Orodha ya biashara kwa mtaji kiduchu zenye uhakika wa kukulipa awamu hii ya tano

Ni muda sijaandika uzi katika jukwaa hili, nimepata msukumo leo baada ya kisa kilichotokea apa katikati na kunifanya nione umuhimu wa kukumbushana lakin pia iwe kichocheo cha kuamsha tafakuri katika maamuzi yetu kweny biashara zetu.

Iko hivi, mwaka juzi nilipata simu kutoka kwa mentor wng na kwa ufupi alisema kuwa kuna kijana amempatia mawasiliano yangu na kunitaka nionane nae. Kweli siku hiyohiyo kijana yule alinipigia na baada ya mazungumzo alitaka kuja ofisini kwa ajiri ya swala lake lakini nilimkatalia kutokana na ratiba ya siku hiyo. Tulipanga siku ya kuonana na nilichogundua kwa mazungumzo ya simu tu kuwa jamaa ana 'mizuka'.

Siku iliwadia tukaonana na baada ya salam na stori kidogo nilimuuliza kuhusu kiini cha sisi kukutana. Kijana huyu ambae wakati wote alikuwa 'mchangamfu' alinieleza kuwa ana 'Project' ambayo amekuwa akifanyia tafiti kwa muda mrefu na kuwa amepata 'wazito' ambao wako tayari kuwekeza kwnye project hiyo. Kwaiyo alikuwa ana hitaji mtu ambae atamsaidia katika mawazo ya namna ya kuongeza na kuboresha project hiyo.

Wakati huu tunaonana jamaa alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni ya mentor wng na hivyo alikuwa amemuomba amsaidie katika hilo. Kwasababu mentor hakuwepo nchini wakat huo na kulikuwa hakuna dalili yotote ya kurejea karibuni, ali m-direct jamaa kwangu kwa ajiri ya kazi hiyo.

Nilipata muda wa kupitia mpango wake biashara ('business plan') na baada ya maswali niliyomuuliza kujibiwa kwa usahihi na kwa uwazi kabisa (labda sababu alipewa assuarance na mentor wangu). Binafsi niliona kabisa huyu ni mtu ambae kafanyia tafiti wazo lake sio zile 'empty set', hivo sikushangaa yeye kushawishi wazito kwa haraka.

Sote tunafaham kinachovutia kwenye business plan ni kipengere cha 'financial statement' (projections) na apa ndipo nilipogundua dosari kubwa. Pamoja na wazo kuwa zuri ila hesabu za makadirio ya mapato na matumizi zilikuwa kinadharia sana yaani 'they were simply based on fantasie rather than reality'. kwa lugha ya kichumi alitumia kitu kinaitwa 'haphazard approach' sina tafsir nzur ya kiswahil lakin itoshe kusema alijipendelea faida sana kinyume na hali halisi.

Hata nilipojaribu kukadiria degree of operating revenue bado nilikuwa nagota kwenye hasara tu. Na kwa mtazamo wangu nilijaribu kumwelesha kuwa kwa 'uchumi wa awamu hii' itakuchukua almost miaka 4 na kitu kufika ata ile hatua ya break even yaani gharama za uzalishaji ziwe sawa na mapato.

Kauli zangu zilianza kufifisha tabasamu la 'amigo' na kwa muda tulipishana sana lakin tukaafikiana kuwa 'tutengeneze' leap of faith hypothesis yaani 'mikakati' ya muda yenye ufanano na lile wazo kuu kama kujaribu soko kabla ya kuingiza mtaji wote. Haikuwa rahisi kwa siku iyo basi tukaachana na mimi nilitimiza ahadi yangu ya kumtumia mawazo yng kwa email.

Tuliendelea kuwasiliana kwa yeye kuni update maendeleo ya hiyo project yake, nikiwa nafaham anafanyia kazi yale 'tuliyokubaliana' na baada ya muda mawasiliano yalikatika kabisa na mim nikawa nilisha sahau kabisa.

Ni mpaka juzi ikiwa ni takriban mwaka toka tuwasiliane nimepata email yake nikiwa safarin ambayo ndio imenifanya niletee uzi huu. Huyu bwana baada ya mawasiliano yetu yeye aliendelea na project yake kama alivokuwa amepanga awali ata labla ya kukutana na mim. kifupi alikuwa yuko 'obsessed' sana na ile 'perfect idea' yake kiasi kwamba ilimfanya kipofu hata kushindwa kuona reality. Kwaiyo yeye alikuwa anatafuta tu mtu wa ziada kumbariki na si kukosoa.

