Jifunze Mambo Mbalimbali Kuhusu Kilimo cha Tunda la Makakara (Passion)

LAT

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
4,401
1,312
maxresdefault.jpg

Heshima kwanza,

Wakuu, nina shamba eneo la Makaa Yamu, Kirua Vunjo, wilaya ya Moshi vijijini lenye ukubwa wa ekari kumi na sita 16 (limepimwa na hati miliki)

Shamba lipo kilometer nne kutoka barabara kuu iendayo Dar es salaam na Mombasa.Shamba hili lipo eneo la ukanda wa tambarare Kusini mwa mlima Kilimanjaro.Ukanda wa eneo hili lilipo shamba langu ni mkubwa sana na wamiliki wengi wa mashamba haya hulima mahindi wakati wa msimu wa mvua (masika).

Eneo hili lina rutuba nzuri sana, udongo wake ni tifutifu. Inaonyesha kuwa water table yake haipo mbali sana.

Wakuu wazo langu ni kugeuza uwanda huu kuwa horticultural hub kwa kilimo cha aina ya zao la matunda ya passion lengo likiwa ni kuweza kusindika tunda hili la passion na kupata passion powder kwa ajili ya flavoring kwenye bidhaa mbali mbali za chakula kama ice creams, cakes, fruit yougurt, juices and soft drinks, jams n.k

Pia tunda hili la passion linaweza kutengeneza wine mzuri sana.

Naomba pia anayejua bidhaa tofauti zinazotokana na zao hili na masoko yanayohusu passion fruit.

Wakuu ninaomba ushauri juu ya utaalam wa ulimaji wa zao la passion, hivyo basi nikiweze kuanzisha kilimo hicho nitatoa mfano wa shamba bora na kuwabadilisha wakulima wote wa eneo / uwanda huu waweze kulima hili zao na baadae kulisambaza maeneo ya nchi nzima ambapo zao hili products zake zina soko lenye bei nzuri na kubadilisha maisha ya wananchi hawa.

Haya ni mawazo tu ya mwanzo ambayo sijayafanyia utafiti wa kina nikisubiri changamoto na michango ya wenzangu wapenda kilimo na wenye utaalam na uzoefu zaidi .

Pia yeyote yule humu JF anakaribishwa kutoa ushauri na mchango wake.

WADAU WENGINE WANAOPENDA KUJUA KUHUSU KILIMO HIKI
Nataka nilime passion (karakara) lakini sijui soko lake kwa hapa Tanzania lakini nimeamua ku-invest kwa Kiwango kikubwa sana hebu nipeni ushauri wana jamvi kabla ya kuanza.

Je soko lipo?!.

Je ni changamoto zipi

Kwa ushauri zaidi
Poleni na majukumu ndugu zangu.

Nilikuwa naomba kufahamishwa kilimo cha tunda hili mchakato mzima ukoje hadi kuvuna na soko lake likoje.jinsi ya kuandaa shamba na jinsi ya kupanda.

Wakati sahihi wa kupanda, huchukua mda gani hadi kuvuna.

Changamoto na jinsi ya kuzitatua

Huuzwaje je ni kwa kilo au kwa kipimo gani na bei gani.

MICHANGO YA WADAU MBALIMBALI
KILIMO BORA CHA PASSION (MAKAKARA)

Ni mimea inyotambaa na kuhimili hali nyingi za hewa (sio ukame) mme huu hustawi zaidi ukanda usio na baridi wastani wa 20c – 30c na kiasi cha mvua 1500mm za ujazo kwa Mwaka, tunda huwa na ukubwa wa sentimeta 10 kwa kipenyo na uzito gramu 90, kuna aina kadhaa za matunda haya lakini yale ya kijani/manjano hustawi zaidi ukanda wa pwani na yale yenye wekundu Fulani hustawi zaidi maeneo ya misitu, hupendelea udongo wa kichanga wenye mbolea na usiotuamisha maji, pia udongo usiwe na chumvi nyingi na pia kusiwe na mwamba chini kasi cha mita moja tu.

