Kwanini Prof. Baregu amenyimwa kazi UDSM?

.. hivi vibabu visipopumzika siye makinda tukimaliza skuli tutafanya kazi wapi?
Sasa kumbe hujamaliza skuli? Sasa akistaafu kabla wewe hujawa na PhD nani atawafundisha wadogo zako? Au simply, nani atakufundisha wewe? Lazima vacancy ijazwe na mtu mwenye sifa, siyo mtu anayetafuta sifa.
 
Naomba kufahamishwa.

Hivi huyu "erudite" msomi Prof. Mwesiga Baregu ni raia wa wapi? Uganda au Tanzania?
 
- Mkuu vipi tena hapa, Chief Secretary ndiye anaye-handle wote unaowasema, watumishi wa juu wa umma na wanasiasa, hawa wote ni yeye mwenye mafaili yao, sasa kwanini hii ishu imeenda kwa Waziri na sio kwa Luhanjo?

- Na besides, hii ishu ilitakwia kuwa handled na utawala wa chuo kwanza, kabla ya kufika kwa Waziri, something is not right mkuu na jinsi hii ishu inavyokuwa handled ninaamini kuna mkono mzito sana unahusika!

Respect.

FMEs!

mkuu wa chuo na mkuu wake wa idara ,...nadhani dr bana...waliulizwa wakasema ..baregu ni Lulu na hawako tayari kumuachia ...kabisa....!!!..ghasia anasema Baregu HANA SOKO....Sidhani kama amepata kufundishwa naye hadi afikie kumponda wakati wote aliowafundisha wanamsifia...
naona kwa kuwa ishu imeingia siasa katibu mkuu na mkuu wa chuo hawakutaka kuiongelea wakamtupia waziri!!
ukiangalia list ya halmashauri kuu CCM utagundua wengi tu ambao ni watumishi wa umma..sijui imekaaje hii!!
kuna wanaofikiri baregu ana njaa ..ukweli hana njaa ..that guy is a revolutionery ....ameamua kufuatilia haki yake ili aweke rekodi sawa....hasukumwi na pesa ...kabisa!!!..kwani hata mkataba wenyewe una pesa kidogo...maprofesa kama issa shivji ...na wengine wa zamani akiwamo marehemu haroub othman ...hawakai chuo kikuu kwa ajili ya pesa ..wangeweza kwenda popote ..na ni kati ya wachache ambao walikataa katu kupewa vyeo serikalini zaidi ya kubaki wanagarakati.....hawa ni watu ambao wanapenda kubakia pale mlimani wakifuata imani ZA AZIMIO LA ARUSHA [mwalimu nyerere] kuwa ..NITAJIELIMISHA KWA JUHUDI ZANGU ZOTE NA KUTUMIA ELIMU YANGU KWA FAIDA YA UMMA.....huu mshahara mbuzi unaolipwa hauwatoshi bali wameridhika...na ndio maana sasa serikali inapata taabu kuwa maintain ma profesa vijana .....kwani wao tofauti na kina SHIVJI ni wa enzi za sasa .,,,,..na compromise kwa ni serikali KUBORESHA MASILAHI !!!
 
Pale akademia huu upuuzi wa public au civil servant hautakiwi kuingia. Pale paangaliwe uwezo wa kufikiri na kufundisha. Ingekuwa ni amri yangu watu kama wakina Issa Shivji wangefia kazini!

Amandla........
 
- Mkuu vipi tena hapa, Chief Secretary ndiye anaye-handle wote unaowasema, watumishi wa juu wa umma na wanasiasa, hawa wote ni yeye mwenye mafaili yao, sasa kwanini hii ishu imeenda kwa Waziri na sio kwa Luhanjo?

- Na besides, hii ishu ilitakwia kuwa handled na utawala wa chuo kwanza, kabla ya kufika kwa Waziri, something is not right mkuu na jinsi hii ishu inavyokuwa handled ninaamini kuna mkono mzito sana unahusika!

Respect.

FMEs!

Kumbukumbu zangu zinaniambia kuwa Utawala wa UDSM walipeleka jina lake pamoja na majina ya wengine wanaotakiwa kuajiriwa kwa mkataba. Inasemwa kuwa yote yalikubaliwa isipokuwa la BEREGU.

Juzi walitaka kumbambikia Mukandara ila naona wameona hii habari bado itarudi kwao tu. Nakubaliana na wewe kuwa hii kazi ilitakiwa kufanywa na kujibiwa na katibu wa Rais na si Waziri. Kujibu kwa waziri kunaonyesha kabisa kuna kitu kinafichwa na kuna mtu hataki kujipaka damu mikononi ingawa ukweli kila mtu anaziona hizo gloves zenye damu zimeandikwa jina la nani.
 
