Historia ya Kabila la Wahaya

[h=5]HISTORIA YA KIOBYA
KYA
MIHIGO

Daudi Brett

UTANGULIZI:-

Katika ukoo mzima wa Abarwani nimeamua kuandika historia ya mtu mmoja tu KIOBYA kutokana na umuhimu aliokuwa nao katika uzao mzima wa Mugarula. Hadhi yake ilijengwa na nafasi aliyokuwanayo wakati wa utawala wa Omukama Kahigi II na Omukama kalemera III wa kihanja, nafasi ambayo aliitumia kuuweka ukoo wa Abarwani juu hakuitumia kwa faida yake na familia yake binafsi ndio maana nimesukumwa na dhamira yake nzuri kuandika historia yake.

DAUDI KIOBYA

MAISHA YA KIOBYA

Kiobya Baitwa ni mtoto kati ya watoto 17 wa Mihigo inakisiwa alizaliwa kati ya mwaka 1847 na 1850 alizaliwa katika kitongoji cha Busiko kijiji cha Ruhanga Kamachumu Kianja. Ukoo wake ni wa Abarwani kutoka katika kijiji cha Katembe na Mulongo huko Bugabo. Mama yake aliitwa Kyelesile wa ukoo wa Basimba kutoka katika kijiji cha Busingo Kamachumu Kihanja.

Babu yake aliitwa Kaweshela alihama toka kijiji cha Kizilu Kibale Bugabo pamoja na ndugu zake sita, walihamia Kihanja kutafuta makao mapya walipata ardhi Ruhanga wakalima mashamba Busiko.Baada ya kifo cha Kaweshela shamba lake alipewa jamaa yake aliyeitwa Kikoito na Kikoito alipohama akapewa Jeremia Njaza, sasa anakaa Rooza Mukabaihukya wote ni wa ukoo wa Abarwani.

Kaweshela alipokufa aliacha watoto 14 kabuli lake halijulikani lilipo Mihigo alipokufa aliacha watoto kumi na saba wafuatao:- Kiobya, Itimaa, Kobalyenda na Ntambara Watoto hawa wanne mama yao ni mmoja haijulikani nani wa kwanza kuzaliwa na nani wa mwisho.Tegambwage, Matunu na Kuzara hawa watatu nao mama yao ni mmoja haijulikani wa kwanza nani na wa mwisho nani.Baitira na Kabakenga inaaminika nao mama yao ni mmoja. Watoto waliobaki kila mmoja alikuwa na mama yake wajukuu zake wakubwa kwa umri walikuwa Bajumuzi na Kakana.Mihigo alipokufa alizikwa katika shamba analokaa sasa mwanae Matunu. Matunu hakuwa mrithi wake mrithi alikuwa Ntambara.

Kiobya hakujua kusoma wala kuandika elimu hiyo ilionekana kama elimu ya kigeni iliyoletwa na wazungu ingawa alipenda watoto wake waipate hivyo aliwapeleka watoto wake wote wa kiume shule zama hizo mtoto wa kike alikuwa hafikiriwi kwa lolote la maendeleo hakuna mtoto wake wa kike hata mmoja aliyepelekwa shule.

Kiobya hakuwa mfuasi wa dhehebu lolote la dini kwa maana nyingine hakuwa na dini hata hivyo hakuwazuia watoto wake wa kike na kiume kuwa wafuasi wa dhehebu lolote la dini wapendalo pia sikumbuki kuwepo kwa yeyote miongoni mwa wake zake aliyekuwa mfuasi wa dini yoyote.

Upande wa michezo Kiobya alikuwa mpenzi mkubwa sana wa mchezo wa BAO (Olwesho) wachezaji wenzake wakubwa wakati akiwa Kanazi alikuwa Kataikile Bwohe na Shedrack Kikaibi na alipokuwa Kyanguge alikuwa Rwakitanga Kasigwa na walikuwepo wachezaji wengine wa siku moja moja, bao alilolitumia bado lipo huko Kyanguge hadi sasa.
KUHAMIA KANAZI

Mnamo mwaka 1895 Omukama Kahigi wa II wa Kihanja alihamisha kikale chake toka Bulembo kihanja kwenda kanazi ili aweze kuitawala vizuri sehemu ya nchi aliyomegewa na utawala wa Wadachi toka katika utawala wa Kyamtwara na Bukara Maruku. Miongoni mwa watu aliohama nao ni Kiobya walipokuwa Kanazi alipewa shamba lenye ukubwa wa ekari kumi, baadae akapewa shamba jingine Kyanguge lenye ukubwa wa ekari kumi na mbili na akaifanya Kyanguge kuwa makao yake makuu.

