i pad3
JF-Expert Member
- Mar 16, 2012
- 1,518
- 378
tukiweka siasa na udini pembeni hili ni wazo zuri sana ambalo linatekelezeka.viongozi kazi kwenu
Leo asubuhi BBC katika dira ya dunia imetangaza kuwa serikali ya Kenya itaanza kutoa KSh. 2,000/= sawa na USD 25 kwa raia wake wote maskini wanaoishi chini ya KSH. 50/= kwa siku. Zoezi hili lilikwisha fanyiwa majaribio katika miji mikuu ya Nairobi na Kisumu. Sasa zoezi hili litaendelezwa katika miji mingine kama Mombasa. Fedha zitatumwa kwa kila mkenya aliyeorodheshwa kama maskini kwa kutumia M- Pesa.
Hivi karibuni Pro. Lipumba aliporejea kutoka Marekani alisema ni vema serikali ikamfungulia kila mwananchi akaunti benki ili iweze kumgawia kila mmoja wetu sehemu ya pato la Taifa inayotokana na mali asili zetu. Na akasema hii itawapa watu motisha ya kulinda mali asili na kuhakikisha hakuna hujuma yo yote.
Je kama serikali ya Kenya imeanza na kuonyesha mfano Tanzania ni nini kutakachotuzuia kufanya kama Kenya? Tafakari!