Sasa project ina mwaka na kitu na hawajaweza ku cover ata gharama za uendashaji, na wale wazito wame mkalia kooni hajui afanye nini. Ingawa ni mwaka tu na kwa sisi wazoefu tunasema ni mapema kutoa judgement lakini still chances of survival are limited

kweli hali ya biashara mtaani ni mbaya bidhaa haziuziki lakin je unauza bidhaa sahihi kwa wakati huu?? usije ukawa una lalamikia kumbe bidhaa unazouza ww watu hawazihitaj wakat huu.

kila awamu huja na changamoto zake na hata matumizi ya watu hubadirika hivyo ni kazi yako wewe mjasiriamali kuwa mwepes wa kung'amua nyakati na kubadilika pale upepo wa mabadiliko uvumapo.

Pesa kwa sasa imekuwa adimu na zile chache walizonazo watu wanatumia kwa mahitaji yao ya msingi au zile huduma/bidhaa ambazo wana urahibu/addiction.

Swali la kujiuliza katika mahitaji yao ya maingi wewe unawazuia nini??.

Je unafahamu kuwa kuna bidhaa ambazo ni addiction kwa watumiaji??

Kwa muktadha wa maswali hayo, mjasiriamali mwenye kiwanda chako au biashara ili uweze kupata uhakika wa mzunguko wa fedha ni lazima bidhaa/huduma zako zizunguke kwenye maeneo hayo mawili.

Mahitaji ya msingi yanafahamika, apa nita gusia zaidi upande wa biashara/bidhaa zenye urahibu.

Neno urahibu limekuwa likitumika sana kuelezea kuhusu utegemezi wa madawa ya kulevya, Lakin ni nadra kulisikia kwenye bidhaa/huduma tunazotumia kila siku.

Basi chukua hii kutoka kwangu(THE LIST) na utizame ni namna unaweza kupiga pesa.

** Apa ntakupa THE LIST ya biashara/huduma ambazo zitakuhakikishia uhakika wa soko ata katika ichumi uliodorora**

Kwa namna ambayo itadizain mpango wako wa biashara basi hakikisha unazunguka kwenye zile bidhaa au huduma ambazo hutengeneza urahitbu kwa mteja baada ya muda wa matumizi.

Kwa muktadha huo, hii ni orodha ya sekta mbalimbali ambazo unaweza ukabuni bidhaa|huduma ambayo afe kipa afe beki lazima itanunuliwa tu.

Sekta ya urembo na utanashati
-urembo na utanashati ni tabia ambayo si rahisi kuiacha, hii ni kwa wadau wa rika zote..waume kwa wake.

kuna biashara nyingi ambazo unaweza ukafaanya ndani ya kipengere hiki zaidi tizama ni vitu gani watu hutumia zaidi, mafuta, perfumes, mawigi, viatu, saloon n.k

Vilevi na hasa pombe.
Urahibu wa pombe wala hauhiitaj maelezo mengi, sekta hii yenyew iko wazi ata mitaani uko..yaani vyuma vimekaza lakin bar zinajaa

Apa unaweza buni wine yako mwenyew, wakala wa jumla wa pombe, kufunvua bar au grocery

Michezo
Kwa bongo mpira wa miguu una wapenzi wengi na ww unaweza kutengemeza pesa kupitia urahibu huu kwa kufungua betting centre, gori la kuonyesha mpira, kuprint tshirts, video games uko iswazi n.k

Repairing centre..
kipini hiki badala ya mtu anununue gari au simu mpya ni bora atengeneze ile ya zamani, wekaza eneo kwa ku kutoa hizo huduma.

Huduma za Vyakula
Sekta hii kwa maneno ya Mo anasema kwa mtu yeyote anaetaka utajiri Africa basi awekeze katika matumbo ya watu. Kwa maneno hayo ni dhahiri sekta hii ina wateja wengi sana na ni ngumu kuyba ata uchumi ukiyumba vipi.

Ni sekta pana inayoanzia kwa mkulima, sokoni, kiwandani mpaka kwa mlaji. Sasa katika chain yote hiyo wewe unachangia vipi?

Itaendelea...

Nikukumbushe Mjasiriamali mwenzangu huna sababu ya kushindwa kuingiza faida ya laki moja au zaidi kwa siku kwa kisingizio uchumi umeyumba. Ukiona unalalamika basi kuna kitu unafanya sio sahihi.

Haya ni mawazo ya kivitendo kutoka kwa mjasiriamali (THE LIST) na sio falsafa mfuu au porojo za semina uchwara..yanatekelezeka!!

Haki za umiliki zote zimehifadhiwa

THE LIST.
Thread nzuri inatukumbusha umuhimu wa ku 'evolve'kwenye biashara zetu. Kuna wafanyabiashara wadogo wanadhani matukio ya kisiasa na uchumi yanayotokea Tanzania na duniani hayana impact kwenye biashara zao hadi its too late.