Kumbukumbu zangu zinaniambia kuwa Utawala wa UDSM walipeleka jina lake pamoja na majina ya wengine wanaotakiwa kuajiriwa kwa mkataba. Inasemwa kuwa yote yalikubaliwa isipokuwa la BAREGU.

Juzi walitaka kumbambikia Mukandara ila naona wameona hii habari bado itarudi kwao tu. Nakubaliana na wewe kuwa hii kazi ilitakiwa kufanywa na kujibiwa na katibu wa Rais na si Waziri. Kujibu kwa waziri kunaonyesha kabisa kuna kitu kinafichwa na kuna mtu hataki kujipaka damu mikononi ingawa ukweli kila mtu anaziona hizo gloves zenye damu zimeandikwa jina la nani.

Baregu na Mkandara watakuwa wanajuana sana. nadhani wapo idara moja pale UDSM na ukumbuke kuwa Baregu ni CHADEMA na Mkandara na akina Bana (mkuu wa idara) ni wakuu wa REDET. REDET ni project katika idara yao (so one can imagine the friction)
 
Naona unamung'unya maneno, ingekuwa vyema kama ungesema kwa uwazi kuhusu uhusiano wa hao watu watatu uliowataja.
 
Suala la Prof. Beregu, limeibukia Bungeni Dodoma leo asubuhi katika kipindi cha maswali na majibu, Mbunge wa Viti maalum Chadema, Bi. Halima Mdee, alimuuliza Waziri wa Elimu kuhusu maswali mawili, la kwanza kwanini Prof. Beregu amekataliwa kuongezwa mkataba kwa sababu tuu yeye ni kiongozi Chadema, huku kuna viongozi wengi tuu wa CCM kwenye utumishi wa umma?. La pili, kama Chadema, itampa ushahidi wa majina ya vigogo wa CCM kwenye utumishi wa umma, jee serikali itakuwa tayari kusitisha mikataba yao?.

Waziri wa Elimu, Prof. Magembe kwanza alikwepa swali la kwanza, kwa kutokuzungumzia kabisa sababu za Prof. Beregu kunyimwa mkataba, bali alisema, Prof. Beregu, alishastaafu toka 1999, hivyo mwajiri anao uhuru wa kumuongezea mkataba au hapana. Kwa sasa, mwajiri ameshapata watu wenye uwezo kama wa Beregu, hivyo hahitajiki tena, ndio maana hakupewa mkataba mpya.

Waziri akakaa, Naibu Spika akasema swali linalofuata (Swali jipya), Mdee akasisimama kumwambia Naibu Spika, swali la pili halijajibiwa. Naibu Spika akalazimisha limejibiwa wewe ndio hutaki kukubali. Akamshum dowm Halima Mdee na kuitisha swali linalofuata.
 
Ninafikiri Prof. Baregu amenyimwa kazi UDSM yaweza ikawa ni Mungu anataka kubariki mwishoni.Njia za Mungu ni tofauti sana na za wanadamu wao wanaweza wakafirkiri wanamkomoa kumbe sivyo.Nawafahamu madaktari (wa kusomea (PhD)) wawili ambao wako nje. Wote walifanya kazi UDSM. Mmoja nafikiri alisitahafu akawa nje ya katika nchi moja ya kusini mwa Afrika. Hivi sasa nchi ile wanamtumia kwa kupata ushauri wake, pia i mmoja wa Makamu wakuu wa chuo Kikuu cha nchi ile. Maisha yake siyo kama alivyokuwa Tanzania. Prof Baregu achangamke kutafuta kazi nje atapata tu. Mwingine amekwenda South baada ya pale alipokuwa akifanyia kazi kukawa muda wake wa kufanya kazi ukawa umeisha kurudia mkataba uliokuwapo ikawa shida . Kilichotokea akapata kazi South Mshahara mzuri zaidi. Prof. aulizie kazi huko, au la siku hizi kuna vyuo vingi lakini inaweza ikawa ni mizengwe kam ya UDSM aachane nao atafute sehemu nyingine bila shaka italipa
 
1265982339_pindanew.jpg

Waziri Mkuu Mizengo Pinda

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema, uamuzi wa Serikali kusitisha mkataba wa aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwesiga Baregu,ulikuwa sahihi...
Pinda ametoa msimamo huo bungeni baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Lyimo (Chadema) kuhoji kile alichosema ni Serikali kujikanganya kuhusu suala hilo la Profesa Baregu.

Akirejea majibu ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe ya hivi karibuni wakati akimjibu bungeni Mbunge mwingine wa Chadema aliyeuliza kuhusu suala hilo, Lyimo alisema kumekuwa na kauli zinazokinzana kuhusu ajira ya mwanataaluma na mwanasiasa huyo.

