Dkt. Wilbert Kleruu - Utata wa kifo chake, historia na maisha yake

@gm,
GM na Wakuu wengine
Pamoja na kwamba hii ni nje ya mada..kuna kitu huwa kinanitatiza... hivi Nyerere ndiye alileta uhuru au "Uhuru" huo was inevitable kuja kipindi kile ( many countries got independence in 1960s ukiachilia mbali Ghana (1957), Guinea (1958) - Chad, Benin, Nigeria, Ivory Coast, Madagascar, Central African Republic, Mali, Niger, Senegal, Burkina Faso, Mauritania, Togo, Zaire, Somalia, Congo, Gabon, Cameroon zote zilipata uhuru in 1960, Tanzania 1961,Algeria, Burundi, Rwanda, Uganda 1962,Kenya 1963, Malawi, Zambia 1964, Gambia 1965,Botswana, Lesotho 1966,Equatorial Guinea, Mauritius, Swaziland 1967...Equatorial Guinea, Mauritius, Swaziland 1968)

Nadhani ilikuwepo a wind of change iliyopelekea wakoloni waondoke ukizingatia kuwa ..it was no longer profitable kunyonya with physical presence. Unyanyaji ulikuwa na faidi zaidi kwa kutoa uhuru wa bendera na kuendelea kunyonya thru ukoloni mamboleo.
Swali.. ni kwanini bado tunaendelea kufagilia sana hili la kuleta uhuru na tusiseme tu kuwa Nyerere ndiye alichukua madaraka kutoka kwa wakoloni na kuasisisi utawala wa waafrika Tanzania huru? na baada ya hapo akaanza ku experiment different things including utopian socialism na ujamaa... sijui ndo
African Socialism... hadi kusababisha maafa ya huyu mkereketwa wa Ujamaa - Dr Kleruu.
 
Sio UJAMAA uliomuua Dr. Kleruu bali tabia na HULKA yake mwenyewe kama kiongozi wa Mkoa. Uongozi ni KIPAJI kwanza, mengine kama vile shule yanauboresha na kupanua uwezo wa kufikiri, kutenda na kufanya maamuzi sahihi kama KIONGOZI.
 
Nijuavyo ni kwamba Lucy Lameck alifariki kutokana na matatizo ya ini.
Nadhani alikuwa anapiga (pombe) kupita kiasi. Nilikutana naye Paris nyumbani kwa balozi Tatu Nuru (rip) yeye alikuwa anapiga brandy kavu kavu.


Mkuu Jasusi umesema ukweli.
Habari ndiyo hiyo! Mengine ni uzushi tu!
 
mwalimu alikuwa anatimiza jukumu la kikatiba la rais wa nchi. maoni ya baadhi wenzetu hapa ni kama vile yeye ndiye alikuwa amehukumu na kisha ametia sahihi watu wanyongwe. kama kuna alioacha kutia sahihi wakati wengine amefanya hivyo, .


presidential prerogative!
 
Mwalimu alikuwa anatimiza jukumu la KIKATIBA la RAIS wa NCHI. Maoni ya baadhi wenzetu hapa ni kama vile yeye ndiye alikuwa amehukumu na kisha ametia sahihi watu wanyongwe. Kama kuna alioacha kutia sahihi wakati wengine amefanya hivyo, pengine hilo ndilo la kuangalia. Mwalimu aliiheshimu sana KATIBA.
Kuhusu vijiji vya ujamaa kwa kweli huu ulikuwa ni UKOMBOZI mkubwa kwa tulio wengi. Tuliweza kupelekwa shule baada kutolewa huko porini tulikokuwa tunaishi, kwa mara ya kwanza tulitibiwa kwenye zahanati; UTANZANIA wetu ulijengeka maradufu; na hadi leo tunaishi kwenye vijiji hivi.

Finally, kuna positive ya Mwalimu maana tumesoma the otherside mpaka tumefika mwisho, ahsante mkuu.
 