UPANDAJI
Mbegu zipandwe kwanza kwenye mifuko ya plastiki yenye udongo wenye rutuba ya kutosha , kiasi cha Mbegu 3 kwa kila mfuko na mara zinapoota mimea ikingwe na jua kali na ikifikia urefu wa sentimeta 30, huweza kuhamishiwa shambani
Kwenye shamba lako hakikisha kuna nguzo zenye waya mmoja kwa ajili ya mimea kutambaa juu yake, sehemu ya juu baada ya nguzo kuzikwa chini ibakie kama mita mbili na kati ya msatari na mstari iwe ni mita 2 (ukanda wa pwani ) na mita 3 ukanda wa juu kiasi, na umbali kati ya nguzo na nguzo kwenye mstari ni mita 6, na mimea ipandwe umbali wa mita 3 kati ya nguzo na nguzo kufuata mstari.

UANGALIZI
MBOLEA
Mbolea za viwandani ziwekwe kutokana na hali ya udongo, muone afisa ugani kilimo ili afanye vipimo kujua mahitaji na upungufu wa udongo,

MAGONJWA WADUDU
Wadudu kama chawa wa mimea na mchwa wekundu ndio adui wa makakara, pia fangasi husshambulia sana maua ya makakara. Dawa za jamii ya kopa zitumike mara dalili za magonjwa au wadudu kuonekana, kiasi cha kilo 2.8 – 3 hutosha kwa hekta moja au gramu 225 kwa ajili ya dumu moja la lita 20

MAGUGU
Makakara yanatakiwa yawe kwenye shamba safi lisilo na majani na magugu, jembe la Mkono au madawa kama ROUND-UP na GRAMOXONE ynaweza kutumika mimea ikishaefuka na kuwa juu kwenye waya

KUFUNDISHA MIMEA
Ni lazima kuyafundisha matawi mawili ya kwanza kwa kuyaelekeza kutambaa kwenye waya kila moja likielekea upande wake na matawi yatakayoota kutokana na matawi makuu nayo yaelekezwe juu kwenye waya yakifikia ukubwa wa sentimeta 30 – 40

KUPUNGUZA MATAWI
Silazima kupunguza matawi kwa sababu mmea mkubwa zaidi ndio hutoa matunda mengi zaidi, labda kama kuna matatizo katika uchumaji ndio unaweza kupunguza baadhi ya matawi kiasi.

UVUNAJI
Uvunaji huanza baada ya miezi 8 – 9 baada yam mea kupandwa na matunda hukusanywa baada ya kudondoka yenyewe chini baada ya kuiva kila baada ya wiki moja, matunda yahifadhiwe sehemu kavu na isiyo na joto , kiasi cha tani 5 – 10 huweza kupatikana katika hakta moja kwa msimu

MAKADIRIO
HEKARI MOJA HUWEZA KUINGIZA MIMEA 670.
KILA MMEA UNAWEZA KUTOA HADI KG 30
KG MOJA HUUZWA KWA BEI YA CHINI Tsh700
HII INAMAANA MKULIMA ANAWEZA KUPATA 670 MIMEA x 30kgs x Tsh700 = Tsh (14,070,000) KWA EKARI KWA MWAKA MMOJA
.
NB: HAYO NI MAKADIRIO MEZANI MATOKEO YA SHAMBANI YATATEGEMEA SANA UFANISI WAKO KATIKA KULIHUDUMIA SHAMBA

KWA MAONI AU USHAURI TUNAKARIBISHA MAWAZO YA WADAU WENGINE

Source: smart ideas
MUHTASARI WA KILIMO CHA PASSION

View attachment 345223

Ni mimea inyotambaa na kuhimili hali nyingi za hewa (sio ukame) mme huu hustawi zaidi ukanda usio na baridi wastani wa 20c – 30c na kiasi cha mvua 1500mm za ujazo kwa Mwaka, tunda huwa na ukubwa wa sentimeta 10 kwa kipenyo na uzito gramu 90, kuna aina kadhaa za matunda haya lakini yale ya kijani/manjano hustawi zaidi ukanda wa pwani na yale yenye wekundu Fulani hustawi zaidi maeneo ya misitu, hupendelea udongo wa kichanga wenye mbolea na usiotuamisha maji, pia udongo usiwe na chumvi nyingi na pia kusiwe na mwamba chini kasi cha mita moja tu.