Kwa mujibu wa Lyimo, Profesa Maghembe katika kujibu, alisema Serikali haikusitisha mkataba kwa kuwa Profesa Baregu anajihusisha na siasa huku akisema kauli hiyo inakinzana na ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia.

“Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi alisema hakuondolewa kwa sababu ni kiongozi wa Chadema maana wapo viongozi wa vyama vingine tuko nao kwenye kazi ambao hawajastaafu. Je, huku sio kujikanganya na kuwachanganya wananchi?” alihoji Lyimo.

Akimjibu mbunge huyo katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo, Pinda alisema, “sina hakika kama ulisoma Waraka wa Utumishi. Inawezekana tatizo linaanzia hapo. Kama hukupata nafasi kuusoma kuona maudhui, unaweza kudhani wamejikanganya".

Pinda amesema, mwajiri ana mamlaka kumwondoa mtu aliye kazini kwa utaratibu wa mkataba. Alisema, “kila unapomaliza, si lazima urudie.”Alisisitiza kwamba waraka umesambazwa kwa umma na unahusu utumishi wa umma.

Aliendelea kufafanua kwamba sababu nyingine ya kusitisha mkataba ni kwa kuzingatia kwamba mtu yeyote akiwa ni mtumishi wa umma, hatakiwi kujihusisha na masuala ya kisiasa. Alisema eneo hilo linamgusa yeyote yule katika utumishi.

Pinda amesema, Profesa Baregu kwa upande mmoja, aliguswa kwenye mkataba baada ya Serikali kuona inatosha.

Hata hivyo alisema hata isingekuwa kwenye mkataba, bado Serikali ingeweza kumchukulia hatua hiyo hiyo kutokana na kushiriki siasa.

Baada ya Waziri Mkuu kujibu hivyo, Mbunge huyo aliendelea kuhoji: Pamoja na kwamba umejibu kwamba watumishi wa umma bado hawastahili kuwa katika siasa, lakini Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi alisema viongozi wengi wa vyama vya siasa wanaendelea kufanya kazi nao.

Wanaruhusiwa kuwa kwenye utumishi? Waziri Mkuu alisisitiza, “Tukubaliane kwanza uamuzi wa mwajiri ni sahihi.”

Kuhusu suala la kuwepo watumishi wa umma wanaojihusisha na siasa, Pinda alimtaka mbunge huyo apeleke majina kama anayo ili hatua zichukuliwe.

Hii ni mara ya pili suala hilo la Profesa Baregu kufikishwa bungeni na wabunge wa Chadema kupitia kwenye maswali.

Wa kwanza kufikisha suala hilo, alikuwa Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Mdee aliyehoji kwa kutaka apewe nafasi ili awasilishe vielelezo vya watumishi wa umma ambao wamekuwa wakijihusisha na siasa.

CHANZO:
HABARILEO
 
Baregu, baregu......

Huyu ni moja wa foreseer wa Tanzania, hata wakati Mkandara anakuwa VC watu walishaonywa haya yatatokea. Kama ilivyo desturi ya maprofesa huwa hawana muda wa kuipigania jamii, kudai haki, mpaka yanavyowakuta, ni maprofesa wengi wana mtindo huu

Kwa kifupi alijua, hata kama alijifanya haoni, alijua kuwa iko siku Mkandara ataanza kumchinja mmoja baada ya mwingine, simply kwa sababu ni wabinafsi na hawana umoja!!!

Ukitaka kuona mfano halisi wa Dr, na maprofesa ambavyo hawana muda na nchii hii, nenda mavyuoni!! sasa kama profesa hakujua hili wa form six atajua nini!!

Mkandara ndiye aliyempigia debe JK kupitia REDET(BBC wakisaidia),ndiye aliyemwambia JK/CCM watumie kauli ya nguvu mpya kasi mpya, ari mpya, ndio huyuhuyu aliyemwambia JK let them 'speak' awaachie watu waongee tu kuhusu ufisadi, maana asingepokea ushauri huu, EL alishaanza kuwawekea zengwe waandishi. JK na Mkandara kupitia gazeti lenu mnaloliona la kufichua wafisadi wala hawana hiyana wanaandika kweli kuhusu ufisadi! si wamefanikiwa, haujasikia watanzania wanatoa sababu 102 za kikwete aendelee kuongoza na sababu ni kuwa mafisadi " wanafichuliwa" !!! hawaendi jela, hawarudishi mali , ila furaha yetu ni kuwajua!

2010 hiyoo JK ikulu!
 
Mjadala huu hauna maana tena, Profesa amesdhakubaliana na walioamua waliyoyaamua na sasa anakula maisha yake mapya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT).