Shamba hili la Kyanguge lilikuwa la Kailembo Byanjweli.Kailembo alihama na kuliacha shamba hili akaamua kurudi kyamtwara alikotoka kwa sababu hakupenda kutawaliwa na Omukama Kahigi. Kailembo Byanjweli alikuwa Omukungu (mtawala wa Kijiji) alifuatana na Omukama Mkotani wa Kyamtwara kwenda Karagwe na baadae Buganda (Uganda) huko ndiko alikokwenda kuomba hifadhi. Kailembo Byanjweli, Kiobya na Mashaija wa Kabale waote ni ukoo mmoja, Kiobya zaidi ya kupewa shamba alipewa Obukungu badala ya Kailembo.

Mnamo mwaka 1897 alipewa shamba jingine Bugera Kanyangereko lenye ukubwa wa ekari 20 na wakati wa utawala wa Omukama Kalemera alipewa shamba jingine la Kasomoro Kanazi lenye ukubwa wa ekari 25. Shamba lake la urithi la Busiko Ruhanga alimpa mwanae Mustafa Nyangasha.Katika kila shamba alilima kilimo cha mazao mchanganyiko kama migomba, mibuni, nk. Ndani ya kila shamba alifuga Ngombe na wakati wote walikuwepo sio chini ya Ngombe wanane waliokuwa wakikamuliwa maziwa, katika shamba la kanazi alijenga nyumba za kisasa zilizojengwa kwa kutumia matofali ya kuchoma, mawe, ziliezekwa kwa bati na zilipigwa rangi kwa kutumia chokaa, pia alifanya hivyo hivyo kwenye shamba la Kyanguge.

KUWA NAIBU (REGENT) WA OMUKAMA
KAHIGI II
Mnamo mwaka 1908 Omukama Ntare VII wa Karagwe aliondolewa madarakani na Wadachi, nchi yake ikawekwa chini ya himaya ya Omukama Kahigi ailinde. Omukama Kahigi II alimteua Kiobya kya Mihigo kwenda kuitawala Karagwe kwa niaba yake. Katika kitabu kiitwacho Tanganyika under German Rule 1905-1912 kilichoandikwa na John IIiffe uk 173 imeandikwa hivi some what later the Germans abandoned their attempt to prop up the ruling house of Karagwe,weakened by succession of child Rulers and natural disaster and installed Kahigis brother in-law KIOBYA as Regent.

Katika kitabu cha historia ya wilaya ya Bukoba kilichoandikwa na Hans Cory ukurasa 126 anasema Ntare alipopata makamo mnamo mwaka 1908 mara moja akaonyesha tabia zilezile za Babu zake Wadachi wakamuondoa Karagwe ikawekwa chini ya utawala wa Kahigi Mukama wa Kihanja ambaye wakati huo alikuwa rafiki na akipendwa sana na Wadachi. Kahigi akamchagua Kiobya Shemeji yake aitawale Karagwe kwa niaba yake.

Omukama Ntare kwanza aliachwa akae Karagwe lakini baadae aliondolewa akapelekwa Kanazi makao makuu ya Omukama Kahigi baada ya vita kuu ya Dunia ya kwanza kutokea alijaribu kuandikiana na waingereza wa Uganda akashitakiwa na Kahigi na Kiobya akanyongwa na Wadachi kwa uasi.Kiobya akaendelea kuitawala karagwe.

Ijapokuwa Kiobya alijitahidi kuitawala Karagwe vizuri yeye kwa kuwa alikuwa mgeni alichukiwa zaidi kuliko watawala wabovu na katili wa jamaa ya haki ya utawala waliomtangulia. Mnamo mwaka 1916 ikawa lazima aondolwe na Daudi Rumanyika mtoto wa Omukama Ntare akapewa mamlaka ya kuitawala karagwe chini ya ulinzi wa Isaac huyu alikuwa Mganda kwa kuwa Daudi alikuwa ni mtoto mdogo wa umri wa miaka 11 na wakati huohuo akapelekwa Uganda kuelimishwa.

Omukama Kahigi II alikufa tarehe 4-9-1916 wakati wa Kifo chake Kiobya alikuwa bado Karagwe alitumiwa ujumbe kumwarifu juu ya kifo cha Omukama akaondoka Karagwe kurudi Kihanja kuhani msiba na tangia hapo hakurudi tena Karagwe. Aliwatuma wanae Mustafa Nyangasha, Ab-Bakari Munema na Anatori Balimunsi kuchukua mali zake na jamaa zake aliokuwa amewaacha huko na utawala wa Wadachi Ukamtawaza rasmi Daudi Rumanyika Kuwa Omukama wa Karagwe.