UPANDAJI
Mbegu zipandwe kwanza kwenye mifuko ya plastiki yenye udongo wenye rutuba ya kutosha , kiasi cha Mbegu 3 kwa kila mfuko na mara zinapoota mimea ikingwe na jua kali na ikifikia urefu wa sentimeta 30, huweza kuhamishiwa shambani
Kwenye shamba lako hakikisha kuna nguzo zenye waya mmoja kwa ajili ya mimea kutambaa juu yake, sehemu ya juu baada ya nguzo kuzikwa chini ibakie kama mita mbili na kati ya msatari na mstari iwe ni mita 2 (ukanda wa pwani ) na mita 3 ukanda wa juu kiasi, na umbali kati ya nguzo na nguzo kwenye mstari ni mita 6, na mimea ipandwe umbali wa mita 3 kati ya nguzo na nguzo kufuata mstari.

UANGALIZI
MBOLEA
Mbolea za viwandani ziwekwe kutokana na hali ya udongo, muone afisa ugani kilimo ili afanye vipimo kujua mahitaji na upungufu wa udongo,

MAGONJWA WADUDU
Wadudu kama chawa wa mimea na mchwa wekundu ndio adui wa makakara, pia fangasi husshambulia sana maua ya makakara. Dawa za jamii ya kopa zitumike mara dalili za magonjwa au wadudu kuonekana, kiasi cha kilo 2.8 – 3 hutosha kwa hekta moja au gramu 225 kwa ajili ya dumu moja la lita 20

MAGUGU
Makakara yanatakiwa yawe kwenye shamba safi lisilo na majani na magugu, jembe la Mkono au madawa kama ROUND-UP na GRAMOXONE ynaweza kutumika mimea ikishaefuka na kuwa juu kwenye waya

KUFUNDISHA MIMEA
Ni lazima kuyafundisha matawi mawili ya kwanza kwa kuyaelekeza kutambaa kwenye waya kila moja likielekea upande wake na matawi yatakayoota kutokana na matawi makuu nayo yaelekezwe juu kwenye waya yakifikia ukubwa wa sentimeta 30 – 40

KUPUNGUZA MATAWI
Silazima kupunguza matawi kwa sababu mmea mkubwa zaidi ndio hutoa matunda mengi zaidi, labda kama kuna matatizo katika uchumaji ndio unaweza kupunguza baadhi ya matawi kiasi.

UVUNAJI
Uvunaji huanza baada ya miezi 8 – 9 baada yam mea kupandwa na matunda hukusanywa baada ya kudondoka yenyewe chini baada ya kuiva kila baada ya wiki moja, matunda yahifadhiwe sehemu kavu na isiyo na joto , kiasi cha tani 5 – 10 huweza kupatikana katika hakta moja kwa msimu.

KILIMO CHA MATUNDA YA PASHENI (KARAKARA)

Habari ndugu msomaji wa makala zangu za kilimo cha mazao mbalimbali kupitia mtandao wetu wa kilimo for life. Leo napenda kuelezea fursa ya kilimo cha kisasa cha zao la matunda ya pasheni au pesheni au karakara nchini Tanzania.

Kilimo cha matunda ya Pasheni ni mojawapo ya fursa muhimu, nzuri na rahisi kwa uhakika wa kukuingizia kipato wewe mkulima kwa kipindi kirefu, hii ni kutokana na ukweli kuwa soko la pasheni ndani na nje ya nchi linakuwa kwa kasi kutokana na uhitaji na faida za tunda lenyewe na pia Juisi yake katka mwili wa binadamu.

