ATTENTION!
Medical research authority of the US have found new cancer in human being caused by silver nitro oxide.
Whenever you buy recharge cards dont scratch with nails as it contains
silver nitro oxide coating and can cause skin cancer.
Share this msg with your loved ones.
---
Naye Bata batani mwaka 2012 aliuliza:
Medical research authority of the US have found new cancer in human being caused by silver nitro oxide.
Whenever you buy recharge cards dont scratch with nails as it contains
silver nitro oxide coating and can cause skin cancer.
Share this msg with your loved ones.
---
Naye Bata batani mwaka 2012 aliuliza:
Jamani hapo jana nilitumiwa sms hii kwenye simu yangu na inasema hivi:
"Tahadhari marekani wamegundua ugonjwa mpya wa kansa unapatikana kwa mwanadamu unaosabishwaa na SILVER NITRO OXIDE ambayo inatoka kwenye unga wa vocha kwa hiyo hakikisha unaponunua vocha unapokwangua vocha na kucha unga ule wa vocha usikuangukie kwani unasabisha kansa ya ngozi tuma sms hii kwa watu wengine"
Je kuna ukweli wowote juu la hiliii maana sms hii imesambaaa kwa watu wengi
- Tunachokijua
- Tangu mwaka 2011 kulikuwa na ujumbe uliokuwa unasambaa mitandaoni hasa FaceBook na WhatsApp ukitahadharisha tabia ya watu kukwangua vocha kwa kutumia kucha zao kwa madai zina kemikali inayoitwa Silver Nitro Oxide inayoweza wasababishia kupata kansa ya ngozi. Ujumbe huo unaeleza kuwa Madaktari Marekani wamebaini kuwa vocha ina kemikali ya Silver Nitro Oxide inayosababisha kansa ya ngozi.
JamiiCheck imefatilia vyanzo mbalimbali na kubaini kuwa kwamba ujumbe huo ulianza kusambaa mitandaoni mwishoni mwa mwaka 2011 na kusambaa zaidi kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2012 na kuendelea baada ya kuanza kuchapishwa na kutafitiwa na kurasa mbalimbali.
Aidha, JamiiCheck pia imebaini kuwa baada ya Ujumbe huu kusambaa mashirika mbalimbali ya uhakiki wa habari yakiwamo AFP, The New India Express, Consumerizim, 211 Check, ambao wamefanya uchunguzi na kubaini kuwa madai hayo hayana ukweli. Katika uchunguzi wao wote wamebaini kuwa hakuna kemikali ya Silver Nitro Oxide katika kadi za vocha kama ujumbe huo unavyodai.
Mathalani, katika uchunguzi wa AFP wanaeleza kuwa
Madai kuhusu kuwapo kwa aina mpya ya kansa ni ya uwongo; wataalam waliwaambia AFP Fact Check kupitia barua pepe Juni 13, 2020 kwamba "Hakuna kemilaki inayoitwa'silver nitro oxide'" msemaji wa Shirika la Ulinzi wa Mazingira la Marekani (EPA).AFP Fact Check ilifanya utafutaji wa rekodi katika database ya Wakala wa Kimataifa wa Utafiti juu ya Kansa (IARC), shirika la serikali linaloendeshwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linaloratibu utafiti kuhusu visababishi vya kansa lakini katika orodha yake hiyo hakuna kemikali ya Silver Nitro Oxide inayotajwa. Nao, 211 Check hawatofautiani na AFP ambao katika uchunguzi wao pia wamebaini kuwa hakuna kemikali inayoitwa Silver Nitro Oxide ambapo wao wamefanya utafiti wao kwa kuwahusisha wataalamu wa kutengeneza madawa na kemikali PubChem na ChemSpider ambao pia wanafafanua kuwa hakuna kemikali yoyote inayoitwa Silver Nitro Oxide.
JamiiCheck pia imepitia ukurasa wa Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (CDC) ambao wao wanaeleza kuwa Kansa ya ngozi inasababishwa zaidi na miale ya jua na vyanzo vingine lakini haijataja kabisa kuhusu kemikali ya Silver Nito Oxide.
Hivyo kutokana na hoja na tafiti hizo JamiiCheck inakubali kwamba hoja inayodai kukwangua vocha kwa kucha kunaweza kusababisha kansa haina ukweli.