KILIMO CHA KAHAWA
KARAGWE

Kiobya alikaa Karagwe tangu mwaka 1908 hadi mwaka 1916 makao yake makuu aliyaweka Kishao Bugene, kile kikale cha Omukama Ntare kilikuwa Nyakahanga. Katika utawala wake alipokuwa Karagwe aliwahimiza na kuwasimamia Banyambo kulima kilimo cha Mibuni na Pilipili ili kujiletea maendeleo kwa kuwa kwa wakati huo ndio yalikuwa mazao makuu ya biashara, hadi wakati huu kahawa ilikuwa haijaanza kuvunwa kwa wingi Karagwe, ilikuwepo mibuni michache tu na kwa watu wachache kahawa iliyovunwa ilipikwa na kukaushwa kwa moshi kwa matumizi ya kutafuna tu.

Ili kuonyesha mfano na kuleta mapinduzi katika matumizi ya zao la kahawa Kiobya mwenyewe alilima na kupanda mibuni mingi sana katika shamba lake la Bugene, Banyambo nao wakashawishika wakaanza kupanda mibuni mingi katika mashamba yao. Shamba na nyumba yake ya Bugene vilidumu hadi miaka ya 1960. Mnamo mwaka 1950 vyama vya ushika vya msingi vya ununuzi wa zao la kahawa vilipoanzishwa katika wilaya ya Bukoba nyumba yake ya Bugene ndiyo iliyofanywa ofisi ya kwanza ya chama cha ushirika wa ununuzi wa zao la kahawa (Bugene Native Farmers Co-operative Society Ltd).

Profesa Israel Katoke kwa ajili ya chuki zake za kikabila za Banyambo kwa Kiobya zilizojengwa kwa kuwatawala akiwa mgeni katika kitabu chake cha The Making of Karagwe Kingdom ameandika matusi mengi sana dhidi ya Kiobya lakini hata hivyo historia itabaki palepale kwamba Banyambo maendeleo waliyonayo sasa Karagwe yanatokana na zao la kahawa ambalo Kiobya alihimiza na kusimamia kupandwa kama sio hivyo maendeleo waliyonayo leo wasingekuwa nayo kwa hilo Banyambo wanapaswa kumshukuru na kumkumbuka Kiobya.


SAFARI ZAKE ZA KUTOKA KIHANJA
KWENDA KARAGWE
Katika safari zake zote za kutoka Kanazi Kihanja kwenda Karagwe na kutoka Karagwe kurudi Kihanja zilikuwa ni za kutembea kwa miguu, njia yake kuu aliyopita mara nyingi ilikuwa ni kutoka Kanazi >Ibwera>Nyakigando>Kabirizi>Ndama Lushanje hapa ni mpakani mwa Kihanja na Karagwe anaingia Kikula anafika Bugene. Enzi hizo sehemu kubwa ya njia hii yalikuwa ni mapori yenye aina mbalimbli ya wanyama Simba, Chui, Faru, Tembo, Twiga na wanyama wengineo walikuwa wakipatikana kwenye misitu hiyo.
Msafara wake wakati wa safari zake ulikuwa haupungui chini ya watu 40 na safari ya kwenda au kurudi ilikuwa inachukua kati ya siku tatu hadi nne, wakati wa safari zake Kiobya hakupenda kuipa nchi yake ya Kihanja kisogo hivyo katika safari zake za kutoka kihanja kwenda Karagwe alikaa kwenye machela akitazama alikotokea yaani akiiangalia Kihanja zama hizo wakuu katika utawala katika safari zao walibebwa juu ya machela.

KIOBYA NA UTAWALA WA
OMKUKAMA KALEMERA
Kama tulivyokwishaona huko juu baada ya kifo cha Omukama Kahigi mwanae Benjamin Mtembei ndiye aliyepaswa kurithi kiti cha Baba yake wakati huo alikuwa ni mtoto mdogo wa umri wa miaka 8 wazee wa ukoo wa Omukama walio wengi hawakupendezwa na mtoto mdogo wa umri kama huo kutawala wakaona ni vyema wamtawaze mtoto mkubwa serikali ikawaunga mkono miongoni mwa watoto wakubwa wa Omukama Kahigi akachaguliwa Alfred Rutabingwa kushika mamlaka akatawazwa akaitwa Omukama Kalemera III.

Mama wa Omukama Kalemera aliitwa Kabalyenda ambaye alikuwa ni dada yake Kiobya kwa kutawazwa mwanae yeye akawa Omukama Omukulu akaitwa Kabibi (Mpanzi), kabalyenda alifariki mwaka 1927alifia Ntungamo Muhutwe baada ya kifo chake mtoto wake Kiobya aliyeitwa Evangelina Kiiza akaitwa jina lilelile la Kabibi.

Kiobya katika tawala zote mbili Utawala wa Omukama Kahigi na Utawala wa Omukama Kalemera alikuwa katika baraza la wazee wa kumshauri Omukama ni wakati wa utawala wa Omukama Kalemera Kiobya alijipatia majina ya tambo na majigambo ya “Rwakaijanangoma”, “Rwakaijanante” na “Ituro lya Rumambo”

Abahinda watu wa ukoo wa utawala walimwamkia Kiobya “shumalaamu zama hizo ilikuwa ni mwiko kabisa kwa Muhinda (ukoo wa Omukama) kumwamkia Mwiru (koo za watawaliwa). Kwa upande wa Omukama binafsi Kiobya licha ya kuwa mtawaliwa alikuwa hamwamkii Omukama (kumulamya) kama ilivyokuwa ikifanywa na watawaliwa wengine isipokuwa yeye wakati wa kwenda kumwamkia alimpa chochote ambacho angekuwa ameshika mkononi kati ya Fimbo, Muhoro au Mkuki na Omukama alikigusa kitu hicho kama ishara ya kukubali salamu hiyo. Kwa mujibu wa mila Omukama hamwamkii mtu yeyote isipokuwa mama yake mzazi tu.

KIFO CHAKE
“Narudi Kyanguge lakini sijui kama nitakuja Kanazi tena.”Haya ni maneno aliyoyatamka Kiobya wakati akiwaaga ndugu, jamaa na marafiki zake wa kanazi wakati akitoka huko kurudi nyumbani kwake Kyanguge. Kanazi palikuwa mahali pa “Ikulatiro” alikaa kwa muda tu alipokwenda kumtembelea Omukama au kama Omukama alimuhitaji. Hakuwa na mke yoyote aliyekaa kanazi isipokuwa alikuwa akienda na baadhi ya wake zake ambao waliungana na wake wenzao ambao walikuwa wanakaa Kanazi Kasomoro.

Wakati akitoka Kanazi Kurudi Kyanguge akikaribia kufika katika uga wa nyumba yake alikuwa akipiga risasi moja hewani ishara ya kuwaarifu ndugu, jamaa na marafiki zake kwamba alikuwa amerudi nyumbani kutoka kanazi, na huku nyumbani nako alijibiwa kwa kupigwa ngoma yake iliyoitwa “katonda” aliyekuwa akipiga ngoma hii alikuwa anaitwa Kasamitara Kyangura wakati anapiga ngoma hii alikuwa anatamka maneno yafuatayo “Ekiita ni Katonda” na waliobaki wanabwagiza “Omukama ni Rugaju” baada ya hapo ilipigwa panda aliyekuwa akipiga panda alikuwa anaitwa Banyeza baba yake Simioni Myaka.

Baada ya siku mbili tangu atoke Kanazi aliugua na siku ya tatu kama alivyojitabiria mwenyewe akafariki dunia ilikuwa tarehe 18-1-1935 majira ya kama saa sita hivi usiku. Mtu muhimu katika ukoo wa Abarwani akawa ameiaga dunia akiwa amezungukwa na ndugu jamaa na marafiki zake. Waliokuwemo ndani ya chumba chake wakati huo ni wake zake Mukasheruzi, Nagayo, Mukafumu, Nagayo Anna, Tibyakushemera, Mukabahaya na Tibashemelelwa. Nduguye aliyekuwepo ni Omwani Nyamaishwa pia walikuwemo wanae Mustafa Nyangasha,Coroneli Bushongore na Willbard Kwelengera katika chumba jirani walikuwemo wanae Tryphone Samson, Daud Brett, Ferdinand silingi, Esteria Mukatesi, Nyangoma, Mathias Balingilaki na Feliciani Binamungu, sebuleni huko kulijaa watu wengi sana. ambao siwezi hata kuwakumbuka.

Manamo tarehe 20-1-1935 majira ya saa 10 jioni Kiobya akazikwa katika kaburi lililochimbwa ndani ya nyumba katika moja ya vyumba vya nyumba yake ya Kyanguge japo ametutoka jina lake limebaki na litaendelea kuwepo kwa vizazi na vizazi. Mungu amrehemu amfutie madhambi yake na ampuzishe kwa amani AMIN.

URITIHI
Mnamo tarehe 21.1.1935 siku moja baada ya mazishi ya Kiobya Omukama Kalemera alituma ujumbe Kyanguge kwa ukoo wa Ambarwani kuwaomba waahirishe zoezi la kumrithisha mtoto atakaye chukua kiti chake mpaka hapo baadaye, kwa mila na desturi za Bahaya siku mbili baada ya mazishi ya marehemu mtoto atakayemrithi na kuwa kiongozi wa familia hukalia kiti cha marehemu.

Kufuatia ombi la Omukama Kalemera utaratibu wa kumsimika kwenye kiti mrithi wa Kiobya ulisimamishwa na aliyepasawa kumrithi alikuwa ni mwanae Koroneli Bushongore na dada yake katika urithi alipaswa kuwa Esteria Mukatesi maana hao ndio walioosha mwili wa marehemu “kugabura”.

Baada ya wiki mbili Omukama Kalemera alituma ujumbe wa pili Kyanguge kwa ukoo wa Abarwani ukiwa na pendekezo la Omukama la kuwaomba kumsimika Petro Tibaijuka kuwa mrithi wa kiobya badala ya Koroneli Bushongero. Barwani waliridhia haja ya Omukama zoezi la urithi lililokuwa limesimama likaendelea Petro Tibaijuka akasimikwa kwenye kiti akawa mritihi kiongozi wa familia na dada yake katika urithi akawa Nyangoma.

Petro Tibaijuka alikuwa anafanya kazi Mwanza alifika Kyanguge siku tano baada ya mazishi ya baba yake.Watoto wa kiume ambao hawakuwa na mashamba walilirithishwa mashamba, na kila mtoto wa kiume alipewa “Batwarwa wa Nyarubanja” kulingana na uwiano wa umri wa kuzaliwa walipewa fedha na ng’ombe kwa kufuata uwiano huohuo. Watoto wote wa kike kila mmoja aliwekwa chini ya uangalizi wa mtoto wa kiume wa kumlinda kwa mila za Bahaya watoto wa kike hawawezi kurithi mashamba. Baada ya miezi sita Banyaruganda walivunja Matanga na kusambaa kuendelea na maisha ya kawaida (kushohora)

Sababu za Omukama Kalemera kumpedekeza Petro Tibaijuka kuwa mrithi wa kiobya ni kwa kuwa alikuwa msomi akijua kiingereza vizuri na akifanya kazi bomani Mwanza kama karani mkuu chini ya District Officer (D.C) sifa ambazo Omukama aliziona zina manufaa katika utawala wake kwa kuwa zilikuwa zinaendana na wakati.

UZAO WA KIOBYA
Inaaminika Kiobya alizaa watoto zaidi ya mia moja na alioa wanawake wengi kwa idadi kama hiyo au pungufu kidogo ya mia moja, hapa chini ni orodha ya wanae ambao wakati anakufa walikuwa hai pamoja na mama zao.
1. Ab- Bakari Munema
2. Anatoli Balimunsi
3. Alphonce Ndyakohasi
Watoto hawa watatu Mama yao aliitwa Banyangoi wa ukoo wa Abatundu mzaliwa wa Bwigula Kihanja.

1. Koloneri Bushongore
2. Tereza Mukaite
3. Willbard Kwelengera
Watoto hawa watatu Mama yao aliitwa Bagane wa ukoo wa Abayego mzaliwa wa katoke Kihanja.

1. Paskazia Mukabengesi
2. Daudi Brett kilyekaija
3. Esteria Mukatesi
Watoto hawa watatu Mama yao aliitwa Anna Nagayo Bagoka wa ukoo wa Abende mzaliwa wa Bugene Karagwe.

1. Joseph Kandabila
2. Fulgence Tibamanywa
3. Feliciani Binamungu
Watoto hawa watatu Mama yao aliitwa Tibyakushemera wa ukoo wa Abayango mzaliwa wa Ihembe Karagwe.

1. Amina Amulungi
2. Fideli Katto
3. Tadeo Rwiza
Watoto hawa watatu Mama yao aliitwa Mukomutanda wa ukoo wa Abende wa Bugene Karagwe.
1. Stephano Bashaija
2. Angerbert Ambele
Watoto hawa wawili Mama yao aliitwa Bagelize wa ukoo wa Abahuga mzaliwa wa Rwayango Mabira Karagwe.

1. Paulo Katabaro
2. Ferdinand Silingi
Watoto hawa wawili Mama yao aliitwa Mukafumu wa ukoo wa Abayozi mzaliwa wa Itoju Kihanja.