UTANGULIZI.
Karakara/Pasheni au Passion fruit, kitaalamu Passiflora edulis ni mmea jamii ya miti ya matunda wenye tabia ya:
  • kutambaa, kujiviringisha.
  • Unakua katika maeneo ya tropiki na nusu-tropiki
  • unazaa matunda ya ukubwa wa yai.
  • Matunda yana rani ya Njano au Zambarau yenye kunukia vizuri.
HALI YA HEWA
  • Karakara hustawi katika usawa wa bahari mpaka mita 2000 .
  • Hustawi vizuri katika wastani wa nyuzi joto 23-27 sentidredi
  • kiwango cha wastani cha mvua ni 800 mm hadi 1700 mm
  • pH ya Udongo ni 5.5 -6.5 na udongo mzuri ni wa mchanganyiko kichanga na kifinyanzi (tifutifu)
AINA ZA PASHENI/KARAKARA.
Kuna aina kuu 2 za Karakara ambazo ni Njano na Zambarau.
Matunda huwa kijani yawapo machanga na hubadilika yanapozidi ku.

Aina ya Njano

Huwa na matunda makubwa zaidi na mashina yake ni makubwa zaidi.

Aina ya Njano hupendelea na hukua vizuri katika maeneo ya mwinuko wa chini na joto (tropiki) .

huanza kuzaa miezi 12 baada ya kupandwa na huzaa kwa wingi sana. Matunda ya Pesheni hukomaa na kuiva siku 80 baada ya Ua kuchavushwa.

Aina ya Zambarau

Matunda huwa madogo zaidi yenye uchachu kidogo, utamu, juisi nyingi na hunukia Vizuri zaidi.

Aina ya Zambarau hupendelea mwinuko kiasi mpaka wa juu takribani mita 2000 na hali ya baridi kiasi.

Aina ya Zambarau hukua haraka na huzaa miezi 7 mpaka 9 mara baada ya kupandwa.

Aina hii huwa na vipindi viwili vya mavuno ya juu kwa mwaka hasa miezi ya Julai na Januari.

UPANDAJI NA MPANGILIO WA SHAMBA:
Panda mbegu katika tuta lililoandaliwa vizuri au kwenye viriba/mifuko iliyojazwa udongo uliochanganywa na mchanga kidogo na mbolea ya samadi. Mbegu huota na kuchipua wiki 2 mpaka 3 baada ya kupandwa. Mbegu zilizohifadhiwa muda mrefu huchelewa kuota na uotaji wake huwa wa chini.

Miche hupandikizwa shambani ikifikia kimo cha sentimita 25 hadi 30.
Chimba Mashimo yenye ukubwa wa sentimita 30 hadi 45 urefu, upana na kimo,.

NAFASI (SPACING)

Achanisha nafasi ya mita 3 baina ya mmea katika mstari na mita 1.8 hadi 2 baina ya mstari na mstari.

Panda miche katika mashimo yenye udongo uliochanganywa na samadi au mboji vizuri.

kuongeza mbolea ya chumvichumvi ya kupandia na kukuzia ni bora zaidi.

STAKING

Tumia nguzo urefu wa wastani mita 1.5 hadi 2 juu ya ardhi kufuata mistari zikipishana mita 6 mpaka 9 na unganisha kwa waya au kamba imara. Nguzo zaweza kuwa za chuma au mti kulingana na uwezo wa mkulima mwenyewe.

Miche inaporefuka ielekeze vizuri kwa kuishikiza au kuiviringisha kuelekea juu kuushika waya/kamba ya juu ili itambae juu yake vizuri.

KUVUNA
Karakara huwa tayari kuvunwa pindi linapobadilika rangi kwenda kwenye umanjano halisia au rangi ya zambarau ambapo kikonyo hukauka na Matunda yaliyokomaa na kuiva huanguka chini yenyewe.

