Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilimo cha Mpunga

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Kingdom_man, Jan 27, 2013.

 1. Kingdom_man

  Kingdom_man JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2013
  Joined: May 19, 2010
  Messages: 523
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Salaam wadau
  Nimepata wazo na hulka ya kujikita katika kilimo nafikiria zaidi ukulima wa Mpunga kwa kukodi shamba kulima na kuuza mazao. Sasa naombeni wataalamu au wazoefu mnifamishe ni eneo gani nzuri lenye rutuba kwa kilimo cha Mpunga na kwa kukodi ni bei gani kwa hekari?!. Sijawi kufanya biashara hii ya kilimo. Naomba unaambie risks za kilimo cha mpunga. Na faida Mfano gunia ni bei gani?!.

  Nipo kibiashara zaidi kama mpunga ni usumbufu basi Naomba pia ushauri ni mazao gani yatalipa na time interval ya kupata faida?!

  Tusaidiane jamani.
   
 2. Kingdom_man

  Kingdom_man JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2013
  Joined: May 19, 2010
  Messages: 523
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wadau naombeni msaada!. Mbona kimya????....
   
 3. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2013
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,332
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 38
  Mkuu mbona umeshachelewa kufanya hiki kilimo cha mpunga?
  Maana Hata shamba la kulima bado hujapata, watu wameshapanda muda mrefu huko mashambani na mpunga umeota tayari.
  Mimi nafikiria fanya kilimo kingine achana na mpunga muda huu mwaka ujao andaa shamba mapema kabla ya Decemba utavuna vizuri mpunga.

  NB: Waweza kufanya kilimo kingine cha mahindi, alizeti, n.k. au zao lingine lolote kutokana na eneo utakalopata.
   
 4. Mu-Israeli

  Mu-Israeli JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2013
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 2,339
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 38
  Wewe uko mkoa gani ?
   
 5. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2013
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 4,892
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 48
  Jipange msimu ujao wa kilimo
   
 6. Mu-Israeli

  Mu-Israeli JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2013
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 2,339
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 38
  Kama anataka kulima mpunga mkoa wa pwani, na akapata shamba la kukodi mwezi huu wa January, anaweza kuwahi msimu wa mvua.
  Akipaia shamba na akaliandaa shamba vizuri ndani ya mwezi February, atawahi mvua zinazoanza mwezi March (mkoa wa pwani).
  Ila inabidi afanye haraka sana vinginevyo atalima shamba dogo kwa ajili ya muda wa maandalizi kuwa mfupi sana.
   
 7. Kingdom_man

  Kingdom_man JF-Expert Member

  #7
  Jan 30, 2013
  Joined: May 19, 2010
  Messages: 523
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Asante mdau. Kwahiyo nikikomaa na kilimo cha mpunga naweza pata pesa ya ya kujikimu sio?
  Zaidi ya pwani mkoa gani mwingine naweza pata kwamba la kukodi kwa being raisi.
  Asante sana!
   
 8. Kingdom_man

  Kingdom_man JF-Expert Member

  #8
  Jan 30, 2013
  Joined: May 19, 2010
  Messages: 523
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Najipanga. Ndio maana nafanya tafiti. Wataamu mnipe mwelekeo!.
  Asante
   
 9. Kingdom_man

  Kingdom_man JF-Expert Member

  #9
  Jan 30, 2013
  Joined: May 19, 2010
  Messages: 523
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kilimo gani kingine kinalipa zaidi ya mpunga AU bora nisumbirie mwakani?!

  Asante Evarm
   
 10. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #10
  Jan 30, 2013
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,003
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 63
  Mchele wa Kyela....the best in africa.
   
 11. Kubota

  Kubota JF-Expert Member

  #11
  Jan 30, 2013
  Joined: Oct 21, 2012
  Messages: 523
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 28
  Ndugu yangu Robbinhood Kilimo cha mpunga kitakachokuinua ni kile cha kwenye maeneo yenye umwagiliaji. Huko ukishamailiza kupandikiza mpunga wako hesabu hiyo ni hela au ni chakula tayari! Achana na kilimo cha kutegemea mvua utalia siku zote! Mkoa wa Morogoro kuna maeneo kupanda na kuvuna ni mwaka mzima, hakuna eti umechelewa msimu, watu wanapanda tu mwaka mzima. Wanaoongelea kuchelewa msimu ni kwa kilimo cha kutegemea mvua. Mashamba ya kukodi ni mengi na bei ni nzuri tu. Kuna maeneo si utani, bei ya kukodi na ya kununua hakuna tofauti, tembea ujionee!
   