Unasema tufuatilie, lakini sijui na wewe mwenyewe umefuatilia kilichoandikwa humu ? Waziri kasema "watu 10 walinyongwa wakati wa awamu ya kwanza." Hakusema kulikuwa kuna hukumu 10. Ina maana siku Nyerere anakabidhi funguo walikuwa tayari wameshanyongwa mtu 10.

Bado ninasisitiza msimamo wangu kua siamini kuwa Mwalimu, alisaini kunyongwa wananchi 10, na hii inatokana na kuisoma article ambapo Mwalimu alisema alisaini kwa mwananchi mmoja tu Mwamwindi, kama alisaini 10 au hakusaini haibadili imani yangu kwamba Mwalimu hakuwa na mkono wa kupenda damu za wananchi,

Sio siri kua policies zake nyingi zilikuwa ni nonesense na zimetupotezea muda mwingi wa-Tanzania wa kusonga mbele, lakini kama ni kuchagua between yeye na hawa Mtandao, I would rather niongozwe na Mwalimu, na pia sio siri kwamba under Mwalimu inaonekana wananchi wengi tulikuwa tumelala usingizi mzito sana,

swali ni je leo tumeamuka?.
 
Field Marshall ES,

Mkuu heshima yako!

Nafikiri FM itabidi uwatafutie wakuu hiyo article uliyoisoma ya Nyerere kusaini death warranty ya mtu mmoja la sivyo naona wataendelea kukukoromea tu na kukushika shati!
 
Field Marshall ES,

Labda swali lingekuwa hivi ni wafungwa wangapi walinyongwa kwa saini ya Mwalimu, Mwinyi, Mkapa na Kikwete. Nadhani hapo tu tungejiuliza kwamba bila saini ya Mwalimu kuna mwingine zaidi maana kwa upande wa Mwalimu yeye alikiri kuwa alisaini kunyongwa kwa mmoja tu. Nadhani tungejua mengi hapa maana kama Nyerere aliidhinisha kifo cha Mwamwindi tu hao tisa nani aliidhinisha?
 
Field Marshall ES,

FMES,

KUna yule mhindi aliyemuua Mkewe kwa kusukuma gari kwenye milima ya Kitonga, huyu alinyongwa wakati wa Mwalimu na si nyakati za Mwinyi!

Sasa tukirudi kwenye makala uliyosoma, Nyerere alikuwa anajutia kutia sahihi kunyongwa kwa Mwamwindi kwa kuwa alijua wazi kuwa hakupaswa kugadhibika kiasi hicho, na hicho ndicho kilichokuwa kinamsumbua.

Si kuwa hakutia saini kwenye hukumu nyingine, bali kwenye hili, alibaini kuwa haki na sheria zilifuata mkondo mmoja usio wa haki.
 
FMES,Rev.Kishoka,B-M-O,gm,

..kuna makosa ambayo ukipatikana nayo unaweza kuhukumiwa kunyongwa.

..katika sheria yoyote ile ya nchi kuna mkono wa Bunge[wananchi], na Raisi.

..binafsi sioni kama Mwalimu anastahili shutuma zozote zile kwa kuidhinisha hukumu za kunyongwa. zingatia neno kuidhinisha, kwasababu mahakama ndiyo mtoa hukumu.

..kama Mwalimu aliidhinisha hukumu yoyote ile ya kunyongwa ni kwasababu mahakama iliamua hivyo.

..kama kuna tukio ambao Mwalimu aliongeza adhabu na kuwa ya kunyongwa, then we definetely have something to talk about. kinyume chake naona tunabishana tuuu, bila sababu ya msingi.

NB:

..kuna wanaodai kwamba Mwalimu alikuwa akiichukia sana adhabu ya kunyonga.

..lakini ukweli unabaki kwamba iliendelea kuwepo, na ilitumika kwa uchache, wakati wote wa utawala wake.

..kwa msingi huo utaona, kwamba kuna some special cases ambazo Mwalimu aliona watuhumiwa wanastahili kunyongwa.

