Edward Lowassa: Bora kuwa na Rais kama Kagame ili tuendelee

Ubungoubungo

JF-Expert Member
Jul 28, 2008
2,502
739
Wakati akiongea, nilimsikia akimsifia Kagame kuwa bora tuwe na Rais kama Kagame ili tuendelee, tusiwe legelege, dhaifu dhaifu tuwe na kiongozi mwenye kuchukua maamuzi magumu kama yana manufaa kwa taifa.

My Take:
Kwa upande fulani najua ana kashfa ya Richmond, lakini pamoja na ufisadi wake nadhani ni bora Lowassa mara mia kuliko rais dhaifu. Kuwa na Rais ambaye kidogo ni dikteta kama Kagame au Lowassa kipindi chake cha miaka miwili kama waziri mkuu, ni bora mara mia kwasababu tukikumbuka kwa ile miaka miwili alichachafya wavivu wengi sana na wengine waliacha kazi.

Nadhani tunahitaji Rais kama Lowassa mfano wa Kagame.
 
Hatuwezi kuendelea kwa kuigiza watu wengine tena madikteta. Heri kuwa Nyerere ili tuendelee kuliko Kagame ambaye ni dikiteta anayenuka na mwizi kama Lowassa. Tanzania hatuhitaji tena kiongozi asiyejiamini. Kwanini rais wa Tanzania asiwe Lowassa au Father of All badala ya Kagame? Ni upuuzi kwa mtu mwenye kivuli kujigeuza kivuli cha mwingine wakati anacho kivuli. Shame on Lowassa mwizi anayepokea pesa ya kustaafu wakati alitimliwa.
 
Lowassa ni mpuuzi. Hatuwezi kuendelea kwa kuigiza watu wengine tena madikteta. Heri kuwa Nyerere ili tuendelee kuliko Kagame ambaye ni dikiteta anayenuka na mwizi kama Lowassa. Tanzania hatuhitaji tena kiongozi asiyejiamini. Kwanini rais wa Tanzania asiwe Lowassa au Father of All badala ya Kagame? Ni upuuzi kwa mtu mwenye kivuli kujigeuza kivuli cha mwingine wakati anacho kivuli. Shame on Lowassa mwizi anayepokea pesa ya kustaafu wakati alitimliwa.

Shilingi ina pande mbili, hata Nyerere anameonekano wa kidikteta kwa mtazamo mwingine.
 
Sidhani kama kulishawai onekana rais dictator tz kama nyerere,...si uliona tulivyokuwa tumefumbwa midomo....chadema wangekuwa huru kama hivi leo kama nyerere angekuwa rais au kipindi kile wangefanya hivi? tulikuwa tumefumbwa midomo tukawa mambumbumbu sukuma twende na hakuna maendeleo wala nini...akili ya nyerere peke yake ndo ilikuwa inaongoza nchi, ndio maana kwasababu kwenye akili yake aliamini ujamaa basi na akili za wabongo zikaelekea kwenye ujamaa tukabaki tumepoa na masikini hadi leo.....yaani hapa tulipofikia ni matokeo ya kuongozwa na akili ya mtu mmoja ambaye hapati challenge yeyote ile.

Yeye aanachokiamini ndicho mnachokifuata hakuna wa kumpinga hata kama anakosea....sasa sijui kipi utamsifia nyerere kama si amani peke yake? kama ni maendeleo.....hata wenzie walioanza naye kutafuta uhuru nchi zao zimeendelea kuliko tz.....jaribu kutathmini miaka ile miwili Lowasa aliyofanya kazi kama angefanya vile hadi leo hii tungekuwa katika hatua gani?...pia, kama tunasema ameiba, ameiba nini? prove it....pia hakufukuzwa aliachia ngazi...hahaha....zamani ukiangalia kwenye post zangu zote nilikuwa nampinga hadi kumtukana Lowasa, lakini imefika kipindi nimeona yeye ndo anayetufaa kuliko kuwa na dhaifu...imajini...kama kikwete anapoondoka akamuweka rais awe Asha rose mingiro...aliyepoa kam maji ya kwenye mtungu?...

labda amuweke mama tibaijuka....kidogo inakuja....kwa wengine wote wanaccm waliobaki, no one to match Lowasa...hakuna mtu anayeweza kuiongoza hii nchi kama lowasa ndani ya ccm..labda atoe chadema na si ssm....ccm yupo lowasa peke yake...wengine wote masifuri.
 
sidhani kama kulishawai onekana rais dictator tz kama nyerere,...si uliona tulivyokuwa tumefumbwa midomo....chadema wangekuwa huru kama hivi leo kama nyerere angekuwa rais au kipindi kile wangefanya hivi? tulikuwa tumefumbwa midomo tukawa mambumbumbu sukuma twende na hakuna maendeleo wala nini...akili ya nyerere peke yake ndo ilikuwa inaongoza nchi, ndio maana kwasababu kwenye akili yake aliamini ujamaa basi na akili za wabongo zikaelekea kwenye ujamaa tukabaki tumepoa na masikini hadi leo.....yaani hapa tulipofikia ni matokeo ya kuongozwa na akili ya mtu mmoja ambaye hapati challenge yeyote ile, yeye aanachokiamini ndicho mnachokifuata hakuna wa kumpinga hata kama anakosea....sasa sijui kipi utamsifia nyerere kama si amani peke yake? kama ni maendeleo.....hata wenzie walioanza naye kutafuta uhuru nchi zao zimeendelea kuliko tz.....jaribu kutathmini miaka ile miwili Lowasa aliyofanya kazi kama angefanya vile hadi leo hii tungekuwa katika hatua gani?...pia, kama tunasema ameiba, ameiba nini? prove it....pia hakufukuzwa aliachia ngazi...hahaha....zamani ukiangalia kwenye post zangu zote nilikuwa nampinga hadi kumtukana Lowasa, lakini imefika kipindi nimeona yeye ndo anayetufaa kuliko kuwa na dhaifu...imajini...kama kikwete anapoondoka akamuweka rais awe Asha rose mingiro...aliyepoa kam maji ya kwenye mtungu?...labda amuweke mama tibaijuka....kidogo inakuja....kwa wengine wote wanaccm waliobaki, no one to match Lowasa...hakuna mtu anayeweza kuiongoza hii nchi kama lowasa ndani ya ccm..labda atoe chadema na si ssm....ccm yupo lowasa peke yake...wengine wote masifuri.
Speak for yourself. Ulifungwa mdomo mwenyewe. Mimi sijawahi kufungwa mdomo. Na isingekuwa Nyerere sasa hivi tungekuwa tumeganda na CCM.
 
Samahani naomba kuuliza: Hivi kampeni urais zimeanza? WANAJF WALIO MAKINI TU NDIYO WANAORUHUSIWA KUTOA MAJIBU
 
Mtu mwizi halafu waziri mkuu mstaafu, du eti anafa kama kagame, MNAEMDANGANYA NANI INAONYESHA DHAHILI MMETUMWA TU NYIE HAIWEZEKANI
 
Tusirudie makosa tena, tuweke vigezo vya mtu amefanya nini.

Lowasa namkubali, ndani ya miaka miwili alifanya kazi kubwa na kuisimamia.

1. Aliweza kufuatilia mkataba uliotuzuia kutumia maji ya ziwa Victoria uliowekwa mwaka na ukatenguliwa leo watu wa Shinyanga wanatumia maji bwerere.
2. Aliweza kusimamia uanzishwaji wa shule za kata,natumaini angewezesha hata walimu kuwepo ktk shule hizo.
3.
 
Wakati akiongea, nilimsikia akimsifia Kagame, kuwa bora tuwe kaksi kama kagame ili tuendelee, tusiwe legelege, dhaifu dhaifu..tuwe na kiongozi mwenye kuchukua maamuzi magumu kama yana manufaa kwa taifa.....kwa upande fulani...najua jamaa lina kashfa ya richmond,....lakini pamoja na ufisadi wake, nadhani ni bora Lowasa mara mia kuliko rais dhaifu....kuwa na Rais ambaye kidogo ni dictator kama kagame au Lowasa kipindi chake cha miaka miwili kama PM, ni bora mara mia kwasababu tukikumbuka kwa ile 2 years alichachafya wavivu wengi sana na wengine waliacha kazi on da spoti....nadhani tunahitaji rais kama Lowasa.....mfano wa kagame...tukijachagua rais dhaifu tena, tutachezewa ngoma za kikwere na hatutafaidi chochote....zaidi ya migawanyo katika nchi na umasikini.

Mawazo mfu.
 
Lowassa ni mpuuzi. Hatuwezi kuendelea kwa kuigiza watu wengine tena madikteta. Heri kuwa Nyerere ili tuendelee kuliko Kagame ambaye ni dikiteta anayenuka na mwizi kama Lowassa. Tanzania hatuhitaji tena kiongozi asiyejiamini. Kwanini rais wa Tanzania asiwe Lowassa au Father of All badala ya Kagame? Ni upuuzi kwa mtu mwenye kivuli kujigeuza kivuli cha mwingine wakati anacho kivuli. Shame on Lowassa mwizi anayepokea pesa ya kustaafu wakati alitimliwa.

Just be flank,hivi unaweza kumfananisha lowasa kiuongozi na hao wengine?,jamaa alikuwa sio mchezo,pamoja na mapungufu aliyonayo bado record yake ya utendaji haijaweza kuvunjwa ndani ya miaka yake miwili ya uPM.
 
Ni upuuzi Lowasa kusema bora Kagame kwanza kama yeye anajiamini kwanini aseme hivyo?.

Kama mnaona Kagame bora Kagame mwenyewe yupo, mchakato wa katiba upo kengeni hoja kuwa mnataka rais wa kuajiriwa alafu wewe na Lowasa wako mumuajiri huyo Kagame, njia ya pili subirini tukiingia kwenye shirikisho la EAC aje kutawala :
 
shilingi ins pande mbili....hata Nyerere anameonekano wa kidikteta kwa mtazamo mwingine.

Sijui kwa nini watu wanamsifu Nyerere kiasi hicho.He had his good and dark sides.Kwa mfano kwa kiasi fulani alifanikiwa kuleta umoja wa Watanzania ingawa sijui kwa nia gani.Inawezekana ni katika mkakati ule ule wa serikali moja ya kishetani ya dunia,which is a bad side.Pia alifanikiwa sana katika kutoa elimu kwa watanzania bure,again sijui kwa nia gani,one can argue on negative sides of this endevour.Mbaya sana ni kwamba Nyerere ali-mismanage uchumi wa Tanzania kwa kiwango cha juu sana,kwa hili sitakuja kumsamehe.No, tuliteseka sana,hasa baada ya vita ya kumng'oa Iddi Amin.
 
Back
Top Bottom