 12. Kubota

  Kubota JF-Expert Member

  #12
  Jan 30, 2013
  Joined: Oct 21, 2012
  Messages: 523
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 28
  Robbinhood, kilimo cha mpunga wa umwagiliaji ni cha uhakika. Risk zake ni pale serikali inapozuia uuzaji mchele nchi za nje, hapo bei hudoda kabisa! Risk nyingine ni kulima eneo lenye mkondo wa mafuriko, huko watu hupata hasara! Na risk nyingine ni ndege na panya kuna misimu hutokea mlipuko wa hao viumbe ambapo wakulima hukimbia mashamba. Ndege wakiwa wengi hata watu 3 kwa ekari moja huweza kutoka povu mdomoni kwa kukimbia huku na kule kufukuza ndege! Ukilima kiangazi peke yako kwa umwagiliaji maeneo yenye wafugaji wa Kimasai jua unawatayarishia malisho! Watakuja kuingiza mifugo yao mchana kweupe na mwenyewe ukishuhudia kwa macho yako! Chezea masai wewe!!??

  Mpunga unafaida kubwa hasa ukiangalia bei ya mchele sokoni hivi sasa, ukistawisha ipasavyo kwenye mashamba ya umwagiliaji kwa kufuata maelekezo ya wataalamu unapaswa upate kuanzia gunia 25 kwa ekari moja! Kila gunia ukikoboa ukapata kilo 70 za mchele ukauza bei ya jumla 1500/= wakati wa uhaba, ekari moja unapata sh 2.6 Millioni! Gharama ya kutunza shamba hadi kuingiza nyumbani Dakawa Morogoro ilikuwa sh 550,000/= mwaka 2011! Sijui msimu uliopita hali ilikuwaje! Kwa hiyo utaona faida ni kubwa tu hasa ukilima eneo kubwa!! Wengi tunafahamu kuwa mchele umekuwa ukiuzwa sokoni rejareja kwa bei kubwa tu! Inawezekana kabisa kuvuna hata zaidi ya magunia 35 kwa ekari iwapo utaalamu utatumika na kutambua misimu yenye mavuno makubwa! Wakulima wazoefu kutoka maeneo ya umwagiliaji watakubaliana kabisa na maelezo haya!!! Hii siyo hadithi ya machungwa 4,000 kwa mchungwa wa miaka 3 nooo!!! It is real!!
   
 13. asigwa

  asigwa JF-Expert Member

  #13
  Jan 30, 2013
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 10,131
  Likes Received: 3,657
  Trophy Points: 113
  Mkuu japo suala la bei na risk siwezi kuongele chochote ila maeneo mazuri kwa kilimo cha mpunga ni IFAKARA ukiwa unaelekea wilaya ya MAHENGE ukishavuka tu mto kilombero kuna eneo wenyeji wanaliita mashambani...
  Ni eneo zuri sana kwa mpunga na linakubali mpunga kweli kweli, pia kuna ardhi ya kutosha na maji ya kutosha pia, kwa suala la soko la bidhaa ni rahisi sana kusafirisha kuja DAR ES SALAAM....
   
 14. Kingdom_man

  Kingdom_man JF-Expert Member

  #14
  Feb 1, 2013
  Joined: May 19, 2010
  Messages: 523
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Aise asante sana mdau. Nashukuru kwa kunipa mwangaza. Naona hii ni idea Nzuri na sio ya kubahatisha. Ntakutafuta tuongee zaidi
   
 15. Kingdom_man

  Kingdom_man JF-Expert Member

  #15
  Feb 1, 2013
  Joined: May 19, 2010
  Messages: 523
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  .
  Sawasawa kamanda. Kwahiyo unanishauri nikajikite morogorokuliko kwenda mbeya AU mkoa mwingine sio?!. Ubarikiwe sana
   
 16. Kingdom_man

  Kingdom_man JF-Expert Member

  #16
  Feb 1, 2013
  Joined: May 19, 2010
  Messages: 523
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Asigwa. Nashukuru sana kwa USHAURI wako. Shukrani
   
 17. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #17
  Apr 1, 2014
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,488
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 63
  Mkuu Kingdom_man nipe update je ulienda kulima?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. i

  ismail yunus Member

  #18
  Jul 3, 2014
  Joined: Nov 23, 2013
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  habari yako mkuu kama wewe una mazao ya kulima ya maharage alizeti mpunga naomba tuwasiiliane number 0768385006 nitakuwa nachukua mzigo kwakoo
   
 19. Mwamba028

  Mwamba028 JF-Expert Member

  #19
  Jul 3, 2014
  Joined: Nov 15, 2013
  Messages: 1,977
  Likes Received: 201
  Trophy Points: 63
  alizeti unanunua kwa sh ngap? Na uko wp
   
 20. i

  ismail yunus Member

  #20
  Jul 3, 2014
  Joined: Nov 23, 2013
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mwamba naomba tuwasiliane katika simu number yangu 0768385006 au tigo 0718116360 please
   

Share This Page