Pia kuna umuhimu wa wafanyabiashara wadogo kufuatilia bunge la budget kuona jinsi wanavyoweza ku influence tozo za kodi kwenye biashara zao kuna umuhimu sana kwa wafanyabiashara wadogo kuelewa siyo kazi tu ya wabunge na serikali kuwa wekea viwango vya kodi au kurekebisha mazingira ya biashara zao. Wanajukumu la kutetea biashara zao kupitia vikao na madiwani na wabunge wao na siyo kukimbilia kufanya maandamano baada budget kupitishwa na bunge na kodi kuwa sheria. Wale TRA sheria inawalinda, pale mtakapoanza kuinfluence wabunge na serikali waanze kutunga sheria za kodi zinatakazo wapendelea hao TRA hawatawasumbua. Ushauri wangu wafanyabiashara wadogo waanze kuwa proactive.
 
Hskuna asiyetaka kulipa kodi, binafsi nilienda mwenyewe TRA na mpaka sasa nipo na leseni yangu mkononi, sina hofu ya kufungua kibanda changu, tatizo ni ukadiriaji wa kodi kwa anayeanza kufanya biashara kama mimi. Hili suala huwezi kulisemea kama hujaenda TRA ukakutana na uhalisia
 
Hskuna asiyetaka kulipa kodi, binafsi nilienda mwenyewe TRA na mpaka sasa nipo na leseni yangu mkononi, sina hofu ya kufungua kibanda changu, tatizo ni ukadiriaji wa kodi kwa anayeanza kufanya biashara kama mimi. Hili suala huwezi kulisemea kama hujaenda TRA ukakutana na uhalisia
Haya matatizo ya kuwa na makadirio makubwa ya kodi, leseni chungu nzima (sijui Fire,TFDA,TBS,OSHA etc) na mifuko ya kila aina ya kuchangia (NSSF,WCF etc) yatapungua kama wafanyabiashara especially wadogo wakianzisha lobbying groups zao. Watengeneze networks na wabunge na serikali iliwa influence sheria zinazotungwa bila hivyo hesabu maumivu. Haiwezekani kupata sheria rafiki kama watunga sheria wenyewe hawajahi kufanya biashara hata siku moja ya maisha yao.
 
Le mutuz akili kubwa atapitia sasa hivi(nimesema tuu)

Anyway kila kitu hapo ni fact!!
Nimewai jaribu hiyo ya chakula kipindi cha nane nane mkoa fulani nikiwa bado ni mwanafunzi wa chuo.Sio siri kwa mtaji mdogo sana ndani ya siku 10 tu nilipata millions.
ILIKUAJE BOSS TUPE MECHANISM
 
chief inaonekana hii ishu ya tra na kodi ni changamoto kubwa sana kwa wajasiriamali sio mbaya km ukija na uzi wa kuwaelimisha namna ya kupata favour ya iz kodi
Ukilipa kodi unakuwa huru sana katika biashara yako. Hakuna namna lazima kodi ilipwe, changamoto ni makadirio yanayofanywa na TRA, huwezi kukwepa kodi labda ufunge biashara.
 
Safi Mkuu kwa kumpa ushauri huyo jamaa kutokana na business plan yake, kilichomuumiza ni upupa wake bila kuangalia hali halisi. Pili kwa ushauri murua wa aina gani za biashara mtu anaweza akatumbukiza senti yake na mrejesho ukawa vyema tu.
Asante sana
 
Hskuna asiyetaka kulipa kodi, binafsi nilienda mwenyewe TRA na mpaka sasa nipo na leseni yangu mkononi, sina hofu ya kufungua kibanda changu, tatizo ni ukadiriaji wa kodi kwa anayeanza kufanya biashara kama mimi. Hili suala huwezi kulisemea kama hujaenda TRA ukakutana na uhalisia
Hebu fafanua tatizo kwenye ukadiriaji. Kwa ninavyofahamu ukienda TRA maelezo yako ndio yanawapa wao muelekeo wa kadirio.
 
-Nyie binadamu mnaifanya JF iendelee kuwa 'superbland' kwa social networks Tanzania.

-'Beauty with brain', ndio kielelezo pekee kinachostahil kuelezea uwepo wenu maana tofauti na wale 'magugu maji' nyie mmepata muda wa kufuatilia makala kama hii..

Am super humbled( le boma nyee)!!
Cc. Inna shunie

Jamaani Mzee wa empty set katukubali kinomaaa......woyoooooooo
 
Back
Top Bottom