Mavuno kwa mwaka katika shamba lililotunzwa vizuri huwa kati ya tani 9 mpaka 15 kwa hekta, hivyo kwa nusu hekta (mita 50 urefu kwa 50 upana) utapata kati ya tani 4.5 mpaka 7.5.

Muda wa Kuhifadhi rafuni (shelf life):
Matunda yanaweza kuhifadhiwa vizuri katika sehemu yenye kivuli, hewa inayozunguka vizuri na joto la kawaida kwa wiki 1 mpaka 2, waweza pia kuhifadhi kwa wiki 4 mpaka 5 katika nyuzi joto 7, ila zingatia baridi ikizidi sana yaweza kusababisha mashambulio ya fangasi.

FAIDA ZA KARAKARA
  • Mbegu zake hutoa mafuta (23%) yanayofanania na ya Alizeti.
  • Majani yake hutumiwa sehemu mbalimbali kama dawa kupunguza shinikizo la damu, kansa na kadhalika.
  • Maua yake hutumika kutibu mfumo wa akili, mapafu, asthma na kadhalika.
  • Ni chanzo kikubwa cha vitamin C, madini ya chuma na virutubisho vinginevyo.
  • Juisi yake ni moja ya viburudisho maarufu na bora sana hasa kwa ladha yake na kunukia kwake vizuri.
Chanzo: Kilimoforlife.com
 
Habari zenu wakuu,

mimi ni mjasiliamali ninayechipukia kwenye kilimo, naombeni kama kuna mtu mwenye utaalam au information kuhusu kilimo cha passion fruits anisaidie kuweka hapa jamvini.

Natarajia kuanza kilimo ichi mwishoni mwa mwaka maeneo ya pwani kwani nimeona demand yake ni kubwa kiasi fulani hapa dsm.

Mkuu LAT niliona mahali umegusia na ukaelekeza kwenye jukwaa la SACCOS ambalo sina access, tafadhali weka hapa jamvini tufaidike na wengine.

Natanguliza shukrani.
 
Dah kumbe na wewe ulitafuta info hapa!

Je, ulishafanikiwa? If yes please help

Hivi matunda haya yanaweza kulimwa ktk ukanda huu pwani?

Mwenye ujuzi atusaidie
 
Ndugu zangu naomba maelezo kuhusu kilimo cha passion yani namaanisha gharama zake kwa heka moja,masoko yake na ushauri mwingine unaolingana, je KINALIPA?
 
Kaka asante.

Nimeiangalio video yote lakini sijaona kwenye masuala ya masoko, yaani naamisha bei. Halafu pia hawajasema gharama za uandaaji wa shamba(miche kiasi gani inahitajika kwa heka moja na vitu vinavyolingana na pia ingependeza zaidi ningepata information za hapahapa Kwetu Tanzania.
 
Kaka dfocus nimeingia hiyo site crops and cultivation nimehangaika sijaona link ya passions,sa sijui nafanyaje?
 
Kaka muisrael mtoto wa yakobo asante hiyo link imekaaa sawa,asante nimepata pa kuanzia sasa.
 
Najua kenya KARI wanao miche aina mpya lakini Tanzania kuna shamba ya serikali inauzaga miche ya matunda korogwe mpigie kesho, kama hana mwambie akuelekeze. 0683 674 348 mwaipopo.
 
Msaada wa kitaalamu kutoka kwa wanajamii forum wenye uzoefu na kilimo cha zao hili la passion fruits.
 
However the purple is quite sweet if u compare with the yellow tofauti yellow ni kubwa kuliko purple.
 
Naandika hapa nikiamini kwamba kuna wataalamu na wajuvyi wa mambo mbali mbali.

Je, ni wapi nitapata matunda ya passion kwa bei rahisi yakiwa bado yako fresh?

Naomba msaada.
 
Meaeneo mengi ya Mkuranga.

Pia kuna passion nyeusi za Iringa zile zinakaa zaidi ya mwezi haziozi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom