Sanctus Mtsimbe
R I P
- Jul 14, 2008
- 1,820
- 1,031
- Thread starter
- #61
Du nilimsahau super koplo Thomas wa mafinga JKT
Mkuu, nasikia kulikuwa na adhabu za kuoga maji ya baridi asubuhi huko kwenye mifereji. Ni kweli?
Du nilimsahau super koplo Thomas wa mafinga JKT
Oh, ulikuwa Coy Eagle! Ruvu, au Buhemba? Ruvu: Uliwakuta maafande Lyimo, Medadi, Zuberi, ...? CO alikuwa nani? Maafande wengi wamefariki, akiwemo Dr Omari, adjutant Jalala (km sijakosea jina).
Wakati wa usiku kwenye disco, tukaona kundi la ma Mp linakuja usawa wa kombania. Tukajua, leeo tumepatikana. Wakaongea na kamanda wa kombania, halafu muda si mfupi wakaondoka. Baada ya wao kuondoka,kamanda akasoma majina yetu na kutuita tutoke mbele. Akautuuliza, nyie mlikuwa kwa kuku leo? Tukamuambia ndio. Akasema safi sana, nyie askari wazuri sana, mmekamatwa, lakini mkaweza kutoroka, pamoja na mayai yenu. Huo ndio uaskari. Hatukupewa adhabu, disco likaendelea!
88/89 Nakumbuka Mafinga kulikuwa na bendi ya Kimulimuli na waimbaji mmoja alikuwa amepanga pale JC kwa jina aka Bichuka na mwingine simkumbuki jina alikuwa anapenda kuigiza nyimbo za regae -jerusalem mmojawapo. Mlay akiwa CO na major Miludi we acha tu walikuwa wanaweza kazi ikitokea kuna master parade ya CO.
siku moja Mlay akaja kukagua usafi wa maaskari hasa soski unavua viatu, we volunteers (volvo) walikuwa wachafu jamani! siku nyingine kibao kikawageukia maafande acha warushwe vichura!
Hebrew said:Mmenikumbusha mbali sana.. Mimi nilukuwa Ruvu, halafu Mgulani (kwata la uhuru) halafu Mlalakuwa, miaka ya mwanzoni mwa 1990. Ruvu nilikuwa Fcoy (makondeko) na kina Afande kesi, simba, mohamed na salehe. CO alikuwa ni kanali urio (nasikia ni marehemu). Nakumbuka kulikuwa nafande mmoja alikuwa anaitwa Mizani na alikuwa mpenzi sana wa mabinti (alikuwa anawasubiri vichakani wakati wanatoroka).
Nyimbo ninazokumbuka ni kama !moto wayaka mama ..moto wayaka..wayaka wayaka", Zaina zaina..zainabu wangu usiku silali" na "canadia ee canadian ee.. (nimesahau maneno hapa). Nilifurahi sana jeshini kuliko hata shuleni (boarding).
Du! Mkuu Kitia, hii True Story ni kali saaana. Ama kweli Jeshini wote tulikuwa level moja.
Nakumbuka pia tulikuwa na watoto wa Vigogo wa zamani akina Nyota Kimario (Sijui yuko wapi siku hizi na Binti wa Malima). Wote kwata mtindo moja.
Naona hapa sio mahala pake,tuna matatizo mengi sana kama taifa,tuachaneni na mtindo huu wa kukumbushana yaliyopita kama hayatusaidii.We do not need the past if can not contribute on our future.
Wewe Sikonge wacha uhuni wako!
Katika kombania yetu tulikuwa na wahindi wawili. Siku moja kwenye disco, baada ya wiki kadhaa za kukaa jeshini, mhindi mmoja akawa anatufundisha wimbo wa kihindi. Tulijifunza, lakini yule mwingine akawa anacheka sana,. Sisi tukadhani kuwa maneno ya wimbo ule yanachekesha. Kesho yake ilibainika kuwa yule Mhindi aliyetufundisha ule wimbo ametoroka. Yule mhindi aliyebaki akatuambia alikuwa anacheka sana maana maneno ya wimbo ni: Kwaherini, mimi kesho natoroka!
Wakati wa usiku kwenye disco, tukaona kundi la ma Mp linakuja usawa wa kombania. Tukajua, leeo tumepatikana. Wakaongea na kamanda wa kombania, halafu muda si mfupi wakaondoka. Baada ya wao kuondoka,kamanda akasoma majina yetu na kutuita tutoke mbele. Akautuuliza, nyie mlikuwa kwa kuku leo? Tukamuambia ndio.
Akasema safi sana, nyie askari wazuri sana, mmekamatwa, lakini mkaweza kutoroka, pamoja na mayai yenu. Huo ndio uaskari. Hatukupewa adhabu, disco likaendelea!
Inasemekana siku moja akiwa tayari na cheo chake alikuwa akikagua mahanga toka A Coy hadi mwisho sijui ni Coy gani pale Ruvu ni ya mwisho.