bwagamoyo by then ila wakaedit baadae ikawa bagamoyo hadi leo!!!!
Koboroloni - ukisimama pale unaona kilele cha mlima kilimanjaro vizuri sana, kuna wadhungu walifika pale wakaona vilele vilivyoachana wakasema kibo alone, wachagga wakashindwa kidhungu ndo wakapaita hivyo hadi leo!!!!!
Ndafu - wadhungu walikuja kwetu kule wakachomewa mbuzi mzimamzima as usual, walipokula wakafurahi wakasema wanderfull, hicho kidhungu nacho kikawashinda wachagga wakaiita NDAFU hadi leo!!!!
 
Bagamoyo - watumwa kutoka bara walikuwa wakifika hapo wanajua hakuna kurudi tena bara so wanabwaga mioyo yao, pakaitwa bwagamoyo by then ila wakaedit baadae ikawa bagamoyo hadi leo!!!!
Koboroloni - ukisimama pale unaona kilele cha mlima kilimanjaro vizuri sana, kuna wadhungu walifika pale wakaona vilele vilivyoachana wakasema kibo alone, wachagga wakashindwa kidhungu ndo wakapaita hivyo hadi leo!!!!!
Ndafu - wadhungu walikuja kwetu kule wakachomewa mbuzi mzimamzima as usual, walipokula wakafurahi wakasema wanderfull, hicho kidhungu nacho kikawashinda wachagga wakaiita NDAFU hadi leo!!!!
Afadhali umeongelea nyumbani maana kidogo nidhani JF yote inaishi Dar!!!!
Chekereni-wazungu walikuwa wanatembea na wachaga flani along the train rails. Mara kwa mbali mzungu akaona treni inakuja kwa kasi akawaambia "Check train!"..mbongo kizungu kilimpita akaanza kusema "chekereni"..and so it is 2date!
 
Kwa wale wa mikoani tunaomba na tafsiri za mitaa hii
Mfaranyaki-Songea
Mwanjelwa-Mbeya
Mazimbu-Morogoro

Mwanjelwa ni jina na Mzee maarufu wa Kinyakyusa aliyeitwa Mwanjelwa, alikuwa akiishi eneo ambalo sasa linajulikana kama Stereo. Sasa kwa kuwa ndie aliyekuwa maarufu eneo hilo, ikabidi watu wabatize eneo hilo "Kwa Mwajnelwa". Kuna eneo pia linaitwa Mama John, hapo hapo Mbeya, huyu mama John nasikia alikuwa mke wa mzee Mwanjelwa (sina uhakika sana)!
 
Mikocheni asili yake ni mzungu mmoja zamani akimiliki eneo akiitwa Michael Chain, Msasani zamani alikuwa akiishi mzee maarufu anaitwa Mzee Hassan,Kwa Aziz ali ndo asili ya familia maarufu ya kina Aziz na hadi leo wana private cemetery pale,kwa Hadija Kopa ni maeneo ya nyumbani kwa Hadija pale Mwananyamala etc,swali nini asili ya majina haya:
Mchambawima?
Makunduchi?
Kunduchi?
Kibandamaiti?
 
Je na mikoa yetu majina yetu yana maana gani?
Dar es Salaam
Mbeya
Tabora
Mara
Iringa
Arusha
Singida
Kilimanjaro
Ruvuma
Mwanza
Shinyanga
Kagera
Tanga
Dodoma
Rukwa
Pwani
Morogoro
Mtwara
Lindi
Manyara
etc etc
 
Wajameni ina maana tunaishi kwenye mikoa tusiyojua maana ya majina yake. Come on please members
 
Kimanzichana ni muunganiko wa maneno mawili...
Kimanzi ni kibinti ambacho kilipendwa sana na mtemi aliyeishi maeneo ya chana hivyo basi eneo hilo likaitwa kimanzi chana yani kibinti cha chana.


Regards
 
Umedanganya Gongo ni neno la Kizaramo lenye maana ya shamba na Mboto ni rutuba kwa maana hiyo Gongo la mboto ilipewa jina hilo kufuatiw eneo hilo kuwa lenye rutuba.

Na Banana ni kweli kuliwa nahiyo Bar lakini hakuna habari ya mgomba wala mdizi.

Kijana wacha ulongo
Kwa Kizaramo shamba ni mgunda!!
 
Msasani:
Hapo zamani nasikia kuwa sehemu hii walikuwa wanaishi Wamakonde na kulikuwa na mtu mmoja maarufu iliyejulikana kwa jina la Musa Hasani. Sasa wamakonde walikuwa wanasema naenda kwa "Mucha Chani" na baadaye wazungu wakaibatiza sehemu ile kuwa Msasani kutokana na kushindwa kutamka "Mucha Chani" kama Wamakonde.
 
Back
Top Bottom