..WAISRAELI HAWANA HUKUMU YA KIFO, LAKINI WALIPOMKAMATA ADOLF HEICHMAN[sp?] KULE ARGENTINA, BUNGE LAO LILIIDHINISHA HUKUMU YA KIFO KWA AJILI YAKE.
 
FMES,

KUna yule mhindi aliyemuua Mkewe kwa kusukuma gari kwenye milima ya Kitonga, huyu alinyongwa wakati wa Mwalimu na si nyakati za Mwinyi!

Sasa tukirudi kwenye makala uliyosoma, Nyerere alikuwa anajutia kutia sahihi kunyongwa kwa Mwamwindi kwa kuwa alijua wazi kuwa hakupaswa kugadhibika kiasi hicho, na hicho ndicho kilichokuwa kinamsumbua.

Si kuwa hakutia saini kwenye hukumu nyingine, bali kwenye hili, alibaini kuwa haki na sheria zilifuata mkondo mmoja usio wa haki.

Hii ndio sawa na crying over spilt over milk, kwa sababu hata kama anajutia hicho kifo kimoja hawezi mrudisha jamaa na familia yake ilikuwa tayari imeathirika vibaya, angenyamaza tu na kuendelea na mambo yake huyu.
 
JokaKuu,

Huyo nazi aliitwa Adolf Eichmann, na ndiye hasa main architect wa ule mpango wa kuangamiza wayahudi ulioitwa "holocaust", ndiye aliyetunga na kuchora plani nzima na utaratibu wa utekelezaji wake. Alinyongwa huko Israel mwaka 1962 baada ya kukamatiwa Argentina na makachero wa Mossad.
 
Kuna holocast ingine rais wa Iran anataka kuileta hapa, pia anataka kuifutilia mbali Israel itoke katika ramani ya dunia!
 
Hii ndio sawa na crying over spilt over milk, kwa sababu hata kama anajutia hicho kifo kimoja hawezi mrudisha jamaa na familia yake ilikuwa tayari imeathirika vibaya, angenyamaza tu na kuendelea na mambo yake huyu.

Makes alot of sense, na ni the bottom line.
 
JokaKuu,

Jokakuu,

Kama Nyerere alichukia adhabu ya kunyongwa angeiondoa lakini katika historia nafikiri sijakutana na sehemu inayosema alijaribu hata kuiondoa hii katiba, kama bunge lingegoma kupitisha angetumia executive power, sina uhakika kama katika katiba yetu tuna executive power ila nafikiri inawezekana.
 
Jokakuu,

Kama Nyerere alichukia adhabu ya kunyongwa angeiondoa lakini katika historia nafikiri sijakutana na sehemu inayosema alijaribu hata kuiondoa hii katiba, kama bunge lingegoma kupitisha angetumia executive power, sina uhakika kama katika katiba yetu tuna executive power ila nafikiri inawezekana.

Bunge wakati huo lilikuwa ni rubber stamp..likiburutwa na Executive!
 
Kuna holocast ingine rais wa Iran anataka kuileta hapa, pia anataka kuifutilia mbali Israel itoke katika ramani ya dunia!

Mkuu kuna HOLOCUST kubwa mno inawamaliza wananchi wetu kila siku. Tofauti ni kwamba yenyewe tumeishaikubali kwamba iwepo tuu. Njaa, vita, magonjwa, umaskini nk..mi nadhani hiyo nayo ni holocust au genocide kabisa (ukiita ile ya Rwanda iliyomaliza watu million moja kwamba ni Genocide, je haya niliyoyataja hapa yanamaliza wangapi kwa mwaka?) sema tuu basi..tunaamua kutumia maneno pale tunapotaka ya-fit mawazo yetu. Bush akisema Iran, N Korea na Syria ni axis of evil..sisi tunasema Njaa, magonjwa na umaskini ndo axis of evil wa mwafrika!
 
Back
Top Bottom