Ameanza kufundisha history of political ideas Jumatatu hii kwenye kituo cha SAUT kilichopo Dar es Salaam pale Msimbazi kwa wanafunzi wa shahada ya uzamili katika mawasiliano ya umma na leo Ijumaa ndio anaanza kuzama zaidi na kutakuwa na mjadala mkali amewaambia wanafunzi wakajiandae ili leo watoe maoni yao kuhusu uhalali au ubatili wa uamuzi wa Bunge kufunga mjadala wa Richmond.

Tumwache ale maisha mapya huko.
 
kumpa prof.baregu mkataba wa kufundisha udsm ni sawa na kuiambia serikali ikalie kaa la moto matakoni. ndio maana unawaona kina sofia simba wanahaha kumnyima mkataba, wanaanza kuongea pumba zao za kuwasuport but in reality, wanamwogopa sana
 
Ukweli ni kuwa Prof Baregu kanyimwa mkataba mpya;na habari hii kama yupo kwenye Sabbatical leave HAINA UKWELI WOWOTE na ITUPILIWE MBALI

UDSM chini ya Prof Mukandara hawajatoa sababu zozote"cardinal"kwa nin i hasa Prof Baregu kanyimwa mkataba mpya ila kuna habari za harufu ya kisiasa;habari ambayo mimi binafsi bado sijaithibitisha!

Kuelezea hali hii ya kunyimwa mkataba mpya Prof Baregu;CHADEMA walikuwa na haya ya kusema:

"Wakati huo huo, chama hicho kimelaani taarifa ya uamuzi wa serikali kwa kushirikiana na Baraza la Wadhamini wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wa kukataa kuongeza mkataba wa aliyekuwa Mhadhiri Mwandamizi chuoni hapo na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Profesa Mwesiga Baregu.

Dk. Slaa alisema uamuzi huo una dalili za kumkomoa kutokana na msimamo wake thabiti wa kuikosoa serikali, kutetea umma na kuunga mkono
CHADEMA.

“Kamati kuu imelazimika kuamini hivyo kwa kuzingatia hali ya kisiasa nchini wakati maamuzi hayo yanafanyika, huku kukiwa na uhaba wa wahadhiri waandamizi kama yeye katika chuo hicho,” alisema Dk. Slaa.
Alisema kilichomtokea Profesa Baregu ndicho kilichotokea kwa Dk. Masumbuko Lamwai, aliyekuwa kiongozi ndani ya Chama cha NCCR-Mageuzi ambaye aliamua kurudi CCM"

Kwa ufupi,Prof Mwesiga kanyimwa makataba mpya na wala hayupo kwenye likizo ya matibabu kama ilivyosemwa na wana JF wengine!

upo sahih mkubwa
 
Pale akademia huu upuuzi wa public au civil servant hautakiwi kuingia. Pale paangaliwe uwezo wa kufikiri na kufundisha. Ingekuwa ni amri yangu watu kama wakina Issa Shivji wangefia kazini!

Amandla........
Unafiki wa serikali ya magamba huo! Tumeuzoea! Hukumbuki ya Tido Mhando?
 
Suala la Prof. Beregu, limeibukia Bungeni Dodoma leo asubuhi katika kipindi cha maswali na majibu, Mbunge wa Viti maalum Chadema, Bi. Halima Mdee, alimuuliza Waziri wa Elimu kuhusu maswali mawili, la kwanza kwanini Prof. Beregu amekataliwa kuongezwa mkataba kwa sababu tuu yeye ni kiongozi Chadema, huku kuna viongozi wengi tuu wa CCM kwenye utumishi wa umma?. La pili, kama Chadema, itampa ushahidi wa majina ya vigogo wa CCM kwenye utumishi wa umma, jee serikali itakuwa tayari kusitisha mikataba yao?.

Waziri wa Elimu, Prof. Magembe kwanza alikwepa swali la kwanza, kwa kutokuzungumzia kabisa sababu za Prof. Beregu kunyimwa mkataba, bali alisema, Prof. Beregu, alishastaafu toka 1999, hivyo mwajiri anao uhuru wa kumuongezea mkataba au hapana. Kwa sasa, mwajiri ameshapata watu wenye uwezo kama wa Beregu, hivyo hahitajiki tena, ndio maana hakupewa mkataba mpya.

Waziri akakaa, Naibu Spika akasema swali linalofuata (Swali jipya), Mdee akasisimama kumwambia Naibu Spika, swali la pili halijajibiwa. Naibu Spika akalazimisha limejibiwa wewe ndio hutaki kukubali. Akamshum dowm Halima Mdee na kuitisha swali linalofuata.

Kwa Baregu sio sawa ila kwa Dr Migiro ni sawa
Kweli hii ndio Tanzania
 
Back
Top Bottom