1. Shuzali Ngaiza
2. Gervazi Babili
Watoto hawa wawili Mama yao aliitwa Kalungi Kahigi wa Ukoo wa Bahinda

1. Mustafa Nyangasha
2. Malifedha Kyabago
Watoto hawa wawili Mama yao aliitwa Kagulila

1. Raphael kiboga
2. Jeremid Lukomwa
Watoto hawa wawili Mama yao aliitwa Tereza wa ukoo wa Abasingo

Tryphone Samson: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Mukasheruzi wa
ukoo wa Abatundu mzaliwa wa Karagwe.

Amisa Kwezi: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Lyagwage mzaliwa wa Karagwe

Domitina Tikyakweba: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Kemisingo wa ukoo wa Abashasha mzaliwa wa karagwe.

Paskazia Mukalangira: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Mukabahaya wa ukoo wa Abatundu mzaliwa wa Karagwe.

Maria Kasoli: mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Kyetoba Rwiza wa ukoo wa Abashozi mzaliwa wa Kigarama Rwagati Kihanja.

Hamisi Babu: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Kyantumile wa ukoo wa Abanyuma mzaliwa wa Maruku Bukara.

Yohana Maria Mapenzi: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Kitundila wa ukoo wa Abagaya mzaliwa wa Kyanjoju Kihanja.

Nyangoma: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Kansiga mzaliwa wa Karagwe.

Petro Tibaijuka: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Tinkunilwa wa ukoo wa Abatundu mzaliwa wa Mugaza Kyanguge Kihanja.

Paulina Kabalebe: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Nkubuye mzaliwa wa Rwanda.

Ameria Kamashsmba: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Mpongwa mzaliwa wa mabira Karagwe.

Martina Tibela: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Kaigane wa ukoo wa Abasaizi mzaliwa wa Karagwe.

Evanjelina Kiiza: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Rooza Nyanjala wa ukoo wa Abamiila mzaliwa wa Ankole Rukiga Uganda.

Kashumuni: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Tindyebwa wa ukoo wa Ababango mzaliwa wa Kyanguge Kihanja.

Zelida Mukajuna: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Suzana Kyobendaga wa ukoo wa Abamiilo mzaliwa wa Rukinga Ankole Uganda.

Mathias Balingilaki: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Bashemere wa Ukoo wa Abasaizi mzaliwa wa Ankole Uganda

Fredrick Kabinyagira: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa Nzine mzaliwa wa Karagwe.

Anastazia Tibikinena: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa ......wa ukoo wa Abaihuzi wa Bugera Kanyangereko.

Asmini Bikale: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa ......wa ukoo wa Abaihuzi wa Bugera Kanyangereko.

Shella Kinuzile: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa ......wa ukoo wa Abayango mzaliwa wa Rwazi Kanyangereko.

Tereza Mukagilage: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa ......mzaliwa wa Karagwe.

Mathayo Mushongi: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa ......mzaliwa wa Karagwe.

Mikaili Katabazi: Mtoto wa Kiobya Mama yake aliitwa ......wa Ukoo wa Abazigu mzaliwa wa Karagwe.

Watoto wa Kiobya Rooza Kemilembe na Zainabu Twahilwa sina kumbukubu za wasifu wa Mama zao.
Hadi Kiobya anachukuliwa na umauti aliacha watoto hai 49 ambao nilikuwa ninawafahamu na aliacha wake hai niliokuwa ninawafahamu 40 kati ya wanawake hao arobaini aliokuwa bado anaishi nao ndani ya nyumba yake ni wake nane tu kati ya hawa wake 8 wawili kati yao hakujaaliwa kupata nao watoto, wake hawa wawili ambao hakuzaa nao ni Nagayo Bwikiza na Tibashemerelwa.Wake ambao alikuwa haishi nao ama alikuwa amewaacha au walikuwa wanaishi na watoto wao baada ya “kugungwa” kutoendelea kushirikiana nao kama wake kwa muda mrefu sana.
Mke wa kwanza wa Kiobya kuoa (Kwebohora au Kwoga) alikuwa anaitwa Nobileki ambaye alizaa nae mtoto mmoja tu aliyeitwa Laurent Byakugira mtoto huyu alikufa miezi michache kabla ya kifo cha baba yake alikufa bila kuzaa (Buchweke) pia binti wa kwanza wa kiobya Kyenchwere nae alikufa bila kuzaa (Bugumba).Kati ya wake zake aliyekufa wa Mwisho ni Anna Nagayo Bagoka alikufa tarehe 19 December 1985. Watoto walioko hai hadi ninapoandika kitabu hiki ni kumi na nne tu ambao ni hawa wafuatao:-
1. Willbard Kwerengera
2. Stephano Bashaija
3. Angelbert Ambele
4. Thadeo Rwiza
5. Amina Amulungi
6. Paskazia Mukabengesi
7. Yohanamaria Mapenzi
8. Rooza Milembe
9. Zainabu Twahilwa
10. Anastazia Tibikinena
11. Domitina Tikyakweba
12. Shuzari Ngaiza
13. Feliciani Binamungu
14. Daudi Brett.
(Ninapochapisha kitabu hiki mwaka 2009 kati ya watoto hao kumi na nne wa kiobya wamebaki watoto wawili tu Shuzari Ngaiza na Paskazia Mukabengesi mungu aendelee kuwapa uhai -Mukhsin Kiobya)[/h]

Je wakina Kiobya wa Kati Ibwera naona vipi Mukshin?
 
Hii imetulia sana kyoma,hayo maeneo ya Basiko sahivi kunaitwa Kasiko na ni mlima kwa chini yake ndo panaitwa luhanga alafu pale Bulembo mpaka leo pameendelea kuitwa hivyo na wengi wao wanaitwa umuruganda" Abasimba" ..Sidhani pia kama ni sahihi sana ila kuna kijisehemu kinaitwa Bungezi kuna familia moja ya Bibi aliitwa ma Rooza sasa sijuhi kama ndo mabaki ya yule Rooza mwenyewe ama la

Na pale kanazi kuna himaya na magofu hadi leo sehemu kubwa panaitwa "Akikale kanazi"
Wakola waitu,historia nzuri kabisa hi
 
Nataka kwenye hii topic kuanza kujadili suala hili, wahaya walitoka wapi?Je mila zao na dini yao ya asili ni ipi?Je koo (oluganda) zilianza vipi na ziko ngapi?

Baada ya wahaya nitajadili makabila mengine, labda kuanzia yale ya great lakes, kwa mfano wasukuma, mpaka makabila yote ya Tanzania tutayamaliza.

Mwenye ujuzi wowote anakaribishwa kuchangia.

Kyoma uliweka mada nzuri alafu ukakimbia, oliyo?
 
I think they are bantu and the origin of bantu is the same to all bantu tribes and its not who, what, and which its about the tribal uniformity that has been in existence for centuries and that therefore they dissected themselves immediately after arriving in lake region formally known as intracustrine region so their origin is the same to any bantu tribe in country, maybe if you wish for different views not the originality of the haya. Thanks
 
Jamani kuna kitabu nilikutana nacho simkumbuki mwandishi ila kilikuwa kinaelezea "Buyango koo za Babito toka Mweyanjale, Kafunjo, Ex-gombolola, mpaka Ndwanilo nadhani mpaka leo kuna Magofu. mjuzi tupe mambo!

Ndi mubito na'akagele nintemwa Luganjo
 
Sasa nitaendelea.

Hivi leo ukienda kwenye ekikale au ikulu ya mkama wa kianja Peter Nyarubamba(pale kanazi) , atakuonyesha jinsi dini ya kale ya buhaya ilivyo.Hii dini bado ipo mpaka leo na Nyarubamba ndio mrithi au high priest wadini yetu hii ambayo ilishambuliwa sana na wakoloni ingawa tenents zake ni very aunthentic and spiritual.

Sasa Mukama Nyarubamba kazi yake ni kufanya rituals fulani wakati fulani wa kuonekana kwa mwezi.(sasa unaona similarities na waisilamu ambao wanasherekea sikukuu zao kutokana na kuonekana kwa wakati fulani kwa mwezi-ingawa la hasha wahaya hawakucopy kutoka wa waisilamu ).

Katika sala zake, Mukama, hasahau kuwaomba wahenga hasa Ruhinda mwanzilishi wa koo ya kifalme ya abahinda( ukoo anaotoka mfalme) ambayo ilitawala sehemu kubwa Buhaya. Je huko Bunyoro wahinda waliingiaje kabla ya kutawala buhaya?
Mada nzuri sana hii lakin naona umekimbia mkuu
 
Rejea kanda za "enanga" (kwa mujibu wa jamaa yangu tuliyefanya naye kazi pale Rutabo) ...! Utapata mambo mengi juu ya ndugu zetu hawa.
 
Kiukwel kwa watu waliowai kujaliwa kufika Bukoba .

Hapa nazungumzia maeneo ya vijijin kama bukoba vijijin yaani watu wa kule wanaishi maisha mazuri sana ukilinganisha na mikoa mingine ...yaani uwez kukuta muhaya anakula ugali na maharage au ananyumba ya nyasi...au analima huku mvua inanyesha.

Lakin ukienda mikoa mingine kwa maeneo ya vijijin kama Singida, Tabora ,Dodoma ,Morogoro , Nk
Isee ni hatar sana watu wanamaisha magumu sana.
 
Wahaya gani unawazungumzia mimi uzuli nimekaa sana wahaya

Nipo nao hapa manzese darajani yaani wengi wao wananiambia wanajuta kuzaliwa bukoba kwa sababu kuna hali ngumu ya maisha ndio maana wengiiii wanaona bora waje mjini kupiga biashara ya ngono.

Biashara ambayo wanapanga nyumba nzima wanaigawa katika vyumba huku wakiuzaaa papuchii elfu 2 baoo mojaa pamoja na chumba na pia hata baadhi wanaume wanatoa kwa bei cheeee.

Kama kuna mtu anabisha ajee manzese darajani au aende mwananyamala hospitali au buguruni sokoni au temeke hospitaliii .
 
Kiukwel kwa watu waliowai kujaliwa kufika Bukoba .

Hapa nazungumzia maeneo ya vijijin kama bukoba vijijin yaani watu wa kule wanaishi maisha mazuri sana ukilinganisha na mikoa mingine ...yaani uwez kukuta muhaya anakula ugali na maharage au ananyumba ya nyasi...au analima huku mvua inanyesha.

Lakin ukienda mikoa mingine kwa maeneo ya vijijin kama Singida, Tabora ,Dodoma ,Morogoro , Nk
Isee ni hatar sana watu wanamaisha magumu sana.
Nadhani wewe kichwani una tatizo la wahaya. Unadhani kula nyama kila siku ni maendeleo???? Hivi unadhani kula ugali na maharage ni dalili za umasikini???
 
Kiukwel kwa watu waliowai kujaliwa kufika Bukoba .

Hapa nazungumzia maeneo ya vijijin kama bukoba vijijin yaani watu wa kule wanaishi maisha mazuri sana ukilinganisha na mikoa mingine ...yaani uwez kukuta muhaya anakula ugali na maharage au ananyumba ya nyasi...au analima huku mvua inanyesha.

Lakin ukienda mikoa mingine kwa maeneo ya vijijin kama Singida, Tabora ,Dodoma ,Morogoro , Nk
Isee ni hatar sana watu wanamaisha magumu sana.
Halafu kitu kingine wahaya ninachowashangaa wanapenda sana kusema wanatokea bukoba badala ya kusema wanatokea kagera sijui kwanini hawapendi kulitaja hili neno kagera wao wanang'ang'ania sisi kwetu bukoba.

Kitu kibaya zaidi ukiwambia wakupeleke kwao bukoba unashangaa wengi wanashukia muleba wanaingia vijijini uko mpka unafika bukoba mjini mnajikuta waliobakia wengi ni wamanyema watu tokea congo ndio wenye bukoba yao ila cha kushangaza wahaya walivyo wa ajabu hawezi kukuambia anatokea muleba yeye atakwambia kwao ni bukoba na wanasema hivyo kwa sababu muleba hakuna maendeleooooooo
 
Mimi nipo huku kwao hawana lolote maisha magumu tuu wanajenga nyumba za tope kama watu wa pwani au wanaita mbavu za mbwa.
Nenda Muleba utaona nenda maeneo kama ngenge, kanywangonge au kule milimani wanaita ngote na Kanyerenyere ndo utajua kuwa wanamaisha mazuri au magumu.
Mhaya hali ugali kwa sababu kazoea ndizi (ekitoke). Ugali na wali wameanza kula hivi juzi baada ya mnyauko kukausha ndizi. Ni moja kati ya kabila vivu kupindukia.
Wanaume hawaendi shamba zaidi ya ulevi na wanawake wanaenda shambani saa moja au mbili lakini saa tatu yupo anasugua gaga nje ya nyumba
Kama hujui kaa kimya
 
Wahaya gani unawazungumzia mimi uzuli nimekaa sana wahaya

Nipo nao hapa manzese darajani yaani wengi wao wananiambia wanajuta kuzaliwa bukoba kwa sababu kuna hali ngumu ya maisha ndio maana wengiiii wanaona bora waje mjini kupiga biashara ya ngono.

Biashara ambayo wanapanga nyumba nzima wanaigawa katika vyumba huku wakiuzaaa papuchii elfu 2 baoo mojaa pamoja na chumba na pia hata baadhi wanaume wanatoa kwa bei cheeee.

Kama kuna mtu anabisha ajee manzese darajani au aende mwananyamala hospitali au buguruni sokoni au temeke hospitaliii .
Sasa mkuu wanauziaje papuchi kwenye hospitali? au sijaelewa!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom